Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini
(TPSF), Dk. Reginald Mengi, akizungumza na ujumbe wa wafanyabiashara wa
Kitanzania uliokwenda China ambao uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi,
Mwantumu Mahiza (wa tatu kushoto) wakati wa chakula cha mchana
kilichoandaliwa na TPSF jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza,
amesema mchango wa sekta binafsi nchini katika kuongeza ajira ni mkubwa
na serikali itakuwa inajidanganya isipolitambua hilo.
Mahiza ambaye jana alitarajia kuhama rasmi kutoka Mkoa wa Pwani aliokuwa
akiuongoza kabla ya kuhamishiwa Mkoa wa Lindi, alitoa kauli hiyo jijini
Dar es Salaam juzi katika mazungumzo ya pamoja na Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF).
Katika mazungumzo hayo, TPSF ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Dk. Reginald Mengi, ilikuwa inampongeza kiongozi huyo kwa mchango wake mkubwa alioufanya kama mtumishi wa umma kwa kuwapeleka wafanyabiashara wa Tanzania nchini China hivi karibuni kwa niaba ya serikali ili kuleta uhusiano wa karibu zaidi wa kibiashara kati yao na wenzao kutoka nchini humo.
Katika pongezi hizo, TPSF walimkabidhi barua mkuu huyo wa mkoa kwa ajili ya kutambua mchango wake alioufanya kuhusu ziara hiyo nchini China. Mahiza alisema serikali isipotambua mchango wa wafanyabiashara nchini kwa maendeleo ya uchumi na kuongeza ajira, itakuwa inajidanganya. Hata hivyo, aliwaomba wanachama wa TPSF kuwashika mkono vijana ili kuinua hali zao za kiuchumi huku wakizingatia vigezo muhimu walivyo navyo vikiwamo elimu, uadilifu na uaminifu na kwamba umaskini unaowakumba Watanzania walio wengi utaondoka iwapo kila mmoja atawajibika katika nafasi yake kwa uaminifu na kwa kumhofu Mungu. Alisema safari ya China ilikuwa ya muhimu mkubwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kujifunza mbinu wanazotumia wenzao kufanikisha shughuli zao za kibiashara.
Aliishauri TPSF kujipanga vizuri kimakundi kwa mfumo huo wa kisekta ikiwa ni moja ya kujifunza mbinu hiyo kutoka kwa wafanyabiashara wa nchini China. Naye Dk. Mengi, alimpongeza Mahiza kwa kutambua umuhimu wa wafanyabiashara nchini na hivyo kuwashirikisha katika ziara yake nchini China ili kujenga uhusiano mzuri kati yao na wa nchini humo. Alisema Mahiza ni wa muhimu kutokana na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na TPSF katika kuinua maendeleo ya uchumi nchini na kwamba wanamuona kuwa ni mwenzao kwani bila kujua lugha ya biashara ingemuwia vigumu kuambatana nao nchini humo ambako walijifunza mambo mengi yakiwamo ya fursa za biashara.
Pia alimpongeza Rais Jakaya Kikwete, kwa kutambua umuhimu wa Mahiza katika uwajibikaji katika majukumu kama mtumishi wa umma na hivyo kumhamishia katika Mkoa wa Lindi ambao una fursa nyingi zikiwamo za uchumi wa gesi asilia na mafuta.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment