Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amewataka wananchi
kuwapima wanaotangaza nia ya kugombea nafasi za urais kama wana maadili
ya dhati katika kutokomeza rushwa.
Akizindua Tamasha la Ulamaa la Qaswida katika
shule ya Benjamen Mkapa jana, Membe alisema uongozi wa heshima ni ule
wenye kuzingatia maadili na unaochukizwa na vitendo vya rushwa.
Alisema rushwa ni kero kubwa kwa wananchi, hivyo viongozi waadilifu pekee ndiyo wanaoweza kumaliza tatizo hilo. “Wachujeni viongozi wanaotangaza nia ya
kuwaongoza, muwapime kama wana maadili ya kutosha, wapimeni kama siyo
wala rushwa,” alisema na kuongeza:
“Rushwa ni tatizo kubwa, viongozi wasio na maadili
hawawezi kumaliza tatizo la rushwa. Angalieni ni viongozi gani wenye
sifa na maadili.”
Membe alisema watangaza nia hao wanapaswa kupimwa na wananchi hadi kwenye dini zao kama ni watu safi ambao wanafaa kuwaongoza.
Alisema ni vyema wananchi wakatumia muda wa
kuwapima viongozi hao katika mambo mbalimbali na kuepuka kuwa wepesi wa
kusikiliza kauli na kuzikubali. “Uongozi wa heshima ni ule wenye maadili. Viongozi
bora ni wale watakaochukia vitendo vya rushwa kwa nguvu zote, jamii
imechoka kushuhudia vitendo hivi vinavyonyima haki,” alisema waziri huyo
wa Mambo ya Nje.
Katika tamasha hilo, Membe aliahidi kuchangia
kiasi cha fedha ambacho alikataa kukitaja akisema yeye si mtu wa
kutafuta umaarufu katika masuala kama hayo. “Nitachangia katika tamasha hili, lakini sitasema
hadharani ni kiasi gani kwa sababu sitafuti umaarufu mwepesi kupitia
hela,” alisema.
Kuhusu ndoto yake ya urais, Membe alisema Juni 7,
mwaka huu wananchi wakae kwenye runinga zao kwani atatangaza nia ya
kugombea urais na kuomba ridhaa kwa CCM. Tayari makada wengine wa CCM
wameshaweka hadharani dhamira yao ya kuwania kiti cha urais katika
Uchaguzi Mkuu baadaye mwaka huu.
Tayari Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa
amezindua mbio hizo mwishoni mwa wiki mjini Arusha na Naibu Waziri wa
Fedha Mwigulu Nchemba alizindua jana mjini Dodoma.
Mwingine aliyezidua nia jana ni Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Wasira mjini Mwanza. “Siku hiyo nitawaeleza wananchi namna nitakavyoitoa nchi hapa ilipo na kuipeleka katika nchi yenye neema,” alisema Membe. Awali, Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa, Jumanne Ligotola aliwataka wananchi kulinda amani na utulivu kwa gharama zozote.
CHANZO: MWANANCHI
Mwingine aliyezidua nia jana ni Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Wasira mjini Mwanza. “Siku hiyo nitawaeleza wananchi namna nitakavyoitoa nchi hapa ilipo na kuipeleka katika nchi yenye neema,” alisema Membe. Awali, Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa, Jumanne Ligotola aliwataka wananchi kulinda amani na utulivu kwa gharama zozote.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment