Lazaro Nyalandu alizaliwa Agosti 18, 1970 mkoani
Singida, hivyo atafikisha miaka 45 Agosti mwaka huu. Kwa sasa yeye ni
Waziri wa Maliasili na Utalii.
Lazaro Nyalandu alizaliwa
Agosti 18, 1970 mkoani Singida, hivyo atafikisha miaka 45 Agosti mwaka
huu. Kwa sasa yeye ni Waziri wa Maliasili na Utalii.
Nyalandu alipata elimu ya msingi katika shule za Pohama na Mrumba zilizoko kijijini kwao huko mkoani Singida na kuhitimu mwaka 1987. Aliendelea na masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Kibaha mkoani Pwani (1988 – 1991) na alifaulu vizuri na kujiunga na Shule ya Sekondari Ilboru ambako alisoma kidato cha tano na sita.
Wakati akiwa mwanafunzi wa sekondari, Nyalandu alikuwa kiongozi wa juu wa Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (Ukwata) 1991 – 1993 na baadaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania walioteuliwa kuzuru jiji la Rio De Janeiro, Brazil na kushuhudia mkutano wa Mazingira mwaka 1993.
Nyalandu alipata elimu yake ya Chuo Kikuu nchini Marekani ambako alihitimu Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Usimamizi wa Biashara (BBA) mwaka 1997 katika Chuo Kikuu cha Wartburg. Kabla ya hapo alikuwa amepata Shahada ya Biashara ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Wardorf nchini humo. Kiongozi huyu, sasa ana Shahada ya Uzamili aliyoipata kwa njia ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Buckingham, Uingereza akifuzu katika masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diplomasia.
Baada ya kuhitimu masomo yake ughaibuni, Nyalandu alianza kazi huko huko Marekani katika Benki ya North West, akifanya kazi katika kitengo cha operesheni za kibenki kati ya mwaka 1998–1999.
Aliporejea nchini Tanzania alifanikiwa kuwa sehemu ya washauri wa mke wa aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa, katika uendeshaji wa taasisi ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF). Ushauri wa timu yake ulisaidia taasisi hiyo kupata misaada mingi kutoka nchi za Ulaya, Marekani, China na nyinginezo. Pia, alikuwa anamsaidia mama huyo katika uandishi wa hotuba zake pale alipokuwa na majukumu makubwa ya kitaifa na kimataifa.
Nyalandu amemwoa mrembo wa Tanzania mwaka 2004 ‘Miss Tanzania’, Faraja Kotta na wana watoto wawili, Sarah na Christopher.
Mbio za ubunge
Tangu alipokuwa kijana mdogo, Nyalandu alionyesha kila dalili kuwa na nyota ya uongozi. Watu wanaomfahamu hawakushangaa walipomwona mwaka 2000 anaingia kwenye mpambano ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akilisaka jimbo la Singida Kaskazini. Kutokana na udhaifu wa upinzani uliokuwepo wakati huo alijua atakuwa na kazi kubwa ndani ya chama chake tu, hivyo, alipopitishwa na CCM akapambana majukwaani na wapinzani na kuwa mbunge.
Mwaka 2005, Nyalandu alipitishwa tena na chama chake kuwania ubunge Singida Kaskazini, akakutana tena na upinzani dhaifu kutoka kwa Kimia Omari Rashid wa Chadema, akajivunia asilimia 93.5 ya kura zote na kuwa mbunge hadi mwaka 2010.
Baada ya kupata uzoefu wa ubunge, kwa miaka kumi, Nyalandu alirudi tena kutetea mara ya tatu; CCM ikampa nafasi mwaka 2010 na wananchi wakamchagua kwa ushindi wa asilimia 87.7 akimshinda kwa mara nyingine mgombea yuleyule wa Chadema wa mwaka 2005.
Ushindi wa mara hii ulikuja na bahati kubwa kwa Nyalandu. Bahati ya kwanza ilikuwa kukwea ngazi zaidi. Rais Jakaya Kikwete alimteua Nyalandu kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Novemba 2010 na alidumu hapo hadi Mei 2011 alipohamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, nafasi aliyokaa kwa takriban miaka mitatu.
Bahati ya pili, Januari 2014, nyota yake ilipaa zaidi akapewa wadhifa mkubwa; mara hii akiteuliwa kuwa waziri kamili wa Maliasili na Utalii, sekta ambayo ina changamoto kubwa sana hapa nchini na hadi namjadili Nyalandu leo hii yeye ndiye waziri wa sekta hiyo nyeti ambayo imenufaisha mamia ya nchi duniani huku Tanzania watu wengi wakisema utalii haujalisaidia taifa kwa kiasi kinachofaa.
Mbio za urais
Nyalandu aliweka wazi nia yake ya kuwania urais Desemba 28, 2014 na alitangaza nia hiyo ya kugombea urais katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Ilongero, katika jimbo analoliongoza, Singida Kaskazini, wakati akihutubia mamia ya wananchi.
Katika mkutano huo alisisitiza kuwa “sasa ni zamu ya vijana kuongoza nchi” huku akiwaambia wananchi kuwa safari yake ya ubunge kwa miaka 15 inaanzisha safari nyingine bila kuwaeleza ikiwa bado ana nia na ubunge au la. Aliambatana na mkewe, watoto wake pamoja na wazazi wake.
Kabla ya kutangaza nia ya urais, Nyalandu aliwahi kusikika akisema kuwa “siwezi kutangaza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao bila kutumwa na watu” lakini kabla watu wenyewe hawajamtuma aliibuka na kuwaita yeye mwenyewe mkutanoni na kuweka nia yake.
Nguvu yake
Nyalandu ni msomi mwenye jitihada kubwa. Si mwanasiasa mzembe au aliyekimbia umande; aliusaka kokote kule na leo hii anaweza kuingia kwenye mizani ya kupimwa kama mtu anayeweza kuongoza nchi au la. Mimi naamini kuwa CCM inahitaji rais ambaye moja ya sifa zake pia ni usomi na kwa sifa hii ya kuwa na shahada tatu za chuo kikuu inambeba Nyalandu.
Jambo jingine ni nguvu ya nyumbani. Nyalandu ni kiongozi mtulivu na anapendwa na watu wake pale Singida Kaskazini. Hii ni nguzo muhimu kisiasa – kuungwa mkono na watu wa nyumbani kwako – na kuna wanasiasa huhamia hata kwa waganga kusaka waungwe mkono na wananchi wa majimbo ya nyumbani kwao; katika hili Nyalandu “atajiganga” na linamwongezea nguvu ndani ya CCM.
Jambo la tatu katika nguvu za Nyalandu ni kwa sababu kuna watu wanaomkubali ndani ya CCM. Tukumbuke kuwa amekuwa mtu wa karibu na mama Anna Mkapa kwa kipindi kirefu na mwanya huo aliutumia pia kuwa na mawasiliano na Rais Mkapa na hata alipokuwa mbunge akazidi kujijenga. Baadhi ya makada muhimu ndani ya CCM wanamtaja vizuri na hii ni nafuu kubwa kwa mwanasiasa anayesaka kuingia Ikulu.

Pia, ana uzoefu wa kukaa bungeni kwa miaka 15. Huu ni uzoefu
wa kipekee kabisa. Alipoingia bungeni, kwa mara ya kwanza, alikuwa
kijana wa miaka 30 leo ana miaka 45. Utumishi wa chombo kikubwa kama
Bunge kwa miaka 15 ni turufu muhimu sana kwake na inamwongezea sifa
muhimu za kumbeba katika kinyang’anyiro.
Udhaifu wake
Pamoja na kutangaza nia ya kuwania urais, Nyalandu bado hajatangazika sana na nadhani timu yake ya mikakati ni dhaifu. Hakika ukizunguka huku na kule husikii akiongelewa kama mgombea urais. Tangu atangaze nia yake hajawa gumzo miongoni mwa Watanzania na hiyo inaweza kumaanisha kwamba atakuwa anajimaliza mwenyewe. Ukimlinganisha na wagombea wenzake wa CCM pamoja na uzoefu wake, ameshindwa kujitangaza vizuri.
Jambo jingine ni mtandao dhaifu. Nyalandu ni kati ya wana CCM wanaohitaji kuwania urais, lakini ana mtandao hafifu na dhaifu ndani ya chama chake. Sote tunajua umuhimu wa kuwa na mtandao mkubwa ili kupata nafasi ya uteuzi ndani ya CCM na ikiwa unakosa mtandao mpana, kama Mkapa mwaka 1995, unapaswa kuwa na wapigadebe wenye sauti kali na za kutisha katika vikao vya maamuzi vya CCM kama alivyokuwa Mwalimu Nyerere, lakini yote mawili anayakosa.
Jambo la tatu ambalo linaweza kuwa udhaifu wake ni kushindwa kusimamia masuala ya msingi katika jimbo lake pamoja na kwamba amekuwa mbunge kwa miaka 15. Ukitaka kuamini haya nenda Singida Kaskazini; ni kati ya maeneo ambayo wananchi wanaishi maisha duni na ya umasikini huku huduma muhimu za kijamii zikiendelea kuwa changamoto kubwa.
Pamoja na watu wa jimboni kwake kumpenda, lakini mara kwa mara amekuwa akikabiliwa na wagombea dhaifu kutoka upinzani, ukweli unabaki kuwa jimbo lake linaweza kuwa sehemu ya mfano wa udhaifu wake kiuongozi.
Nyalandu ni mtu anayependa maisha ya juu na kusafiri, ndiyo maana katika utumishi wake, akiwa Waziri wa Utalii na Maliasili amekuwa na safari zisizoisha nje ya nchi wakati utatuzi wa masuala ya maliasili unapatikana kirahisi kwa kuimarisha ulinzi wa wanyama ndani ya nchi badala ya kujifunza mikakati mipya Ulaya na kwingineko. Yeye amekuwa akisisitiza kuwa amekuwa akisafiri kwa shughuli maalumu za serikali kwa lengo la kutangaza utalii pamoja na shughuli zenye maslahi kwa Taifa.
Nini kinaweza kumfanya apitishwe?
Dhana ya ujana, kama ambavyo ameiongea yeye mwenyewe wakati anatangaza nia, itambeba. Ikiwa CCM inahitaji rais kijana na wa kizazi cha sasa, Nyalandu anaweza kuwa miongoni mwa chaguo kwa kazi hiyo. Lakini lazima aendelee kukithibitishia chama hicho kuwa yeye ni wa kizazi cha sasa, kwa maneno na matendo siyo kizazi cha sasa mdomoni huku matendo yanakuwa yaleyale yaliyowachosha wananchi.
Sababu nyingine ambayo ni muhimu kwake ni uzoefu wa kukaa bungeni miaka 15 ikiwamo miaka mitano katika nafasi mbalimbali za uwaziri huku akiruka vihunzi vyote vya mabadiliko kadhaa ya Baraza la Mawaziri la Rais Kikwete. CCM inaweza kuhitaji mteule wa kisasa, lakini lazima awe na uzoefu. Kukaa kwake bungeni muda mrefu zaidi inaweza kuwa karata ya kujivunia kwake.
Usomi wake pia ni karata nyingine katika dhana hii ya kupitishwa. Ana shahada tatu za Chuo Kikuu na amekuwa na rekodi nzuri ya kitaaluma tangu shule ya msingi, hivyo kichwani mwake kuna kitu cha kutumainiwa. Tunajua kuwa vyama vyote havihitaji marais “mbumbumbu” na kategoria hii inambeba.
Nini kinaweza kumwangusha?
Kutoelewana na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM ni moja ya mambo yanayoweza kumwangusha Nyalandu kwenye mchujo. Vyombo vya maamuzi bado vinakumbuka ile dhana ya “mawaziri mizigo” ambayo ilishupaliwa, nchi nzima, na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye tangu mwaka 2013. Kinana na Nape ni viongozi wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM kwani kwenye orodha ya mawaziri ambao walipaswa kubadilishwa na Rais Kikwete, Nyalandu pia alitajwa kwenye orodha ya “mizigo hiyo”. Lakini Kikwete alipofanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri, Nyalandu alibakizwa.
Vita ya viongozi wa juu wa CCM dhidi yake iliendelea tena mwaka huu ambapo Kinana na Nape walipokuwa mikoa ya Singida, Dodoma na Arusha, kila walipokutana na vilio vya wananchi kulalamikia utendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Kinana aliwajibu kwa kumnanga Nyalandu kuwa “anazurura, anafanya matembezi na kupiga maneno bila kushughulikia matatizo ya wananchi”.
Nyalandu alipoona kama wenzake wanamharibia safari yake ya urais, aliwajibu kwa kusema, kwa kiwango kikubwa vita anayokabiliana nayo na madongo anayopigwa na baadhi ya viongozi wake ni kutokana na uamuzi wake wa kudhibiti uwindaji wa tembo kwa zaidi ya asilimia 50, hali ambayo sasa inaonekana kuwakera baadhi ya watu wenye maslahi na biashara hiyo. Mvutano huu wa Nyalandu na viongozi wenzake ni hatari katika mbio zake za urais.
Suala la pili linaloweza kumwangusha ni kashfa zilizopo kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii. Kama nilivyoeleza awali, kitendo tu cha kukabidhiwa uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika nchi kama Tanzania, tayari kinaweza kuwa kikwazo cha mbio zako za urais kutokana na asili ya wizara hii isiyoishiwa kashfa na tuhuma.
Tangu Nyalandu aongoze wizara hii kumekuwa na mengi yanazungumzwa juu yake. Hili pamoja na mengine mengi tusiyoyafahamu yataibuka wakati wa mchujo na yanaweza kumweka mahali pabaya na hata kumwondoa kwenye mchuano katika hatua za awali, hususan ikiwa vyombo vya usalama na uchunguzi vya serikali vitakuwa na taarifa za uhakika za uhusika wake na sakata za aina hiyo.
Asipopitishwa (Mpango B)
Pamoja na Nyalandu kuanza harakati za kuusaka urais hajawaaga wana wa Singida Kaskazini kuwa hatogombea tena ubunge. Hali hiyo inaweza ikatafsiriwa kuwa hana uhakika na urais, hivyo, anajitosa kote kote ili asikose bahati pande zote mbili. Tabia ya namna hii inaweza pia kutafsirwa kama tamaa au kukosa “focus” ya kisiasa.
Mwanasiasa mahiri na makini, mara zote, hufanya jambo moja kwa wakati fulani katika siasa na anapoamua kupanda ngazi huwaachia wengine wajifunze kule alikotoka. Hapa Nyalandu hajapatendea haki.
Namtazama Nyalandu kama mtu mwenye mipango ya kuendelea na ubunge ikiwa hatateuliwa, na kwa hali ya kisiasa ya ndani ya jimbo lake, ikiwa atapita kwenye kura za maoni za ndani ya CCM, kwenye ngazi hiyo, anaweza kuchaguliwa kirahisi ukizingatia kuwa mtandao wa upinzani unakua polepole Singida Kaskazini.
Hitimisho
Nyalandu si mshindani wa kutisha miongoni mwa wanaosaka urais kupitia CCM mwaka huu na hawafikii wanasiasa wengi tu ndani ya chama hicho ambao watachukua fomu kuomba ridhaa ya chama chao.
Wakati huohuo siasa ni matangazo; ukienda huko Kagera, kwa mfano au Mtwara, ukiuliza jina “Lazaro Nyalandu” unaweza kukuta wananchi wengi hawamjui na labda pia hawamsikii, amejificha mno kwenye harakati zake hizi, na naweza kusema katika kujitangaza amezidiwa kimikakati na vijana wenzake wenye uzoefu mdogo tu ambao pia wametangaza nia. Pamoja na yote hayo, tunamtakia kila la heri katika safari yake.

CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment