
Mdee alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Magu, Mwanza mjini juzi jioni ikiwa ni sehemu ya ziara ya Bawacha katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Magharibi.
Alisema ipo mikataba ambayo serikali tayari imekwishasaini, lakini kuna utata kati yake na wawekezaji na makampuni iliyosainiana nayo.
Alitaja mikataba hiyo kuwa ni mkataba wa ujenzi wa njia ya treni ya umeme ambao tayari serikali imekwisha saini na kampuni moja ya Kimarekani kupitia Wizara ya Uchukuzi.
Alisema licha ya Tanzania kusaini mkataba huo, lakini mkataba huo una utata kwa kuwa haijulikani na hata ikitafuta katika mitandao haipatikani kama ilivyo kwa kampuni nyingine.
Mdee alisema Watanzania wanawapenda wawekezaji, lakini ni vizuri uwekezaji huo ukafanywa kwa uwazi na kufanya uchunguzi wa kutosha kabla ya kuingia katika mikataba ili kuepusha matatizo yanayoweza kuigharimu nchi na kuiingiza katika matatizo kama ilivyokuwa kwa mikataba ya Richmond na mingine.
“Watanzania tunapenda uwekezaji waje kwetu, lakini ni lazima tuwafahamu uadilifu wao na kama ni salama au la na mikataba ifanywe kwa uwazi kwa sababu bila kufanya hivyo, tunaweza kuipeleka nchi yetu pabaya kama ilivyokuwa kwa Richmond na mingine,” alisema Mdee.
Pia, Mdee alisema Tanzania imekuwa ikiingia katika mikataba mibovu kwa sababu viongozi wamekuwa wepesi kukubali kwa ajili ya misaada kutoka mataifa makubwa.
     CHANZO:
     NIPASHE
    

No comments:
Post a Comment