Rais Jakaya Kikwete
Siku tano baada
ya Rais Jakaya Kikwete kusema kuwa tamko la Jukwaa la Wakristo (TCF)
kuwataka waumini wao kupigia kura ya ‘hapana’ Katiba Inayopendekezwa
lilikuwa la hasira, viongozi hao wamejitokeza tena na kusisitiza kwamba
msimamo wao huo utabaki kama ulivyo.
Katika tamko pamoja walilolitoa jana baada ya
kukutana juzi mjini Dodoma, viongozi hao wamemtahadharisha Rais Kikwete
kuwa kuendelea kupigia debe Katiba Inayopendekezwa na kuruhusu Mahakama
ya Kadhi, kunaweza kulitumbukiza Taifa katika machafuko na hali ikiwa
hivyo Serikali ndiyo itakayolaumiwa.
Tamko hilo limesainiwa na viongozi walewale
waliosaini lile la awali la Machi 12, mwaka huu ambao ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti
wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu
Tarcisius Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania
(CPCT), Askofu Daniel Awet.
Tamko hilo la maneno 921, limeendelea kuwataka
waumini wao kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa
kwa kupiga kura ya ‘hapana,’ msimamo ambao tayari umeibua msuguano baina
yao na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo aliyesema viongozi wa dini hawana mamlaka ya
kuwaamulia waumini wao aina ya kura wanayostahili kupiga.
Pia, Jukwaa hilo limewataka viongozi wakuu wa
Serikali –Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais Kikwete wasifurahi kwamba
ujumbe wao umewafikia viongozi wa dini waliozungumza nao hivi karibuni,
kwa kuwa watu waliokutana nao si wawakilishi rasmi na hawana uwezo wa
kutoa uamuzi au kukubaliana juu ya jambo la kitaifa. “Maaskofu tuliokutana hapa (mjini Dodoma) hatuna
hasira na wala hatuongozwi na hasira wala mihemko katika kufikia maamuzi
tunayofanya kama ambavyo wengine wanavyotutafsiri, tunafikia maamuzi
yetu baada ya maombi na sala na tunasukumwa na upendo kwa wananchi ili
kujenga Taifa lenye umoja, amani, utulivu na maelewano,” lilisema tamko
hilo likihitimishwa kwa maneno ya Biblia kutoka Mithali 29: 1, “Aonywaye
mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafla, wala hapati dawa.”
Jumamosi iliyopita, Rais Kikwete akifungua mkutano
wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam iliyoshirikisha wajumbe
kutoka mikoa mbalimbali ikijumuisha viongozi wa dini za Kiislamu na
Kikristo, alisema msimamo wa TCF kuhusu kuipigia kura ya ‘hapana’ Katiba
Inayopendekezwa ni wa hasira na usiokuwa na tija kwa maendeleo ya
Taifa.
“Nimeyasoma matamko hayo yote kwa umakini,
imenishangaza, imenisikitisha na kunihuzunisha. Siamini kwa nini
wamefikia huko kwa kuunga au kutokuunga mkono,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema: “Waacheni waumini waamue
Katiba wanayoitaka wao... hayo matamko niliyoyasoma yamejaa hasira kwa
Serikali kupeleka bungeni Muswada wa Mahakama ya Kadhi.”
Maaskofu hao walikuwa Dodoma kufuatilia kwa kina
Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali ya mwaka 2014 unaopendekeza,
pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria za
Kiislamu la mwaka 1964 unaotambua Mahakama ya Kadhi.
“Muswada huu unapendekeza kuanzishwa Mahakama ya
Kadhi ambao utawasilishwa bungeni leo kwa hati ya dharura na hivyo
kuufanya umma wa Watanzania kutokujua maudhui yaliyomo katika muswada
huo wakati bado hoja zetu za msingi tulizopeleka kwenye Kamati ya Katiba
na Sheria ya Bunge na kwa Waziri Mkuu hazijajibiwa,” Ilieleza taarifa
hiyo.
“Tunamtaka Rais aagize muswada huu uondolewe
bungeni na usijadiliwe tena kwa kuwa utafiti wa Tume ya kurekebisha
sheria ulishaonyesha madhara ya uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi.
Vinginevyo, kuendelea kujadiliwa kwa muswada huu maana yake ni kwamba
Serikali inajihusisha na itagharimia mahakama hiyo.”
Bunge laondoa Muswada wa Mahakama ya Kadhi
Mikutano ya viongozi
CHANZO: MWANANCHI
Walisema; “Yalijitokeza kwenye semina kwa wabunge mwishoni mwa
wiki ni ishara ndogo ya kile kitakachotokea maeneo yote ya nchi yetu.
Hapa tunajiuliza, endapo maneno ya Rais ni kweli, mbona Bunge
linaendelea kujadili kitu ambacho Serikali haitajihusisha wala
kukigharamia?”
Tamko hilo lilionya: “Tunamtaka Rais (Kikwete)
aiepushe nchi yetu na kuingizwa kwenye mapigano ya kidini ambayo
kuyadhibiti itakuwa vigumu. Pia tunamwomba Rais Kikwete akumbuke na
kutafakari kile kilichotokea na kinachotokea nchi ya Afrika ya Kati,
kati ya kundi la Seleka na kundi la Anti Balaka.
Bunge laondoa Muswada wa Mahakama ya Kadhi
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana bungeni jana na
kuthibitishwa kwa nyakati tofauti na Naibu Spika, Job Ndugai na Katibu
wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah zilisema kuwa muswada huo hautajadiliwa
katika mkutano wa 19 wa Bunge unaomalizika leo, badala yake utapangiwa
siku nyingine.
“Suala la Mahakama ya Kadhi halitawasilishwa
bungeni tena mpaka hapo litakapopangiwa siku nyingine. Hata Waziri Mkuu
(Mizengo) Pinda wakati akizungumza katika semina ya wabunge aliliweka
sawa suala hili. Kwa kauli alizozitoa hakuna haja tena ya kuhoji kama
suala hili litakwenda bungeni au la,” alisema Kashillilah. Ndugai alisema ni vigumu kwa suala hilo kuwasilishwa bungeni na kwamba litajadiliwa katika vikao vijavyo vya Bunge.
Mikutano ya viongozi
Maaskofu katika tamko lao, walisema wameshangazwa
na tabia ya viongozi wa Serikali ya kuitisha na kuendesha mikutano
wanayodai ni ya viongozi wa dini lakini isiyo rasmi.
“Machi 03, 2015 Waziri Mkuu (Pinda) aliitisha
mkutano kupitia mchungaji mmoja ambapo hakuna hata kiongozi mmoja wa
taasisi au kanisa aliyeshiriki. Jambo la kushangaza ni kile kilichotokea
Machi 28, 2015 ambapo Rais Kikwete alishiriki kikao cha kikundi ambacho
siyo rasmi, yaani Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam. “Mikutano ya jinsi hii kati ya Serikali na wale
ambao imewaona kuwa ndiyo viongozi wa dini siyo sahihi kwani viongozi wa
dini wana taratibu zao za kualikwa au kuwakilishwa katika mikutano na
viongozi wa Serikali au wa dini au madhehebu mengine. “Kwa mantiki hiyo tunawashauri viongozi wa
Serikali waache kabisa kutumia vikundi visivyo rasmi kualika mikutano
wanayodhani kuwa itakubalika na waumini wa dini hizo. Mikutano yote ya
jinsi hiyo itakayoitishwa ni batili na maamuzi yake hatuyatambui na
hatutayatambua.”
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment