Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed.
Kashfa ya Escrow imeibuliwa upya bungeni baada ya
wabunge kudai kuna kampuni ya Simba Trust inayomiliki asilimia 50 za
kampuni ya Pan Africa Power (PAP), ambayo inadaiwa kuhusika katika
ufisadi wa uchotwaji wa zaidi ya Sh.bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta
Escrow.Hayo yaliibuliwa jana bungeni na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
wakati wa kuwasilisha hotuba yake ya kambi hiyo kuhusu makadirio ya
mapato na matumizi ya mwaka 2015/2016 ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Msemaji wa kambi hiyo, Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed,
alisema wakati umma wa Watanzania unataka kuelewa wamiliki wa kampuni ya
Simba Trust lakini katika hali ya kushangaza Wakala wa Usajili wa
Biashara na Leseni (Brela), umegoma kutoa majina ya wamiliki wa kampuni
hiyo.
“Kambi rasmi ya upinzani tunaitaka serikali ieleze kwanini taasisi
hii ya Brela iliyo chini ya wizara hii bado inakataa kutoa majina ya
wamiliki wa Simba Trust, imekuwa kama ilivyokuwa makampuni yaliyohusika
na uchotaji mabilioni ya Epa na fedha za mradi wa Meremeta,” alisema.
Mnyaa alisema hatua ya Brela kukataa kutoa majina ya wamiliki wa
kampuni hiyo kuna unganisha na dhana kwamba wamiliki wa kampuni hiyo ni
viongozi wandamizi wa serikali ya CCM.
Alisema matatizo ya kiutawala yaliyopo katika sekta ya umma nchini
yamesababisha sekta ya viwanda kushindwa kujiendesha kiushindani.
Aliongeza kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la na Elimu, Sayansi na
Utamaduni (Unesco), limebainisha kuwa viwanda vingi vinaendeshwa kwa
hasara kutokana na kuwapo kwa gharama kubwa za uzalishaji, tija ndogo,
riba kubwa za kibenki,tatizo la umeme na urasimu.
Mnyaa alisema licha ya kwamba Shirika la Viwango Tanzania (TBS),
lipo lakini takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na
bidhaa feki kwa ukanda mzima wa kusini na mashariki mwa Bara la Afrika.
“Tukio la hivi karibuni kampuni ya UNI-METAL EAST AFRICA Co
iliingiza bandarini mabati feki 100,000 na TBS ikakamata mabati feki
15,000 tu na 75,000 yaliyobaki yalikuwa tayari yameingia kwenye mzunguko
na Watanzania walikuwa wameshanunua mabati hayo,” alisema.
Awali Dk. Kigoda alisema serikali imeandaa utaratibu ambao
utawezesha kuwapatia wafanyabishara wadogo maarufu wamachinga leseni
maalum ili watambuliwe na kuondokana na adha ya kunyanyaswa katika
maeneo wanayofanyia biashara zao.
Dk. Kigoda alisema moja ya mikakati ya wizara katika kipindi cha
2015/2016 ni pamoja na kufufua viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo
havifanyi kazi kikamilifu kikiwamo kiwanda cha matairi cha General Tyre
cha jijini Arusha na kiwanda cha nguo Urafiki.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment