Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia.
Akizungumza na NIPASHE, Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema suala la mvutano katika majimbo hayo aulizwe siku ya leo. “Nashukuru kwa swali hilo, lakini naomba uniulize Jumatatu nitakuwa na jibu kamili,” alibainisha Mbatia.
Mwanzoni mwa Mei, mwaka huu, vyama vinavyounda Ukawa vya Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF vilikutana kwa saa 48 kujadili namna ya kusimamisha mgombea mmoja katika kila kata, jimbo na urais.
Viongozi hao walieleza kuwa wamefikia muafaka katika majimbo 227 kati ya 239 na kwamba ni sawa na asilimia 95 katika majimbo ya uchaguzi.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment