
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
kimeibuka na ushindi dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi
wa marudio wa Serikali za Mitaa katika mtaa wa King'azi B, Kata ya
Kwembe, jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi huo uliofanyika juzi katika mazingira ya amani na utulivu,
ulishirikisha wagombea wa nafasi ya mwenyekiti, wajumbe wa serikali ya
mtaa na wa viti maalum kutoka vyama vya Chadema na CCM. Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa uchaguzi huo, George Lupia,
alisema kuwa Chadema kimeshinda nafasi zote hizo dhidi ya wapinzani
wake CCM na hivyo kuwa viongozi wa mtaa huo.
Msimamizi huyo alisema kuwa mgombea wa Chadema, Donath Mtemekele,
alishinda kwa kupata kura 585 huku wa CCM, Daud Ngaliba, akipata kura
376 na kwamba kura 18 ziliharibika. Lupia alisema wananchi ambao walikuwa wamejiandikisha katika
daftari wa wapigakura walikuwa ni 1352, lakini waliojitokeza kupiga kura
ni 979.
Mtaa wa huo ulirudia uchaguzi baada ya uchaguzi wa Desemba 14,
mwaka jana kuvurugika na kuahirishwa mara mbili kutokana na sababu
mbalimbali. Uchaguzi huo ulivurugika kutokana na vurugu ambazo zinadaiwa
kufanywa na wafuasi wa vyama hivyo ambavyo vilikuwa vinachuana kuongoza
mtaa huo.
Katika uchaguzi huo wa mwaka jana, ilidaiwa kuwa mgombea wa nafasi
wa mwenyekiti kupitia Chadema alikuwa ameshinda kwa kura 312 huku wa CCM
akipata kura 207. Kufuatia ushindi huo, Chadema kimesema kitawatumikia ipasavyo wananchi wa eneo hilo ili kuwaletea maendeleo.
KAULI YA DK. SLAA
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema chama chao
kimeupokea wa furaha ushindi huo akissema ukombozi umeanza kuonekana
kutokana na wananchi kufanya uamuzi shahihi. “Tumeupokea ushindi kwa furaha kwa mataokeo haya ni jinsi gani
ukombozi umeanza kuonekana, wananchi wamemchagua kiongozi sahihi
wananyemtaka kwa ridhaa yao,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa alisema kuwa kilicho mbele yao ni kuwatumikia wananchi kwa moyo mmoja na kuwaondelea kero zinazowakabili.
KATIBU KATA AZUNGUMZA
Naye Katibu wa Chadema wa Kata ya Kwembe, Raphael Gwelino, alisema
siri ya kupata ushindi katika mtaa huo ni maanadalizi mazuri
waliyoyafanya na kupambana na hujuma zote walizotaka kufanyiwa. “Tunashukuru tumeshinda kwa kishindo, tulijiandaa vizuri pamoja na
hujuma zote tulizotaka kufanyiwa, wananchi wamefurahi sana wametengeneza
jeneza lina bendera ya Chama cha Mapinduzi, wanalipitisha mtaani,”
alisema Gwelino.
Aidha, alisema watakuwa makini kusimamia miradi iliyopo katika mtaa huo ukiwamo mradi wa maji unaofadhiliwa na Saint Marry.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment