Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi kwenye
Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma alipotangaza nia ya kugombea urais
kupitia CCM jana.
Naibu Waziri wa
Fedha, Mwigulu Nchemba ametangaza nia yake ya kugombea urais kupitia CCM
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba akieleza jinsi atakavyoivusha Tanzania
kuwa nchi yenye uchumi wa kati utakaopatikana kwa kutoa haki kwa watu
wote.
Akitangaza nia hiyo jana kwenye Ukumbi wa Mwalimu
Nyerere katika Chuo cha Mipango Dodoma, Nchemba alisema: “Ahadi yangu
kubwa kwenu ni kwamba nitawavusha. Nitawavusha wanaCCM wenzangu pamoja
na Watanzania kwa ujumla wakati ni sasa tunataka Taifa letu lifike kuwa
nchi yenye uchumi wa kati,” alisema Nchemba na kuongeza: “Ninachoomba kutoka kwenu, mniamini na mniunge
mkono katika hili… nitawavusha. Lakini tukumbuke kwamba kila mmoja
lazima atimize wajibu wake katika utendaji kazi ili tufikie huko
tunapotaka kufikia.”
Nchemba aliyekuwa ameongozana na mkewe, Neema na
watoto wake watatu, Isaack, Grecious na Joshua pamoja na ndugu jamaa na
marafiki, alisisitiza kuwa ili kufikia malengo hayo, lazima nchi iwe na
mfumo wa uwajibikaji utakaowezesha kulinda rasilimali za Taifa na
kuongeza Pato la Taifa.
Huku akitumia kauli mbiu ya ‘Mabadiliko ni
Matendo, Wakati ni Sasa’, ambayo ataitumia katika safari yake ya
kuelekea Ikulu, Nchemba aliyetumia dakika 115, kuanzia saa 10.10 jioni
hadi saa 11.25 jioni, alisema atapambana na tabia za watu kufanya kazi
kwa mazoea, rushwa, ufisadi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano
atakayoiongoza endapo atachaguliwa, itakuwa ya uadilifu na uaminifu.
Alisema iwapo atachaguliwa, ataifanya nchi kuwa ya
kipato cha kati sambamba na watu wake, kujenga Taifa linalojitegemea
kibajeti na kuwajengea uwezo wananchi kumiliki uchumi wao wenyewe.
Huku akieleza jinsi atakavyomaliza kilio cha
ukosefu wa ajira, wanafunzi, wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara na
watu wa kada mbalimbali nchini, Nchemba alianza hotuba yake kwa
kuwashukia baadhi ya watu wenye dhana potofu juu ya mtu anayestahili
kuwa rais wa nchi.
“Nimeamua kutangazia nia hapa Dodoma kwa sababu
ndipo makao makuu ya nchi na kama nikiwa rais nitaapishiwa hapa. Pia
sikutaka kutangazia nia nyumbani Iramba ili kuondokana na umimi,”
alisema na kushangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo.
Awajibu wanaomponda
“Uzoefu ni mazoea ya starehe. Mtu aliyekaa katika uongozi ni mtu aliyesahau shida za Watanzania.
Jambo la kwanza na la msingi ni kuitambua ajenda
ya Watanzania, Watanzania watamuunga mkono kiongozi kwa kuitambua ajenda
yake,” alisema.
Alisema wakati akijitathimini kutangaza nia ya
kugombea alikuwa akifahamu ajenda ya Watanzania, huku akisisitiza kuwa
umaskini hakuusoma katika vitabu, bali amekulia katika maisha ya
kimaskini.
Mipango yake
“Ukizungumzia ukosefu wa ajira na dawa hospitali hilo sijalisoma
vitabuni, ukizungumzia ajira kwa vijana na watu wote hilo jambo
sijalisoma vitabuni.”
Alisema katika pitapita zake, amesikia habari za
mtu anayefaa kuwa rais zikihusishwa na umri na uzoefu, “Ujana na uzee
haviwezi kuwa sifa ya kuiongoza nchi. Kukaa serikalini muda mrefu
haiwezi kuwa sifa ya kutosha kuliongoza Taifa hili, unaweza ukakaa sana
serikalini lakini ukasababisha hasara kubwa. Hata kuishi ni hivyohivyo,
kinachoangaliwa si kuishi miaka mingi, bali ni kipi ulichokifanya. Leo
hii marehemu (Edward) Sokoine hakumbukwi kwa sababu alikaa sana
serikalini, anakumbukwa kwa matendo yake kwa kipindi kifupi alichokaa
serikalini.”
Huku akishangiliwa alisema, “Kiongozi akipatikana
kwa mazoea atafanya kazi kwa mazoea. Vita ya kwanza tunayotaka
kuikomesha katika nchi yetu ni kufanya kazi wa mazoea. Tunahitaji mambo
matatu; mabadiliko, mbinu za kufanya mabadiliko na utayari wa kufanya
mabadiliko.”
Kuhusu umri alisema: “Wengine wanaongelea umri
wamesahau kuwa Katiba inasema umri wa kugombea ni miaka 40, hata vitabu
vitukufu vimeandika kwamba umri wa miaka 40 ni sahihi mtu kupewa utume
na unabii, Mussa alipofikisha miaka 40 aliaminiwa kwenda kuwakomboa
ndugu zake.”
Alisema hata Mwalimu Julius Nyerere alikuwa rais akiwa na miaka 40, tena akitoka kufundisha sekondari.
“Watu wanataka kuwatoa Watanzania katika ajenda
kwa kuzungumzia vitu vyepesi. Eti wanasema ukimaliza kuwa rais wakati
bado kijana utafanya nini. Nifanye nini tena wakati nitakuwa
nimeshamaliza kazi. Najipambanua kwa ajenda yangu na wale
watakaoniangalia wataangalia ajenda yangu,” alisema.
Mipango yake
“Kwa miaka 50 tumekuwa tegemezi, sasa imetosha
tunakwenda kujitegemea. Kujitegemea ni kila mmoja kulipa kodi
anayostahili,” alisema.
Alisema wakati wa watu wachache kubeba mzigo wa
kodi umefikia mwisho na kwamba kila mtu anayestahili kulipa atailipa,
awe mdogo au mkubwa.
“Tunakwenda kuachana na utaratibu wa kukimbizana
na wauza vitumbua kuwadai kodi. Kujitegemea ni nidhamu ya matumizi na
sasa tunakwenda kuziba mianya ya rushwa,” alisema.
Alisema ili uchumi umilikiwe na Watanzania
wenyewe, lazima njia za kuwapatia watu kipato ziboreshwe kwa sababu
uchumi wa nchi unakua lakini wananchi bado wanalia umaskini.
“Njia ya kuwatoa hapo walipo ni kuongeza thamani
ya mazao na kazi wanazozifanya kwa sababu asilimia 70 ya Watanzania ni
wakulima. Lazima wakulima watafutiwe pembejeo na masoko. Tunatakiwa
kutumia sekta binafsi ili kuwa na viwanda vingi nchini,” alisema na
kutoa mfano:
Rushwa
Kufanya kazi kwa mazoea
“Pamba ya Tanzania inaweza kutumika kutengeneza sare za shule,
za jeshi na viatu kutoka katika viwanda vilivyopo nchini. Tuna wanafunzi
zaidi ya milioni nane na kila mwaka wanaandikishwa shule, kwa nini
tulilie soko la nje halafu sare zao tunanunua nje.”
Kuhusu mafuta, Nchemba alisema kilimo cha alizeti
kikiboreshwa kitazalisha ajira nyingi na hilo linaweza kufanyika pia
katika sukari, kahawa, chai na korosho.
“Awamu ya tano, nchi itaingia katika uchumi wa viwanda na vijana watafanya kazi kwa kupokezana,” alisema.
Mwigulu aligusia suala la Watanzania kutozwa kodi
zisizokuwa na kichwa wala miguu na zisizoendana na uzalishaji wa
biashara husika, huku akitolea mfano mama ntilie na wamachinga.
“Wakubwa wakitaka kuwekeza wanapewa likizo ya
miaka 10 ya kulipa kodi lakini anayefungua saluni anatozwa kodi wakati
akiwa anapaka rangi jengo hata biashara hajaanza,” alisema na
kushangiliwa.
Rushwa
Akizungumzia rushwa alisema: “Rushwa hupofusha
macho ya wenye akili na kurejesha nyuma maendeleo na hupindisha ukweli
na kuwanyima haki maskini.”
Alisema awamu zote nne za Serikali zimejitahidi
kupambana na rushwa, ila awamu ya tano itakuja na njia tofauti kwamba
atakayethibitika kupokea au kutoa rushwa atachukuliwa hatua haraka ili
iwe fundisho.
“Sasa hivi mtu akikamatwa na rushwa kesi zimekuwa
na mlolongo mrefu. Tutabadilisha Sheria namba 11 ya Kupambana na Rushwa
ili kuipa meno Takukuru iweze kushughulika na suala hili na
atakayebainika atafilisiwa, kufukuzwa kazi na kufungwa,” alisema.
Alisisitiza: “Habari ya mtu kula rushwa ya fedha
nyingi na kuondolewa katika cheo chake ni sawa na kumpa likizo, ni sawa
na kumfanyia ‘send off’ kwa fedha za walipakodi.”
Kufanya kazi kwa mazoea
Akizungumzia suala la kufanya kazi kwa mazoea
alisema: “Serikali ya awamu ya tano itaondokana na ukiritimba unaoondoa
ufanisi. Hakutakuwa na ucheleweshaji wa kutoka kwa ajira kwa kisingizio
cha kibali. Nchi hii ina upungufu wa wafanyakazi kila wizara na taasisi.
Kura za wanaCCM
Lazima ufanyike utaratibu wa kujua idadi ya vijana wasio na kazi
ili waweze kupatiwa nafasi. Inakuwaje mtu anastaafu halafu unasema
hakuna wa kuziba pengo lake!”
Alisema anazungumzia uchumi kwa sababu ameusomea
na kusisitiza, “Kuna matatizo kwenye mgawanyo wa keki ya Taifa. Leo hii
watu wakipewa dhamana ya kusimamia shirika la umma wanachokifanya ni
kutafuna fedha za walipakodi. Jambo hili haliwezekani maana kuna
wajawazito wanalala chini.”
“Haiwezekani sungura akawa mdogo kwa baadhi ya
Watanzania na sungura huyohuyo akawa mkubwa kama tembo kwa baadhi ya
Watanzania. Haiwezekani shirika la umma wakalipana posho za juu huku
watoto wa maskini wanakosa mikopo. Nitakomesha rushwa kwa kuzingatia
masilahi ya wafanyakazi,” alisema.
Alisema ni wakati wa Tanzania kuwa nchi ya viwanda
na katika kuthibitisha hilo, hayatafanyika makosa tena katika uwekezaji
wa gesi kwa kuweka wazi mikataba na fedha zitakazotokana na mauzo ya
gesi lazima zihifadhiwe katika akaunti za benki za ndani ya nchi.
Kuhusu elimu na afya, alisema sasa umefikia mwisho wa wananchi kununua dawa. “Kila anayeugua anaambiwa akanunue dawa lakini
kila mwaka mnasikia Serikali inadaiwa fedha za dawa. Katika hili
tutadhibiti kila kitu ikiwamo wale wanaoiba dawa na tukimbaini
tutamnyang’anya leseni yake na atakwenda jela,” alisema.
Kuhusu elimu alisema: “Miaka mitatu ijayo tutakuwa
na wanafunzi wengi na tutahitaji zaidi ya Sh700 bilioni kwa ajili ya
mikopo, kazi iliyopo mbele yetu ni kuweka chanzo maalumu kwa ajili ya
elimu ya juu ili mtoto yoyote mwenye sifa asikose nafasi ya kwenda chuo
kikuu kwa sababu tu ya kukosa mkopo.”
Pia aligusia suala la kuimarisha ulinzi na usalama
na Muungano ambao alisisitiza kuwa ni lazima ulindwe na kuifanya
Zanzibar kuwa na uchumi wa viwanda.
Katika hotuba yake, Mwigulu alisema ili kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji ni lazima kugawa ardhi kwa kila upande.
Kura za wanaCCM
Katika hotuba yake Nchemba aliwaangukia wanachama
wa CCM akisisitiza kuwa amejitathimini vya kutosha na anaweza kukiongoza
vyema chama hicho na Watanzania wote.
“Ahadi yangu kubwa kwenu ni kwamba nitawavusha.
Kabla ya kufika kwa Watanzania nitaomba ridhaa ya wanaCCM. Ninakijua
chama hiki na ahadi yangu kwenu nitawaunganisha wanaCCM na Watanzania
wengine,” alisema. “Tunakwenda kukomesha kufanya kazi kwa mazoea na kusimamia
rasilimali na kuweka usawa, haya ndiyo tunasema ni mabadiliko kwa
vitendo na wakati wa kufanya hayo ni sasa. Taasisi zote za usimamizi
nafasi zake zitapatikana kwa ushindani,” alisema. “Anayeanzisha kibanda cha kibiashara lazima
aandaliwe mazingira ya biashara yake. Tunawahamisha wamachinga kwa
kigezo cha kusafisha jiji utadhani wao ni uchafu. Ukiwaondoa wakati
walikuwa wakifanya kazi halali watarudi na kufanya kazi zisizo halali,”
alisema.
Ajibu maswali
Ilivyokuwa
Alisema anaomba ridhaa kwa wanaCCM ili akafanye
kazi mapinduzi katika Taifa na kuleta haki, heshima na upendo katika
eneo lililotawala na chuki. “Naomba mambo matatu, kwanza mniamini, mniunge
mkono na jambo la tatu nitawavusha. Kwenye vita ya umaskini mimi ni mtu
sahihi, wakati sahihi na muda sahihi ni sasa,” alisema.
Ajibu maswali
Alipoulizwa kuhusu hotuba yake ya kama
haimhatarishii mbio zake za kuelekea Ikulu, Nchemba alisema hana shaka
na chama chake wala Watanzania na ndiyo maana amesema atawavusha.
Kuhusu atakavyoshughulikia rushwa kubwa kama za
EPA, Meremeta na Escrow ambazo watuhumiwa wake wameonekana wakitanua na
fedha hizo, alisema sifa moja ya mtu anayeweza kupambana na rushwa ni
yeye kutokuwa mla rushwa.
Alisema iwapo atapata ridhaa ya Watanzania, rushwa
litakuwa ni janga na hivyo litashughulikiwa kama tatizo maalumu...
“Adhabu kali itatolewa ili mtu asirudie tena kufanya hivyo.”
Alisema siyo rushwa kubwa tu, bali nyingine
zinazotokana na ununuzi wa umma ambao watu wamekuwa wakipandisha juu bei
ya bidhaa... “Hatutakuwa na uvumilivu katika mazingira haya.”
Ilivyokuwa
Kuanzia saa 7.00 lango la ukumbi wa Mwalimu
Nyerere katika Chuo cha Mipango na Maendeleo ulikuwa wazi na idadi kubwa
ya watu walianza kuingia wengi wakiwa vijana kutoka mikoa ya Dodoma na
Singida huku kukiwa na idadi kubwa ya viongozi wa dini.
Wabunge waliohudhuria ni Ally Keissy, Omary
Badwel, Modestus Kilufi, Martha Mlata, Asumpta Mshama na baadhi ya
wabunge kutoka Zanzibar.
Mbali na madiwani, makatibu na wenyeviti wa CCM kata na mitaa
kwa Manispaa ya Dodoma, Katibu wa CCM Mkoa Albert Mgumba na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM, Anton Kanyama.
Wengi wa vijana waliovaa fulana za rangi za Bendera ya Taifa huku wengi wakivaa skafu kama anavyovaa wakati wote Nchemba.
Baba mzazi wa Mwigulu, Mzee Madelu Nchemba na mama
yake, Asha waliongoza wanafamilia ya Naibu Waziri huyo kutoka Kijiji
cha Makunda Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Nje ya ukumbi, mabango yaliyojaa picha zake
yalipambwa zikiwa na maandishi, “Mabadiliko ni kwa vitendo, wakati ni
sasa,” ambayo wengi walikuwa wakipiga picha hapo. Mengine ni kupanga ni
kuchagua na kutenda ni kwa vitendo, wakati ni sasa.
Mabango yaliyobebwa na vijana yalikuwa na ujumbe
mbalimbali ukisomeka, Mwigulu mkombozi wa Watanzania 2015, Mwigulu ni
Sokoine aliye hai 2015 njia ni nyeupe.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment