2:20 pm Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva asema matokeo
ya majimbo matano yaliyosalia yatatangazwa leo jioni. Mshindi wa
uchaguzi wa urais atakabidhiwa cheti cha ushindi kesho.Usalama umeimarishwa katika ukumbi wa Julius Nyerere ambako tume hiyo imekuwa ikitangazia matokeo ya uchaguzi wa urais.
12:30 pm Tume ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza matokeo ya urais ya majimbo 34.
11.45am:
Mgombea wa CHADEMA Edward Lowassa akatazwa kuingia katika jumba la
matokeo ya uchaguzi ili kutoa pingamizi yake ya matokeo hayo.
11.30am:
Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania pamoja na Ireland Kaskazini umetoa
taarifa ukipinga kufutiliwa mbali kwa matokeo ya Uchaguzi kisiwani
Zanzibar.
Ubalozi huo umesema kuwa hauoni sababu za kufutiliwa
mbali kwa matokeo hayo ilhali waangalizi walifurahishwa na vile uchaguzi
huo ulivyofanyika kwa amani.
Wameitaka tume ya uchaguzi Kiswani Zanzibar kuorodhesha matokeo hayo bila kuchelewa.
10.15am:
Mgombea wa urais wa chama cha CHADEMA anayeungwa mkono na UKAWA Edward
Lowassa wameelekea katika makao ya tume ya uchaguzi NEC kuwasilisha
pingamizi yao kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu Tanzania. Baada ya kutoka
huko wataelekea katika makao makuu ya UKAWA kuvihutubia vyombo vya
habari.
11.00am: Maeneo ambayo matokeo yao yametangazwa na yale ambayo bado hayajatangazwa nchini Tanzania
10.00am:
Kufikia sasa mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha CCM John
Pombe Magufuli anaendelea kuongoza katika kura zilizohesabiwa
9.58pm: Rais mpya wa Tanzania kujulikana leo
Tume
ya uchaguzi nchini Tanzania hii leo inatarajiwa kumtangaza rais mpya wa
taifa hilo hii leo.Hatua hii inajiri siku moja tu baada ya Upinzani
kupinga matokeo ya uchaguzi huo kwa madai kwamba kulikuwa na
udanganyifu mkubwa. Tayari tume ya uchaguzi Kisiwani Zanzibar imefutilia
matokeo ya uchaguzi kisiwani humo.
9.33am: Yalio maagazetini nchini Tanzania.
9.30am:Marekani
imelaani hatua ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC ya kufuta matokeo ya
uchaguzi wa urais pamoja na wajumbe wa bunge la wawakilishi visiwani
humo.
9.15am:Makamishna wa tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar
wameushtumu uamuzi wa mwenyekiti wao Jecha Salum Jecha kwa
kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa kisiwa hicho bila ya kuwashauri
9.00am:Tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar inajiandaa kutangaza tarehe mpya ya marudio ya uchaguzi huo.
6.15am:Kisiwani Zanzibar hali ni shwari. Ni asubuhi njema.
Matokeo
ya uchaguzi wa urais nchini Tanzania yanaendelea kutolewa huku BBC
ikiendelea kukufahamisha kuhusu matukio tofauti nchini humo. Tume ya
Taifa ya Uchaguzi imetangaza
matokeo ya majimbo takriban 187 na matokeo zaidi yanatarajiwa leo.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment