Social Icons

Pages

Wednesday, July 16, 2014

NCHI ZA BRICS YAZINDUA BENKI YA MAENDELEO

Rais wa Urusi Vladimir Putin, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Rais wa Brazil Dilma Rousseff, Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Africa Kusini Jacob Zuma katika picha ya pamoja  kwenye Mkutano wa 6 BRICS Julai 15, 2014. (Picha wa Reuters)

Viongozi wa kundi la nchi zinazoinukia kwa kasi  kiuchumi duniani lijulikanalo kama BRICS wamezindua benki ya maendeleo ya thamani ya dola bilioni 100 na mfuko wa akiba kuzisaidia nchi wanachama kukabiliana na migogoro ya muda mfupi ya kiuchumi. Hiyo ndiyo hatua ya kwanza madhubuti kuchukuliwa na kundi hilo linalojumuisha nchi za Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini katika kuelekea kuubadilisha mfumo wa kimataifa wa kifedha unaotawaliwa na nchi za magharibi. Benki hiyo ambayo itakuwa Shanghai   inalenga kufadhili miradi ya miundo mbinu katika nchi zinazoendelea. India itaendesha operesheni zake kwa kipindi cha miaka mitano ya kwanza ifuatiwe na Brazil na baadaye Urusi. BRICS waliamua kuchukua hatua za pamoja kujiimarisha kiuchumi na kifedha kufuatia kupungua kwa mitaji katika masoko yanayoinukia mwaka jana kulikosababishwa na kupunguzwa kwa fedha za kuchochea uchumi kwa nchi hizo kutoka kwa Marekani.
Chanzo: DW


No comments: