Rais Jakaya Kikwete.
Jukwaa la Wakristo Tanzania, limesema linashangazwa
na tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali wenye tabia ya kuitisha
mikutano wanayoiita ni ya viongozi wa dini huku ikiwa siyo rasmi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na
Jukwaa hilo, imeeleza kuwa viongozi hao wamekuwa chanzo cha mvutano
uliopo baina ya dini mbili na kwamba watakuwa chanzo cha kuvurugika kwa
amani nchini.
Taarifa hiyo ambayo imesainiwa na Mkuu Habari na Mawasiliano wa
Baraza la Kikiristo Tanzania (CCT), Mchungaji John Kamoyo, ilisema jopo
la Maaskofu kutoka TEC, CPT lilikutana Machi 30, mwaka huu, mjini
Dodoma, kuondoa dhana kuwa linaongozwa na hasira na mihemko katika
kufikia maamuzi linavyoyafanya kama wengine wanavyotafsiri bali
linasukumwa kwa upendo wa wananchi ili kujenga taifa lenye umoja, amani,
utulivu na maelewano.
Kamoyo alisema Machi 03, 2015 Waziri Mkuu aliitisha mkutano kupitia
Mchungaji mmoja ambapo hakuna kiongozi wa taasisi au Kanisa
aliyeshiriki, na kwamba Machi 28, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete,
alikutana na kikundi ambacho sio rasmi yaani Kamati ya Amani ya Mkoa wa
Dar es Salaam.
“Maaskofu tuliokutana Dodoma hatuongozwi na hasaira wala mihemko
katika kufanya uamuzi kama wengine wananavyotafsiri, tunafikia uamuzi
baada ya maombi kwa upendo wa wananchi na kujenga taifa lenye umoja na
amani,” alisema Mchungaji Kamoyo.
Kamoyo alisema walikewenda Dodoma kufuatilia kwa kina Muswada wa
Sheria mbalimabali za mwaka 2014 pamoja na mrekebisho mengine ya Sheria
ya Tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment