Mahasimu wao katika kundi C Ghana na Afrika kusini hazijaamua nani
atakuwamo katika vikosi vyao. Maandalizi ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika yanaendelea, wakati
timu inayopigiwa upatu kutoroka na kombe hilo Algeria imetaja kikosi
chake cha mwisho kwa ajili ya fainali hizo mwakani nchini Guinea ya
Ikweta
Kocha mpya wa Ghana Avram Grant, ambaye
aliiongoza Chelsea katika fainali ya kombe la Champions League mwaka
2008 na kushindwa kwa penalti dhidi ya Manchester United , amechagua
kikosi cha kwanza cha wachezaji 31.
Kocha wa Afrika kusini , Ephraim "Shakes" Mashaba , amewaita wachezaji
34 kwa ajili ya kambi ya mazowezi baada ya krismasi mjini Johannesburg.
Cape Verde , Gabon na Mali tayari zimekwisha chagua vikosi vyao vya
mwisho kwa mashindano hayo ya kila baada ya miaka miwili yanayojumuisha
timu 16 zinazopambana katika fainali hizo katika viwanja vya mjini Bata,
Ebebiyin, Malabo na Mongomo nchini Guniea ya Ikweta.
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, mwenyeji Guinea ya Ikweta, Guinea na
Cote D'Ivoire bado hazijataja vikosi vyao kabla ya muda wa mwisho wa
Januari 7 wa kutangaza vikosi vyote vitakavyoshiriki katika fainali.
Kocha wa Algeria mzaliwa wa Ufaransa Christian Gourcuff amewajumisha
wachezaji 18 kati ya kikosi cha wachezaji 23 waliokwenda Brazil mwaka
2014 katika kombe la dunia na kuifikisha timu hiyo ya kaskazini mwa
Afrika katika duru ya mtoano kwa mara ya kwanza.
Grant amewaondoa kundini Kevin-Prince Boateng na Sulley Muntari, ambao
waliondolewa katika kikosi cha kombe la dunia nchini Brazil, baada ya
kudokeza kuwa angependa kuwaita tena wachezaji hao.
Mchezaji wa siku nyingi wa kati Michael Essien , ambaye alicheza chini
ya Grant akiwa Chelsea , ni mchezaji nyota mwingine ambaye ameshindwa
kuingia katika kikosi hicho.
CHANZO: DW KISWAHILI

No comments:
Post a Comment