Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira akiwahutubia
wananchi kwenye Ukumbi wa Benki Kuu Tanzania (BoT) mjini Mwanza
alipotangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM.
Waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika, Stephen Wasira ametangaza nia ya kuwania urais
akisema iwapo CCM itampa ridhaa ya kupeperusha bendera yake,
atahakikisha utendaji wa Serikali yake unakuwa wa kitaasisi.
Alitangaza nia hiyo katika Ukumbi wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) Mwanza jana Wasira alisema: “Baada ya kutafakari kwa
makini nimeona uamuzi wa kugombea nafasi hii ya juu kabisa kwa nchi yetu
ni sahihi na wakati muafaka, kwa kuwa nina nia ya kupeleka nchi hii
katika ngazi ya juu kabisa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.”
Katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya ITV na Star TV, Wasira alisema: “Leo nakuja hapa Mwanza kuvunja ukimya na kumaliza minong’ono kwa kutangaza rasmi kwamba nimekata shauri ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya ITV na Star TV, Wasira alisema: “Leo nakuja hapa Mwanza kuvunja ukimya na kumaliza minong’ono kwa kutangaza rasmi kwamba nimekata shauri ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Wasira aliyekuwa ameongozana na mkewe na baadhi ya
viongozi wa CCM, alisema angependa kuwaeleza Watanzania ni kwa nini
amechukua uamuzi huo kwa kuwa jambo hilo si dogo.
“Kwanza ni haki yangu. Raia wote wana haki ya
kugombea, ni haki ya kikatiba. Lakini ninayo sababu nyingine ambayo ni
kubwa zaidi, naifahamu vizuri Tanzania kwa muda mrefu tangu miaka ya
1970 nimeshirikishwa katika uongozi wa Taifa hili nikiwa na miaka 25,”
alisema Wasira akibebwa na historia ya utendaji ya muda mrefu.
Wasira alitamba kuwa iwapo atateuliwa na CCM na
kushinda urais, Serikali yake itasimamia uadilifu na kupambana na rushwa
na amedhamiria kupandisha viwango vya maendeleo. Aliwaonya Watanzania
kutothubutu kuukabidhi urais kwa mla rushwa, kwani kuna siku atauza
Ikulu.
“Ili kukabiliana na changamoto hizi kubwa, itakuwa
lazima kwa chama chetu kumteua mgombea ambaye hana historia ya
kuhusishwa na ufisadi, iwe kwa kutuhumiwa tu au kuhusika kweli. Mgombea
anayejua historia ya nchi yetu, pale ilipo na kule inakopaswa kuelekea.”
Akimnukuu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere
mara kwa mara, Wasira alisema kiongozi huyo aliwahi kusema kuwa rais wa
Tanzania ni lazima achukie rushwa na anatakiwa aonekane kwa vitendo
akiichukia... “Siku hizi kila kiongozi anakemea rushwa kama fasheni hata
wala rushwa wanaikemea kwa sababu bila kufanya hivyo wanaona mambo yao
hayatawanyookea.”
Kauli hiyo ya Wasira iliwafanya wafuasi wa chama hicho kusimama na kumshangilia huku wakiimba ‘Wasira sema usiogope.’
Alisema: “Mwalimu Nyerere aliwahi kuniuliza
ninataka nini kati ya utajiri na kuongoza watu, alisema nikitaka utajiri
nichague kuwa mfanyabiashara kwani nitanunua kwa bei rahisi na kuuza
aghali.”
Alisema Nyerere alimweleza kuwa hawezi kuwa tajiri
kwa kazi ya kutumikia watu kwa mshahara na kwamba mfanyabiashara ndiye
anaweza kutajirika. “Kwa hiyo nimewatumikia Watanzania katika nafasi
mbalimbali tangu nikiwa na umri wa miaka 25 lakini sijawahi kuhusishwa
na kashfa za rushwa, nyie ni mashahidi sijawahi kuhusishwa na kashfa za
Epa wala Tegeta Escrow,” alisema.
Alisema hahusishwi na masuala ya rushwa kwa sababu alichagua
kuwa mtumishi wa watu na kwamba hawezi kutajirika kwa kazi hiyo na ndiyo
maana hana tamaa.
Alisema ukiona mtumishi wa watu anatajirika, basi ufahamu kwamba ni mla rushwa kwa sababu mshahara hauwezi kumtajirisha.
Wasira aliyewahi kuzuiwa kuwania ubunge na
Mahakama ya Rufani kwa tuhuma za kutoa rushwa, alisema akiwa rais
ataliweka tatizo la rushwa kuwa katika mjadala wa kitaifa ili kupata
mbinu mbadala za kumaliza tatizo hilo. “Mnaweza mkanipima hapa kuhusu rushwa siyo kwamba
siongozi wizara zenye mamlaka, hapana! Ningeweza kuuza mbolea yenu.
Hatutaki mtu kuzungumzia rushwa kama fasheni, tunataka tukuone usoni na
moyoni kuwa unachukia rushwa,” alisema.
Mamlaka za mikoa, wilaya
Alisema Serikali yake itahakikisha tawala za mikoa na wilaya zinapewa kipaumbele katika ukuaji wa mabadiliko kwenye maeneo yao. “Kipaumbele kitawekwa kwenye ushiriki wa jamii
katika maendeleo, kitawekwa kuhamasisha ushiriki, umiliki na usimamizi
wa maendeleo ya mahali kwa kuzingatia mageuzi yao. Nitatekeleza dhana ya
‘korido za maendeleo’ ili wakulima wanufaike na unafuu wa gharama kwa
sababu ya kufanana kwa kanda za mazao ya kilimo ambazo mara nyingi
huvuka mipaka ya kiutawala ya mikoa.”
Alisema uchumi wa mahali utafanya mageuzi yake
kuingizwa kwenye ajenda ya maendeleo wakati uanzishwaji viwanda kupitia
usindikaji na kuongeza thamani, utahamasishwa na vichocheo
vitakavyotumia fursa ya ukuaji na mageuzi kwa wote.
Miundombinu
Waziri huyo alisema Tanzania inahitaji miundombinu
mingi kuanzia vinu vya kufulia umeme hadi mifumo ya usambazaji
majisafi, viwanja vya ndege, bandari, mitandao ya barabara, reli na
mawasiliano ya simu. “Utawala wangu utaweka kipaumbele cha hali ya juu
ili kuhakikisha uwapo wa miundombinu ya uhakika na gharama nafuu kwa
ajili ya wazalishaji na walaji kuendana na ukuaji wa juu unaomfaidisha
kila mmoja,” alisema.
Wasira, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kuandaa
Ilani ya CCM 2015-2020, alisema serikali yake itaweka kipaumbele katika
maeneo matatu makuu ili kupata matokeo kwa miaka mitano, aliyataja kuwa
ni kuongeza uzalishaji umeme hadi megawati 7,000 ifikapo mwaka 2025.
Afya
Elimu
Uchumi
Eneo jingine alisema ni kujenga njia za reli kuunganisha bandari
kandokando ya bahari, kwenye maziwa na vituo vya mkakati vya kuvutia
mipaka ya nchi na maeneo yote muhimu ya uzalishaji. Pia, ili kuhakikisha
mawasiliano yenye kasi ya hali ya juu ya intaneti yanafika katika
majiji, miji na vijiji vyote.
Afya
Wasira alisema Serikali yake itahakikisha huduma za bima ya afya zinapatikana kwa wote. “Uwekezaji wetu wote katika elimu, utengenezaji wa
nafasi mpya za ajira, miundombinu na utawala bora vitakuwa na mafanikio
kidogo kama hatutazingatia afya za raia wetu. Utawala wangu utaweka
dhamira ya kujenga huduma bora za afya itakayowahudumia watu wote. Bima
ya afya, hasa ya jamii, itapewa kipaumbele kuimarisha upatikanaji wa
huduma bora za afya.”
Alisema licha ya kuwapo mafanikio na kuongeza
idadi ya wataalamu wa afya na hospitali nchini kwa miaka 50 iliyopita,
huduma zake hazilingani na mahitaji kwani watu wengi hawawezi kupata
tiba kwa sababu ya umaskini. “Wale wanaomudu gharama za matibabu wanakimbilia
nje kuyapata. Utaratibu huu unaligharimu Taifa fedha za kigeni hivi
sasa deni linazidi kulimbikizwa kwenye hospitali hizo kama India, watu
wetu wengi wanaishi na magonjwa yanayotibika lakini taratibu
yanawadhoofisha kisha kuwaua,” alisema Wasira.
Elimu
Iwapo atapitishwa na CCM na hatimaye kuchaguliwa
kuwa rais, Wasira alisema utawala wake utaweka dhamira ya kuunda upya
elimu ya Tanzania ili kuandaa rasilimali watu yenye weledi wa kutosha
yenye kufaa kwa sekta ya umma na binafsi. “Tutaweka mkazo wa kuleta ubora wa elimu ngazi
zote kwa kuandaa mitaala (mitalaa) kamilifu kwa ajili ya elimu bora,
hasa kwa kuwekeza katika walimu wa kutosha na walioiva vyema na
mazingira ya kazi ili yaendane na idadi kubwa ya uandikishaji,” alisema.
Uchumi
Wasira alisema dira ya serikali ya awamu ya tano
ni kujenga uchumi imara wenye kuleta ushindani na mkazo mkubwa kwenye
serikali yake itakuwa kuleta maendeleo yanayomjumuisha kila mmoja.
Alisema anataka kuhakikisha kila Mtanzania anapata
nafasi ya ajira yenye hadhi ili aweze kushiriki kwa namna yenye tija
katika michakato ya ukuzaji wa uchumi. “Serikali yangu itajenga katika misingi iliyowekwa na awamu
zilizotangulia hasa rekodi nzuri ya uchumi mpana wa nchi, uwekezaji
katika miundombinu na kufikia viwango vizuri vya ukuaji uchumi kwa
wastani wa asilimia saba kwa mwaka.
Ajira
Uzalishaji viwandani
Uvuvi
“Nitaweka dhamira ya kuongeza viwango vya ukuaji
hadi kufikia asilimia 12 kwa mwaka na kurekebisha uchumi ili kuwapa
fursa Watanzania wote kushiriki katika maendeleo ya nchi yao.”
Alisema Serikali yake itafanya kazi katika maeneo
manne, ikiwamo mabadiliko katika kilimo na shughuli za vijijini,
kuanzisha viwanda kwa msukumo wa kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na
rasilimali.
Wasira alitaja kazi nyingine ambayo Serikali yake
itafanya kama CCM itampitisha kuwa ni pamoja na kutengeneza fursa za
ajira zenye hadhi kupitia biashara ndogondogo na za kati, kufanya uchumi
wa huduma uwe wa kisasa ukiwamo utalii na sekta nyingine za huduma kama
viwanda.
“Watu wengi wanategemea kilimo ili kuendesha
maisha yao, kipaumbele cha juu kitakuwa katika mapinduzi ya kilimo na
uchumi wa vijijini ili kufanya uwe na uzalishaji wa juu ambao utaleta
mabadiliko katika maisha ya Watanzania,” alisema Wasira.
Ajira
Akizungumzia ajira kwa vijana, Wasira alisema
anadhamiria mbali na kutazama ajira rasmi zenye mshahara, ataweka mkazo
katika ajira na fursa za kupata kipato katika kilimo, biashara
ndogondogo na huduma za uzalishaji viwandani. “Kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Kazi na
Ajira, karibu vijana milioni moja wanaingia kwenye soko la ajira kila
mwaka, lakini 200,000 tu ndiyo wanaoajiriwa. Huu uwiano mbaya kama
hautashughulikiwa unaweza kusababisha matatizo ya kijamii na kisiasa,”
alisema.
Uzalishaji viwandani
Wasira alisema ataweka kipaumbele cha juu katika
kuleta mageuzi ya uchumi na kutengeneza ajira endelevu zenye hadhi na
uanzishaji viwanda utapewa msukumo ili iwe injini ya chanzo cha ajira.
Uvuvi
Wasira alisema uwezekano wa kukua kwa sekta ya
uvuvi inawezekana, kwani Taifa limejaliwa kuwa na pwani, maziwa na mito
ambayo ataweka dhamira ya kuleta mabadiliko katika sekta hiyo ili iwe
biashara yenye tija na kuongeza uzalishaji wa kipato kwa watu wengi
wanaojishughulisha na uvuvi.
Mapinduzi ya kilimo
CHANZO: MWANANCHI
“Mkazo wangu utakuwa katika kuimarisha vitendea kazi na kukuza
stadi za kiteknolojia ili uvuvi uwe na uzalishaji zaidi, kupanua masoko
na kuhamasisha uongezaji wa thamani ili kukuza sekta ya uvuvi,” alisema
Wasira.
Mapinduzi ya kilimo
Wasira alisema Watanzania wengi wanategemea kilimo
ili kuendesha maisha yao, hivyo serikali yake itatoa kipaumbele cha juu
katika mapinduzi ya kilimo na uchumi wa vijijini ili kufanya uwe na
uzalishaji wa juu ambao utaleta mabadiliko katika maisha ya Watanzania. “Kwa kuzingatia uwezekazo mkubwa ambao Tanzania
inao katika kilimo na idadi kubwa ya watu wanaoishi vijiji asilimia 70
hadi 75 wanaendesha maisha yao kutokana na kilimo na uchumi wa vijijini,
hivyo nitajitahidi kuendeleza sekta hii ili kuleta mabadiliko na
kukifanya kilimo kiwe cha kisasa,” alisema.
Alisema anayo dhamira ya kuongeza ubora wa
uzalishaji kwenye ngazi ya shamba ili kukuza kiwango cha vipato vya
Watanzania walio wengi ambao wanajishughulisha na kilimo. “Mikakati itakayotumiwa ili kuongeza uzalishaji
kwenye kilimo ni kutumia njia bora za kilimo, sayansi na teknolojia na
ubunifu kwa namna ya utafiti, huduma za ugani, miundombinu vijijini kama
barabara, umeme na umwagiliaji. Katika mchakato huo uendelezaji masoko
utapewa mkazo wa pekee ili kuhakikisha kinachozalishwa kinapata soko la
uhakika,” alisema.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment