Kasisi
mmoja nchini Italia, ameweka kifaa kanisani mwake kinachoweza kubana
mawasiliano ya simu baada ya kuchoka kuwaomba waumini kuzima simu zao
kila wakati alipokuwa anahubiri.
Alilazimika kuomba idhini ya polisi kuweka kifaa hicho baada ya kuchoka kusikia milio ya simu zikipokea ujumbe. Mpango
huo umesifiwa sana na waumini ingawa imewaudhi wenye maduka katika mji
wa Naples wanaosema kifaa hicho kinatatiza masafa na mawasiliano yao na
pia kifaa hicho kimeathiri mashine za kutoa pesa. Wanasema kifaa hicho pia kinatatiza shughuli zao ambapo wateja huagiza bidhaa kupitia simu zao za mkononi.
Lakini kasisi Don Michele
Madonna, anakana kwamba kifaa chake kinatatiza shughuli za wenye maduka
akisema kinaathiri tu mawasiliano kwa simu kwa waumini walio kanisani
peke yake. 'Nilinunua kifaa hicho kutoka kwa duka la vifaa vya
elektroniki, na kuwauliza polisi ikiwa ilikuwa sawa kuweka kifaa hiicho
kanisani mwangu. Ni kifaa kizuri sana kwa sababu kimemaliza tatizo la
watu kupigiwa simu na kuzipokea wakiwa kanisani.
Mmiliki mmoja wa
maduka alisema: 'Tangu kasisi Madonna kuweka kifaa hicho ndani ya kanisa
, nimepata matatizo sana kutumia kadi yangu katika biashara yangu. '' 'Kadi hii haifanyi kazi vyema na ninapoteza sana pesa zangu.''
Kasisi Michele Madonna aliamua
kuchukua msimamo huo kwa sababu waumini walikuwa na mazoea ya kutumia
simu zao kanisani wakati kasisi huyo akihubiri. Kilichomuudhi zaidi
kasisi huyo ni watu kupokea simu kanisani na hata wakati wa mazishi. Kasisi Don alinunua kifaa hicho kwa dola sitini. Kabla
ya kukinunua kifaa hicho alianza kwa kuwasihi waumini kutotumia simu
zao kanisani kwa sababu zilitatiza shughuli zake. Alianza kwa kuweka
mabango kanisani humo lakini ujumbe huo wengi hawakuuzingatia na hapo
ndipo akalazimika kuweka kifaa hicho ambacho kinazuia watu kupokea au
hata kutumia simu zao kanisani.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment