Pages

Wednesday, March 25, 2015

SERIKALI YAMPONGEZA DK. MENGI KWA KUINUA SACCOS

Serikali imepongeza jitihada za Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, katika kuwezesha Vikundi vya Kuweka Fedha na Kukopa (SACCOS) hasa vya wanawake na vijana kwa lengo la kufanikisha mpango wa maisha bora kwa kila Mtanzania.

Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, alisema serikali inatambua na kuthamini jitihada hizo na alihamasisha wafanyabiashara wengine kufuata nyayo za Dk. Mengi. Waziri Malima, alikuwa akijibu swali la nyongeza la Diana Chilolo (Viti Maalumu-CCM), aliyeitaka serikali  kupongeza jitihada za baadhi ya wafanyabiashara wanaosaidia wananchi, akitoa mfano wa Dk. Mengi, aliyemuelezea kwamba amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia SACCOS hasa za wakina mama na vijana.
”Serikali ipo tayari kumpongeza mfanyabiashara huyu ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania, pamoja na kuhamasisha wafanyabiashara wengine, kubeba jukumu la kuwezesha SACCOS za akinamama na vijana kwa lengo la kuwezesha kufikia mpango wa serikali wa maisha bora kwa kila Mtanzania?” alihoji Chilolo.
Akijibu swali la msingi lililoulizwa na Hussein Nassor Amar (Nyang’wale) ambaye alitaka kufahamu sababu za serikali kukopesha fedha SACCOS za mijini tu huku za vijijini zikikosa fursa hiyo, alisema katika bajeti ya serikalini,  hakuna fungu la fedha kwa ajili ya kukopesha vyama hivyo.
“Hata hivyo wapo wadau wengi wanaoingia katika makubaliano maalumu na SACCOS,  kisha kuziwezesha serikali ilishajiondoa katika kufanya biashara na hivyo haijatengeneza mpango wa kukopesha taasisi yoyote ikiwamo SACCOS,” alieleza Malima
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment