Mkuu wa jeshi la Pakistan Raheel Sharif akiwa na rais Ashraf Ghani
Jeshi la Pakistan limeongeza mashambulizi yake dhidi ya wanamgambo wa
Kiislamu na kuuwa wanamgabo 57 kwa mashambulizi ya angani na ardhini.
Jitihada hiyo imechochewa na shambulio la kigaidi la jumanne
lililosababisha vifo vya takribani watu 148 wengi wao wakiwa wanafunzi. Ndege za kijeshi zimeshambulia maficho 20 ya wanamgambo hao ya katika
wilaya ya kikabila ya Khyber iliyopo mji wa Peshawar, ambako wanamgambo
wa Taliban Jumanne iliyopita walifanya mashambulizi yaliyosababisha vifo
vya watu watu 148, wakiwemo wanafunzi 135 katika shule inayiomilikiwa
na jeshi.
Majeshi ya ardhini yanafanya kazi bega kwa bega
Taarifa ya jeshi la nchi hiyo inaeleza kuwa majeshi ya ardhini
pia yamesonga mbele na kuingia katika maeneo ya ndani zaidi katika eneo
la bonde la Tirah, eneo lenye milima karibu na mpaka na Afghanistan
ambako makundi kadhaa ya wanamgambo yenye mafungamano na kundi la
al-Qaeda yamejihimarisha kwa kuweka makazi yao huko. Katika operesheni tofauti askari wa Pakistan wamewauwa wanamgambo watano
wanaoshukiwa kuwa ni Taliban katika mji wa kusini wa bandari ya wa
Karachi. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa msemaji wa kikosi hicho.
Hali ya utulivu yarejea Peshawar
Hali ya kawaida imeanza kurejea taratibu katika mji wa Mjini Peshawar
baada kukaribia karibu kushindwa kuendelea na shughuli zake za kawaida
hapo jana wakati wa maombolezo ya shambulio baya kabisa kuwahi
kushuhudiwa nchini Pakistan kwa zaidi ya muongo mmoja. Katika mji mkuu wa Islamabad, wanasiasa na viongozi wa jeshi wameanzisha
mjadala wa wazi wenye shabaha ya kile walichokiita "mjadala wa mpango
mpya wa kukabiliana na wanamgambo"
Waziri Mkuu Sharif aapa kuangamiza ugaidi
Katika mkutano huo, Waziri Mkuu Nawaz Sharif aliapa kuyasambaratisha
makundi ya wanamgambo wa Kiislamu kwa kutumia nguvu zote za kijeshi na
na kuamua mara moja kumalizika kwa miaka sita kusitisha kunyonga kwa
waliokutwa na hatia ya ugaidi. Maelfu ya raia wa Pakistan waliingia mitaani katika miji yote mikubwa
kulaani shambulizi hilo lililouwa watu wengi na kuishinikiza serikali
kuchukua hatua madhubuti dhidi ya wanamgambo nchini humo.
CHANZO: DW KISWAHILI
No comments:
Post a Comment