
Alitoa kauli hiyo wakati, akijibu hoja za wabunge waliochangia hoja zilizogusa wizara yake kuhusu mapendekezo ya serikali ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2015/16.
Alisema hatua hiyo ni kinyume cha utaratibu, kwani tangu lilipotokea kosa la benki hiyo nchini Cyprus na kufungwa, BoT ilichukua hatua, ikiwamo kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa suala hilo.
Waziri Saada alisema anashangazwa na hoja ya Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, ya kutaka gavana ajiuzulu kwa kosa, ambalo hajalifanya.
“Mheshimiwa Kafulila naona yupo sana na Gavana wa BoT. Sijajua mantiki yake ni nini kilichotokea Cyprus hadi kufikia Gavana wa BoT anahusikaje ajiuzulu? FBME imekuwa Suspected kwa Money laundering (ukatatishaji wa fedha), imetokea Cyprus Tanzania kuna branch (tawi), ambalo anayesimamia ni Gavana wa Benki Kuu, sasa inakuaje ajiuzulu kwa sababu ya jambo hilo?" alihoji Waziri Saada.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment