Thamani
 ya sarafu ya Urusi imedorora kwa kiwango kikubwa zaidi licha ya 
jitihada za benki kuu ya nchi hiyo kuongeza kiwango cha chini cha riba 
ilikujaribu kuzuia kudorora zaidi  kwa uchumi wa taifa hilo kubwa tajiri
 wa mafuta na gesi ya kupikia.
Benki kuu ya Urusi ilikuwa 
imetangaza kuongezeka kwa kiwango cha chini cha riba kutokea asilimia 
10% hadi asilimia 17% ikiazimia kuzuia kushuka kwa thamani ya sarafu 
hiyo dhidi ya dola ya kimarekani.
Aidha Benki  kuu ya taifa hilo 
ilitaka kupunguza makali kwa raiya kufuatia mfumuko wa bei ya vyakula na
 vitu vingine vya kimsingi. Benki kuu ya Urusi imeongeza kiwango chake cha ushuru na kufikia asilimia 17 kutoka asilimia 10 nukta 5 ya awali.
Taifa hilo linasema kuwa maamuzi hayo yameafikiwa baada ya kushuka kwa viwango vya mtaji na ugumu wa maisha. Hilo limefanyika saa kadhaa baada ya sarafu ya Urusi, kushuka kwa kiwango kikubwa, tangu mwaka 1998, kwa zaidi ya asilimia kumi.
Simon Derrick, ambaye ni mtaalamu mkuu wa maswala ya kifedha katika benki ya New York Mellon, hajatamaushwa na maamuzi hayo. Kudorora
 huko kwa uchumi kumechangiwa pia na vikwazo Kutoka kwa mataifa ya 
magharibi, kutokana na mzozo unaoendelea Nchini Ukraine.
CHANZO: BBC SWAHILI 
No comments:
Post a Comment