Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira
Kati ya mwaka 1964–1967, Wasira alisoma elimu ya
Sekondari katika Chuo cha Ukufunzi Uingereza (British Tutorial College)
na kuhitimu kidato cha nne.
Historia yake
Stephen Wasira alizaliwa mwaka 1945 katika Wilaya
ya Bunda, Mkoa wa Mara (ana miaka 70). Alisoma katika shule tatu
tofauti, ya kwanza ni Shule ya Msingi Bariri 1956-1959, ya pili ni Shule
ya Msingi Nyambitilwa 1960–1961 na kisha akamalizia Shule ya Msingi
Kisangwa mwaka 1962 - 1963.
Kati ya mwaka 1964–1967, Wasira alisoma elimu ya
Sekondari katika Chuo cha Ukufunzi Uingereza (British Tutorial College)
na kuhitimu kidato cha nne.
Wakati anasoma sekondari (1965–1967), pia alifanya
kazi akiwa msaidizi wa masuala ya maendeleo ya jamii na alipohitimu
kidato cha nne alianza kuitumikia Tanu akiwa katibu wa wilaya mwaka
1967-1973.
Mwaka 1975–1982 alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na
mwaka 1982 akateuliwa kuwa Ofisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania
Washington, D.C. Alipokuwa huko alisoma na kuhitimu Shahada ya Kwanza ya
Uchumi na Uhusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Amerika (American
University) kilichopo Washington DC mwaka 1982–1985.
Wasira alisoma Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa
Umma kati ya mwaka 1985–1986 na aliporejea nchini kuendelea na utumishi
wa uwakilishi wa wananchi, aliteuliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Pwani mwaka 1990-1991.
Kati ya mwaka 1993–1995 alisoma tena Shahada ya Uzamili ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Amerika.
Ndani ya chama chake CCM, amekuwa Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) tangu mwaka 2007 na mwaka 2012
akachaguliwa katika wadhifa huo na tena kwa kura nyingi kuwashinda
wajumbe wote wa Tanzania Bara. Lakini pia amekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu
ya CCM tangu mwaka 2011 na tena 2013 hadi sasa.
Mbio za ubunge
Wasira alianza utumishi wa ubunge akiwa na miaka
25, hii ilikuwa mwaka 1970 aliposhinda ubunge wa Jimbo la Mwibara na
akaongoza hadi mwaka 1975 huku Rais Julius Nyerere akimteua kuwa Naibu
Waziri wa Kilimo.
Mwaka 1985, Wasira aligombea na kushinda ubunge wa
Jimbo la Bunda (wakati huu likiwa limemeguliwa kutoka lilikuwa Jimbo la
Mwibara. Katika kipindi hiki aliteuliwa na Rais Mwinyi kuwa Naibu
Waziri wa Serikali za Mitaa na baadaye Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya
Mifugo mwaka 1989 hadi 1990.
Kipenga cha vyama vingi kilipopulizwa mwaka 1995,
Wasira alihitaji kuwaongoza wana Bunda lakini akaangushwa kwenye kura za
maoni za ndani ya CCM, aliyemwangusha ni Jaji Joseph Warioba (Waziri
Mkuu na Makamu wa Rais Mstaafu). Wasira hakuridhishwa na ushindi wa
Warioba na aliamua kuihama CCM na kwenda NCCR Mageuzi wakati huo ikiwika
na akachaguliwa kwa kura 18,815 dhidi ya 17,527 za Warioba na hivyo
akawa mbunge kupitia NCCR.
Mbio za urais
Nguvu yake
Warioba alikata rufaa Mahakama Kuu nayo ikatengua ubunge wa
Wasira mwaka 1996 baada ya kujiridhisha kuwa kulikuwa na rafu nyingi
zilizofanyika ikiwamo matumizi ya rushwa na ikampiga marufuku kugombea
kwa miaka kadhaa. Wasira alikata rufaa mara kadhaa na kushindwa.
Mahakama ya Rufaa ilikubaliana na hukumu ya Mahakama Kuu.
Uchaguzi wa marudio ulipofanyika mwaka 1999 Wasira
alikuwa amekwishatangaza kuihama NCCR kutokana na siasa za ugomvi na
mara hii alimuunga mkono mgombea wa UDP, Victor Kubini lakini mara baada
ya uchaguzi huo aliamua kurejea CCM. Miaka mitano iliyofuatia (2000 –
2005) na hata minne iliyopita (1996 – 2000), Wasira alijielekeza katika
biashara ya kusafirisha mazao ya bahari nje ya nchi.
Alirejea katika ulingo wa siasa mwaka 2005 na
kushinda kura za maoni ndani ya CCM na akapitishwa kugombea ubunge wa
Bunda na akapita bila kupingwa. Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Waziri
wa Maji Januari 2006- Oktoba 2006.
Kati ya Novemba 2006 – Novemba 2010 alikuwa Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, lakini Februari–Mei 2008 aliwahi
kutumikia kwa muda Ofisi ya Waziri Mkuu akiwa Waziri wa Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Katika uchaguzi wa mwaka 2010, Wasira aligombea
tena ubunge wa Bunda na kushinda kwa asilimia 66.1 na Rais Kikwete
akamteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu kabla ya
mwaka huu kurudishwa kuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.
Mbio za urais
Wasira ni miongoni mwa wana CCM ambao bado
hawajatangaza rasmi kuwania nafasi hiyo, lakini amewahi kunukuliwa mwaka
jana akisema yupo tayari kwa hilo. Aliwahi kufanya mahojiano na gazeti
moja la kila wiki, Septemba 2014 na kuthibitisha kuwa ataomba ridhaa
hiyo kwa kile alichokiita “maombi mengi kutoka kwa wanaCCM wanaoona
anaweza kukabiliana na changamoto zinazolikabili Taifa katika wakati
huu”
Wasira amenukuliwa akithibitisha jambo hilo kwa
kusema “Kwa kifupi, nimekwishashauriwa sana, lakini nasubiri ruhusa ya
kanuni za chama. Kwa kweli kwa kiasi kikubwa nimeshafikia uamuzi wa
kugombea. Nitagombea kupitia CCM.”
Nguvu yake
Wasira ni mmoja wa mawaziri maarufu katika
Serikali ya Kikwete, mwonekano wake, vituko vyake, uongeaji wake na kila
anachokifanya, kinamtofautisha mno na wenzake. Umaarufu huu una maana
kubwa kwa mtu anayehitaji kuongoza nchi, kufahamika ni muhimu na hili
ameshalivuka.
Pili, amekuwa na rekodi nzuri ya kiutendaji katika
awamu zote alizopitia. Uchapakazi, ufuatiliaji na usimamizi ni moja ya
sifa kubwa za Wasira kwa watu waliofanya naye kazi. Rekodi hii pia
inamuongezea alama muhimu.
Tatu, amekuwa mhimili muhimu wa Serikali ya
Kikwete na ndiyo maana ili kujipunguzia mzigo wa kazi na kuhitaji mtu
mwenye uwezo wa kufanya uamuzi katika Ofisi ya Rais, Kikwete alimteua
kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu. Wasira anakuwa
mmoja wa watu walio karibu sana na Rais Kikwete kushinda watu
wanavyofikiria. Hii ni nguvu nyingine muhimu kwake.
Udhaifu wake
Nini kinaweza kumfanya apitishwe
Mwisho Wasira ni mcheshi na ni mtu wa kawaida sana. Kwa
wanaomfahamu wanajua kuwa hajajitengenezea “himaya binafsi”, uwezo wa
kifedha wenye kuibua shaka na mambo mengine kama hayo. Maisha haya ya
kawaida yanamfanya awe mmoja wa viongozi wa kawaida. Lakini zaidi ya
yote, anapenda mijadala, kubishana na kushindanisha hoja na ni rahisi
hata kuwamudu vijana.
Udhaifu wake
Kauli za vitisho na zinazoashiria udikteta. Moja
ya udhaifu mkubwa wa Wasira ni kupenda kudharau haki, hoja na hata madai
ya watu wengine. Mathalani, zilipotokea vurugu kadhaa katika mikutano
ya vyama vya siasa zikihusisha polisi kuzuia shughuli za vyama hivyo na
baadaye mapambano ya polisi na raia na labda raia kuuawa, Wasira
alijitokeza hadharani na kushangaa kwa nini Msajili wa Vyama vya Siasa
hajavifuta, ilhali akijua kwamba waliozuia mikutano ya vyama kinyume na
sheria inavyotaka ni Polisi na walioua Raia ni polisi. Kauli hizi
zinaashiria kuwa Wasira ni mtu anayeamini katika dola zaidi kuliko haki
na mustakabali wa wananchi.
Jambo jingine ni “ubishi na ujuaji”. Ukimsikiliza
Wasira katika vyombo vya habari, bungeni na kwingineko, unaona kabisa
kuwa kauli zake mara zote hazitolewi kujibu maswali yaliyoulizwa au
kutatua matatizo yaliyopo, bali maswali hayo huishia kuuliza maswali
mengine kwa kejeli na weledi mkubwa wa kiuzungumzaji.
Kwa mfano, alipoulizwa na mwandishi mmoja wa
habari juu ya kuteswa na kuumizwa kwa Absalom Kibanda, Wasira alijibu:
“…Kibanda ni nani katika siasa za vyama vingi Tanzania hadi Serikali
imsake na kumtesa? Yeye siyo Mbowe, Slaa au Lipumba. Hata kama Serikali
ingeamua kupambana na maadui zake Kibanda bado hawezi kufuzu kwa sababu
yeye hayuko chama cha upinzani.”
Unaweza kuona kuwa mwandishi amemuuliza swali
muhimu ambalo lilihitaji ufafanuzi mkubwa wa Serikali, badala ya
kulijibu, anaanza kumshusha Kibanda na kuonyesha kuwa si lolote wala
chochote katika ulingo wa raia muhimu katika nchi.
Wangapi tunajua mchango wa Kibanda katika
kusimamia ukuaji wa haki za vyombo vya habari na waandishi wa habari
Tanzania? Kwa nini waziri mwenye hadhi ya Wasira haanzi hata kusema
alivyosikitishwa kutokana na kuumizwa vibaya kwa mhariri huyo mwandamizi
na badala yake anaanza kuonyesha kuwa “Kibanda si lolote”. Kauli hizi
zisidharauliwe hata kidogo, ndizo zinapaswa kuwagutusha wananchi kujua
aina ya viongozi wao wanaohitaji kuongoza dola.
Nilikuwa najiuliza, Kama kesho Wasira akiwa Rais
wa nchi hii halafu mwandishi mwingine ameuawa au kuumizwa, atajibu nini?
Unaposhindwa kuwa mwaminifu na mlinzi wa maisha na haki za watu
unapokuwa mdogo, huwezi kujifunza kufanya hivyo utakapokuwa mkubwa.
Nini kinaweza kumfanya apitishwe
Kama Wasira atapitishwa na CCM, basi uzoefu wake
ndani ya chama hicho na Serikali itakuwa moja ya silaha zilizomvusha.
Uzoefu wa Wasira ndani ya CCM na Serikali wa miaka zaidi ya 50,
unambeba. Huyu anaweza kuwa waziri mwenye uzoefu mkubwa katika Baraza la
Mawaziri la Kikwete kuliko mwingine yeyote. CCM ikihitaji mtu mkongwe
ili awe mgombea wake bila shaka Wasira ndiye atakuwa moja ya chaguo
muhimu.
Lakini pia, Wasira anaungwa mkono na makundi
hasimu ndani ya CCM. Mara kadhaa imeelezwa namna makundi hasimu
yanavyovutana kiasi cha kutishia uhai wa mbele wa chama hicho. Bahati
aliyo nayo Wasira ni kuwa mmoja wa watu ambaye anaheshimiwa mno na
makundi husika. Kama CCM itahitaji kutuliza hali ya ndani ya chama chake
kwa kupata mtu ambaye hatatumia nguvu kubwa kuyaunganisha makundi
hasimu, basi Wasira ni mmoja wao.
Kwa kiasi fulani, Wasira ana uwezo mkubwa wa
kushughulikia masuala ya kimataifa. Hata nchi yetu ilipopata ugeni
mkubwa wa Rais Barack Obama wa Marekani, nimeambiwa kuwa ni Wasira ndiye
aliyekabidhiwa jukumu kubwa la kuwa karibu na wageni muhimu na
kuwaelekeza masuala muhimu.
Nini kinaweza kumwangusha?
Asipopitishwa (Mpango B)
Hitimisho
Kuna taarifa kuwa kulitokea manung’uniko kwa baadhi ya mawaziri
wengine ambao waliona kama Wasira anapewa “promo” kubwa japokuwa taarifa
ya chanzo kimoja cha Ikulu inasema; “mzee (yaani Kikwete) anamuamini
sana Mzee wa Wasira na ni mshauri wake mkuu, ndiyo maana alipewa umuhimu
mkubwa kwenye ujio wa Obama.”
Jambo jingine linaloweza kumvusha ni kuwa mmoja wa
viongozi wasio na kashfa za wizi wa fedha za umma. Kama ndivyo basi
unaweza kusema kuwa uadilifu wake nao siyo wa kutiliwa shaka. Hata
dhoruba zote ambazo zimeikumba Serikali ya Kikwete tangu mwaka 2005 na
kila mara akibadilisha mawaziri na manaibu wao, Wasira ameendelea kuwa
na namba ya kudumu. Moja ya vitu vinavyombeba ni uaminifu na kujua kazi
yake. Hili nalo linaweza kuifanya CCM ihitaji mtu wa namna yake.
Japokuwa, tuhuma za kutoa rushwa Bunda mwaka 1995, haziwezi kufutika.
Nini kinaweza kumwangusha?
Mambo kama matatu hivi yanaweza kumwangusha Wasira.
La kwanza ni dhana ya ukigeugeu. Mwaka 1995
aliposhindwa kura ya maoni ndani ya CCM kule Bunda, alihamia NCCR na
kushinda ubunge. Kwa hivyo, yeye ni mmoja wa wana CCM waliowahi kukihama
chama hicho kabla hawajarejea tena baadaye. Katika rekodi ya marais
walioongoza nchi hii kupitia CCM, hapakuwahi kuwa na mmoja ambaye
aliwahi kuhama chama chake na baadaye akarejea kisha akapewa nafasi ya
kugombea urais. Kuna baadhi ya wana CCM wahafidhina wanamtizama kama mtu
anayeweza kufanya uamuzi wowote ilimradi aendelee kuwa kiongozi. Kwa
sababu ya kasumba hii, Wasira anaweza kujengewa hoja ya uimara wake wa
kudumu ndani ya CCM kisha akaondolewa.
Lakini pili, Wasira si mtu mwenye nguvu ya pesa.
Kwa wanaomfahamu wanalijua hili. Nimeshaeleza kuwa hadi sasa hana
mitandao ya kifedha inayomuunga mkono na ili upite na kugombea urais kwa
CCM ya sasa unahitaji kuwa na fedha za kutosha, hakuna maajabu mengine.
Sioni kama Wasira ana ubavu wa kuvuka kizingiti hiki ili walau awe
mmoja wa wagombea wenye nguvu na watakaoonekana kwenye mchujo wa mwisho.
Umri mkubwa ni jambo jingine muhimu. Tanzania
haikuwahi kuwa na Rais ambaye anamaliza miaka yake 10 akiwa na miaka 80.
Ikiwa CCM itampitisha ndiyo itakuwa mara ya kwanza tunaongozwa na mtu
ambaye anamaliza akiwa kikongwe kabisa, nadhani haitakuwa tayari kwa
hilo. Kwa changamoto za nchi hii ambazo zinahitaji watu wenye nguvu,
ubongo unaofikiri sawasawa, wanaoweza kujisomea na kutafakari kila jambo
– nadhani Wasira pia anaweza kuangushwa na kipengele hiki.
Asipopitishwa (Mpango B)
Tayari Wasira anaonekana kuwa ana mpango thabiti
mkononi ikiwa hatagombea urais, mpango wake ni kurejea Bunda na kugombea
ubunge kwani amekuwa mkali mno kila washindani wake (Esther Bulaya
kutoka CCM, Dk Lucas Webiro na makada wengine kadhaa kutoka Chadema),
wanapoonyesha kufanya harakati jimboni humo na hasa wanapoonyesha kuwa
hajafanya jambo kubwa kwa watu wa Bunda. Lakini kwa sababu yeye ni
mjasiriamali, namuona pia akiwa na chaguo la kurudi kufanya biashara na
kupumzika majukumu na mikikimikiki ya umma na au kuendelea kuishauri
Serikali na kuhamasisha maendeleo mkoani Mara, akiwa mtu aliyekaa
serikalini muda mrefu.
Hitimisho
Ukweli ni kuwa, nafasi ya Wasira katika uwanja wa
kisiasa za kitaifa na hata ndani ya Jimbo la Bunda kwenyewe ni ndogo
sana. Kama hatasoma alama za nyakati hata ndani ya jimbo nadhani vijana
watamuadhiri aidha, ndani ya kura za maoni za CCM au ataangushwa na
mgombea kijana wa Ukawa ikiwa bado CCM itampitisha.
Katika safari hii ya urais simuoni akifika mbali
lakini lolote linaweza kutokea. Jambo la msingi ni kuwa, namtakia kila
lililo jema katika kufikia malengo aliyojipangia.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment