Social Icons

Pages

Tuesday, November 18, 2014

SHAMBA LILITOLEWA NA ACU KUPIMWA UPYA

Naibu Waziri wa Ardhi, George Simbachawene.
Hatimaye Serikali imeingilia kati mgogoro wa uvamizi wa shamba la Chama Kikuu cha Ushirika Arusha (ACU), kwa kuagiza lipimwe upya ili ligawanywe kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Ardhi, George Simbachawene alitoa agizo hilo juzi alipozungumza na wananchi wa Kijiji cha Valesca ambao wiki iliyopita walivamia shamba hilo na kugawana.
Alisema hekali 1,500 za shamba hilo zilizotolewa na ACU ili zigawanywe, ni lazima zipimwe ili wanaohitaji ardhi wapewe.
Alisema kuna wanaomiliki eneo kubwa la ardhi ndani ya Shamba la ACU, hivyo ni lazima taratibu zifuatwe ili wapunguziwe na wengine wanufaike.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari aliunga mkono uamuzi huo kwa kuwa maelfu ya wananchi wa eneo hilo hawana ardhi.

CHANZO: MWANANCHI

No comments: