Katibu
mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon anatarajia kuanzisha uchunguzi
kuhusu vitendo vya mashambulizi dhidi ya nyenzo za Umoja wa Mataifa
wakati wa mapigano ya Israel dhidi ya Gaza karibuni.
Ban Ki Moon ameliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kuwa uchunguzi huo utaangazia hatua ya wapiganaji wa Hamas kuhifadhi silaha katika maeneo yanayoshukiwa.
Katika tukio moja,makombora ya Israeli yaligharimu maisha ya watu waliokuwa wakipata hifadhi katika shule ya umoja w amataifa huko Gaza.
Hata hivyo Ban Ki amesema kuwa baada ya kufanya ziara yake huko Ghaza amejionea hali halisi ilivyo huko na kwamba inasikitisha kutokana na madhara ya mashambulizi ya mapambano ambayo yamekuwa yakitokea huko.
CHANZO: BBC Swahili

No comments:
Post a Comment