Makamu mwenyekiti wa CUF, Juma Duni Haji.
Baada ya kuhitimu shahada ya kwanza, aliajiriwa kama
mwalimu wa Sekondari ya Beit Al Ras, wakati huo ikiitwa Gamal Abdil
Nassir (jina la Rais wa zamani wa Misri), na baada ya mwaka mmoja
kahamishiwa Sekondari ya Lumumba na kufundisha kidato cha tano na sita
na baadhi ya wanafunzi wake ni “magwiji” wa siasa za Zanzibar; Ismail
Jussa, Thuwayba Kisasi na wengineo.
Historia yake
Historia yake
Juma Duni Haji ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Wananchi (CUF) ngazi ya Taifa na ni Waziri wa Afya wa Serikali ya
Zanzibar. Juma Duni alizaliwa Novemba 26, 1950, Zanzibar (Novemba mwaka
huu anatimiza miaka 65).
Alianza elimu katika Shule ya Msingi Mkwajuni
mwaka 1959 hadi 1965 kisha akajiunga na Shule ya Sekondari Gamal Abdel
Nassar (siku hizi inaitwa “Beit el Ras”) mwaka 1966 na kuhitimu mwaka
1969.
Duni aliendelea na sekondari ya juu (kidato cha
tano na sita) katika Chuo cha Lumumba, Zanzibar kati ya mwaka 1970–1971.
Wakati akisoma Sekondari ya Beit el-Ras na Sekondari ya Lumumba,
alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa ASP.
Duni alidahiliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
ambako alisoma Shahada ya Sayansi katika Elimu (BSC Education) kati ya
mwaka 1972 hadi 1975.
Baada ya kuhitimu shahada ya kwanza, aliajiriwa
kama mwalimu wa Sekondari ya Beit Al Ras, wakati huo ikiitwa Gamal Abdil
Nassir (jina la Rais wa zamani wa Misri), na baada ya mwaka mmoja
akahamishiwa Sekondari ya Lumumba na kufundisha kidato cha tano na sita
na baadhi ya wanafunzi wake ni “magwiji” wa siasa za Zanzibar; Ismail
Jussa, Thuwayba Kisasi na wengineo.
Mwaka 1978–1979, Duni alikwenda masomoni
Uingereza, akasoma na kuhitimu Stashahada ya Juu ya Elimu katika Chuo
Kikuu cha Reading na aliporejea alihamishiwa Ofisi Kuu ya Wizara ya
Elimu na kupewa wadhifa wa Ofisa Mipango ya Elimu.
Duni alipata mafunzo mengine muhimu ya kitaaluma
nchini Nigeria mwaka 1980 juu ya Mipango ya Elimu na mwaka 1982
alipelekwa Japan kujifunza kwa kina Mipango ya Kiuchumi.
Pia, Mwaka 1980 Rais Aboud Jumbe, alimteua Juma
Duni kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mipango (Zanzibar) na baadaye kuwa
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango (Executive Secretary Planning
Commission). Duni alianza safari ya kisiasa kwa “kulazimishwa”
mwaka 1984, baada ya serikali ya Muungano kutoa Waraka wa Serikali
(white paper) na kutakiwa wananchi watoe maoni yao juu ya hali na
matatizo ya Muungano.
Makatibu wakuu wa Serikali ya Zanzibar ya wakati
huo akiwemo yeye walitoa maoni dhidi ya muungano, uhuru huo wa kitaalamu
uligeuzwa kuwa mchungu kwani walisingiziwa kwamba wamefanya kinyume na
walivyoagizwa na baadhi yao wakapewa onyo kali na wengine wakateremshwa
vyeo.
Duni aliteremshwa cheo kutoka wadhifa wa Katibu
Mkuu hadi mwalimu wa kawaida kwa Tangazo la Rais, akatakiwa kwenda
kufundisha Shule ya Mikunguni.
Mbio za ubunge
Mwaka mmoja tangu aanze kufundisha Mikunguni akaambiwa
anashiriki siasa hapo shuleni na kuwatia kasumba chafu wanafunzi wa
shule hiyo na hivyo akahamishiwa Shule ya Lumumba.
Baada ya muda mfupi huko Lumumba nako akahamishwa
na kurudishwa Ofisi Kuu ya Elimu kama Ofisa Mipango wa Elimu. Akiwa
Ofisa Mipango alituhumiwa kuwa anakwenda nyumbani kwa Maalim Seif
Sharrif usiku wa manane kufanya siasa na ikaipasa serikali imhamishie
Idara ya Ukaguzi.
Kwenye idara ya ukaguzi nako akaambiwa anafanya
siasa kwa kutoka saa za kazi na kukaa kwenye vibaraza (vijiwe),
akarejeshwa tena Ofisi Kuu na huko akaambiwa kwamba anaondoka kwenda Dar
es Salaam bila kuaga kwa wakubwa zake na mara nyingi ameonekana usiku
akifanya siasa na Marehemu Abrahman Babu (ambaye wala hakuwepo Zanzibar
wakati huo).
Wizara ilipomchoka na kukosa cha kumfanya
ikamrejesha kwa Mkurugenzi Mkuu wa Utumishi ambaye hakuwa na kazi ya
kumpa, sana sana alimwambia abaki nyumbani bila kazi kwa zaidi ya miezi
sita.
Baadaye, mkurugenzi wa utumishi akamrejesha tena Wizara ya Elimu baada ya Duni kuwauliza kosa lake na kushindwa kumueleza.
Duni alipoona visa hivyo vinamuumiza na
vinamchosha aliomba ruhusa ya likizo bila malipo kwenda kusoma, ombi
ambalo nalo pia lilikataliwa na ndiyo akaamua mwenyewe kuondoka na
kwenda kujisomesha kwa fedha zake Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza
na kuhitimu stashahada ya Juu ya Biashara kati ya mwaka 1993-1994.
Wakati alipofika Uingereza akatumiwa barua ya
kuachishwa kazi na kupoteza haki zake zote za miaka 18 ya utumishi
serikalini. Mwaka huo 1994 akiwa bado nchini Uingereza, akaunganisha
tena kwa shahada ya uzamili/umahiri akibobea kwenye usimamizi wa
Rasilimali Watu na kabla hajaihitimu akarejea nchini ili kusaidia
upinzani kujipanga kiuchaguzi.
Moja kwa moja akajiunga na vuguvugu la uchaguzi wa
kwanza wa vyama vingi. Chama Cha Wananchi (CUF) kikamteua kuwa Mgombea
mwenza wa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya
chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba wakati bado hajakamlisha shahada
yake ya pili ya uongozi na utawala.
Tangu ajiunge CUF ameshika nyadhifa mbalimbali kwa
nyakati tofauti, amekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar na
Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha CUF Taifa mwaka 1999–2003, amekuwa
Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha CUF kati ya mwaka 1997-2010, amekuwa Naibu
Katibu Mkuu CUF (Zanzibar) kuanzia mwaka 1999-2010, Amekuwa Mjumbe wa
Baraza Kuu la Uongozi Taifa CUF Taifa kati ya mwaka 1999-2014.
Hivi sasa yeye ni Makamu Mwenyekiti wa CUF, nafasi
aliyochaguliwa mwaka 2014 na analazimika kuishikia hadi uchaguzi
mwingine wa ndani ya chama chake utakapofanyika, mwaka 2019.
Mbio za ubunge
Juma Duni Haji si mgeni katika masuala ya
“kibunge’ au ya kiuwakilishi. Mwaka 1997 aligombea nafasi ya Ujumbe wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar (Mwakilishi wa Zanzibar anafanya kazi
kama za Mbunge wa Bunge la Tanzania) Jimbo la Mkunazini, akashinda na
kuwa mwakilishi kuanzia mwaka 1997-2000.
Mbio za urais
Nguvu zake
Mwaka 2009 aliteuliwa na Rais Amani Abeid Karume kuwa Mjumbe wa
Baraza la Wawakilishi kwa mara ya pili, akakaa katika wadhifa huo hadi
uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ulipofanyika na kuundwa kwa Serikali ya
Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK).
Katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Juma
Duni aliteuliwa na Rais wa Zanzibar kuwa mwakilishi na kisha akateuliwa
kuwa Waziri wa Afya wa Zanzibar, wadhifa ambao ameushikilia hadi sasa.
Mbio za urais
Juma Duni ni mmoja wa Watanzania ambao wamewania
kuongoza taasisi ya urais kwa muda mrefu sana, japokuwa hajawahi
kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini kwa vipindi
takribani vitatu yeye amekuwa ni Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Amefanya hivyo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1995,
mwaka 2005 na mwaka 2010, mara zote akiwa mgombea mwenza wa Profesa
Ibrahim Lipumba wa CUF.
Juma Duni ni mmoja wa wanasiasa ambao wanatajwa
sana kuwa na sifa, uwezo, vigezo na kila sababu ya kuweza kuwa rais wa
nchi. Nilipomuuliza mipango yake juu ya mawazo hayo ya wananchi juu yake
alinieleza kuwa yeye ni mtumishi wa watu na kila mara alikotumwa
alikwenda. Juma Duni alinivunja mbavu aliponiambia kuwa hata leo
akiteuliwa kwenda kuongoza ‘kijiji au kitongoji’ ilimradi Watanzania
wametaka hivyo, ataitikia wito.
Nguvu zake
Nguvu ya kwanza inayompa Juma Duni uwezo mkubwa wa
kuongoza nchi ni elimu yake. Kiongozi huyu ana shahada mbili za Chuo
Kikuu na Stashahada mbili za Juu kutoka katika Vyuo Vikuu
vinavyoheshimika duniani.
Zaidi ya yote amechanganya taaluma akibobea kwenye
masula ya sayansi, elimu, uchumi, Biashara na Usimamizi wa Rasilimali
Watu. Ni wanasiasa wachache sana wenye upeo mkubwa katika taaluma zaidi
ya mbili au tatu na taaluma hizi zinampa sifa na uwezo zaidi wa kuwa
rais bora.
Lakini jambo la pili ni uzoefu kazini, kiongozi
huyu ameanza kazi kama mwalimu na kupanda hadi kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara na baadaye Waziri. Na hata ndani ya chama chake amepanda kutoka
kuwa mwanachama wa kawaida, Naibu Katibu Mkuu hadi kuwa Makamu
Mwenyekiti wa chama Taifa.
Lakini jambo muhimu kuliko yote, Juma Duni ni
mpigania haki mkongwe na mfungwa wa kisiasa ambaye hakuwahi kuogopa kifo
wala mateso. Mwaka 1997 hadi 2000 (miaka minne), alikuwa miongoni mwa
wanachama na viongozi wa CUF waliotuhumiwa “kutaka kuipindua serikali ya
Zanzibar”, wakapewa kesi ya uhaini “Kesi Maarufu kwa jina la Machano
Khamis Ali na wengine” na kukaa gerezani miaka minne kabla mahakama
haijatoa hukumu ikisisitiza kuwa hakuna uwezekano wa serikali ya
Zanzibar kupinduliwa kwa sababu iko chini ya Muungano.
Lakini pia mwaka 2001–2002 (zaidi ya mwaka mzima),
Juma Duni alikuwa mmoja wa viongozi wa CUF waliobambikiziwa kesi ya
kisiasa wakihusishwa na kumuua Askari Polisi aliyeuawa Pemba. Cha
kushangaza ni kuwa, mauaji yale ya Pemba yalipofanyika, Juma Duni
alikuwa yuko Unguja, lakini kamatakamata ilipoanza naye akawekwa kwenye
orodha na kukaa gerezani bila sababu.
Uthubutu na uimara wa Juma Duni katika kupita kwenye misukosuko mikubwa unamfanya awe mwanasiasa wa aina yake hapa Tanzania.
Udhaifu wake
Nini kitamfanya apitishwe
Nini kinaweza kumwangusha?
Asipopitishwa (Mpango B)
Hitimisho
Wanasiasa wengi huwa ni waoga kukabiliwa na changamoto za dola
na kuhofia kukaa gerezani, wengi wa wanasiasa huona shida sana kukaa
gerezani siku moja au wiki moja, achilia mbali mwezi.
Juma Duni amekaa gerezani kwa kuonewa kwa miaka
mitano, yeye pamoja na wenzake, waliitwa wahaini lakini walithubutu
kuendelea na mapambano bila kurudi nyuma. Hii ni sifa ya kipekee.
Na mwisho, Juma Duni ni Mtu wa kawaida sana.
Ukipishana naye barabarani huwezo kujua kama ni waziri katika serikali
au Makamu Mwenyekiti wa Chama kikubwa kama CUF.
Wakati tuko Bunge Maalum la Katiba ungemkuta
anatembea barabarani na kufanya manunuzi binafsi kwa mguu na akitoka
huko akakutana na muuza muhogo, angejinunulia na kuanza kula polepole
huku akiongea na vijana, hana makuu na ni mmoja wa viongozi ambao
wanajali sana utu wa watu wa kawaida, kushirikiana na watu hao na
kuwasaidia kimawazo na kifikra.
Udhaifu wake
Moja ya mambo ninayoyachukulia kama udhaifu wa
Juma Duni ni ubishi kupita kiasi akiwa anadai jambo ambalo anadhani
linapindishwa. Pamoja na kuwa viongozi hupaswa kudai haki sana lakini
wanapaswa kutokuwa “ving’ang’anizi” wa kudai haki kiasi cha kunyima
upande wa pili fursa ya kufanya maamuzi sahihi. Duni akitaka jambo lake
lazima liwe na huenda hii siyo sifa muhimu kwa viongozi wa kisasa.
Lakini jambo la pili ni tabia yake ya kuibua kauli
tata na zinazoibua mijadala mikubwa na kuikwaza sana CCM ambayo chama
chake kinashirikiana nayo katika serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.
CCM mara kadhaa wamesikika wakimshutuma Juma Duni kwa tabia yake ya
kuwananga kama “masultani weusi”.
Kauli hizi za Juma Duni zimewahi kugeuzwa na CCM
wakasisitiza kuwa amewaeleza Wazanzibari kuwa “utawala wa mtu mweusi
mwisho ni kesho”. Mmoja wa viongozi wa CCM ambao nimeongea naye
ameniambia kuwa kauli zake zinawaudhi sana na kwamba si mfano sahihi.
Nami kwa upande wangu nimeona kuwa zinaweza kuwa sababu ya CCM
“kujifanya” wamechokozwa na wao wakaendeleza chokochoko ambazo mwisho wa
siku haziiweki Zanzibar mahali sahihi, hasa katika Serikali ya Umoja wa
Kitaifa.
Nini kitamfanya apitishwe
Jambo la kwanza linaloweza kuifanya CUF impitishe
Juma Duni kuwa mgombea Urais wa chama hicho na baadaye Ukawa ni kwa
sababu ya uzoefu wa ugombea mwenza wa kiti cha urais na mtu ambaye
amezunguka sana katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Hilo
pekee linatosha kabisa kumuamini na kumpa kazi hii kwa sababu ana
uzoefu, uwezo, sifa na anajua namna ya kufanya mambo yaende.
Lakini pili, naona Juma Duni akipitishwa kugombea
urais wa Tanzania kwa tiketi ya CUF na baadaye Ukawa ikiwa mgombea urais
wa Ukawa atapaswa kutoka Zanzibar. Nawaona wanasiasa wachache sana
ndani ya upinzani kule Zanzibar, wenye uzoefu, haiba, elimu na uwezo wa
kumfikia yeye ikiwa kweli nchi inahitaji kuwa na viongozi imara
watakaoivusha.
Nini kinaweza kumwangusha?
Jambo moja litakalomkwamisha Juma Duni katika kupita kwenye
chujio la CUF na Ukawa katika kusaka tiketi ya uongozi wa nchi ni ikiwa
ataamua kugombea uwakilishi. Kama nilivyoeleza, Juma Duni kuna nyakati
ni kiongozi mbishi sana na akiamua jambo lake analisimamia. Ikiwa
ataamua kugombea Uwakilishi (Na nimeambiwa kuwa ameanza harakati hizo)
ina maana hatapita kwenya mchujo wa kuchukua nafasi ya urais wa Tanzania
kwa tiketi ya Ukawa.
Lakini jambo la pili ambalo litamkwamisha kwenye
mchujo ni la moja kwa moja. Ni hukumu ya yeye ni Mtanzania wa asili ya
wapi. Hukumu hii inatokea pale ambapo CUF na labda Ukawa wataamua kuweka
mgombea urais kutika upande wa Tanzania Bara, uwezekano wa Juma Duni
kuwa rais wa Tanzania mwaka huu, utafikia tamati mahali hapo.
Asipopitishwa (Mpango B)
Namtazama Juma Duni katika mipango miwili ikiwa
hatagombea urais wa Tanzania. Mpango wa kwanza ni kupewa fursa ya
kuendeleza kazi aliyoifanya mwaka 1995, 2005 na 2010 ya kuwa mgombea
mwenza wa urais wa Tanzania na mara hii nadhani akiungwa mkono na vyama
vya Ukawa.
Pili, ni kugombea uwakilishi ili kutafuta tiketi
ya kuwahudumia zaidi wananchi na hata kuendelea kuwa waziri ikiwa Rais
wa Zanzibar ajaye ataamua kumteua na ama kupewa jukumu la kuvaa viatu
vya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka
huu kule Zanzibar. Jambo hili litaweza kutokea ikiwa CUF ndiyo itakuwa
“Kaka Mkubwa” katika serikali ya pamoja inayoendelea kikatiba upande wa
Zanzibar.
Hitimisho
Hakika, tutakubaliana kuwa nchi hii ina viongozi
wenye uwezo mkubwa sana na wanaweza kabisa kulivusha taifa ikiwa
watapewa nafasi. Mmoja wa viongozi hao ni Juma Duni.
Juma Duni ameniambia kuwa moja ya maumivu makubwa
aliyowahi kuyapata katika siasa za nchi hii ni kushindwa kuonana na baba
yake mzazi (Mzee Duni), akiwa gerezani. Mbaya zaidi, siku ambayo
alikuwa amuone baba yake kwa mara ya mwisho, ilikuwa siku ambayo Duni na
wenzake waliletwa mahakamani Vuga kusikiliza kesi ya uhaini.
Baba yake Juma Duni, (Mzee Duni), aliomba msaada
kwa askari wa FFU, ili amsalimie mwanaye ndani ya jengo la mahakama, na
kwa bahati mbaya mzee yule alikua na matatizo ya usikivu (uzito wa
kusikia) Askari mmoja akamuamrisha Mzee Duni aondoke mara moja, kwa
sababu mzee yule hasikii vizuri hakumuelewa askari na akajaribu kuongeza
hatua moja mbele, askari yule akampiga kofi zito mzee wa watu na
kuanguka chini, hakuweza kumsogelea wala kumsalimu.
Tukio lile lilitokea huku Juma Duni akiona,
ameniambia aliumia sana na kwa bahati mbaya, huo ndiyo ukawa mwisho wa
Juma Duni kumuona mzee wake. Muda si mrefu Mzee Duni (baba) alifariki
dunia mwanaye Juma Duni akiwa gerezani na hakuruhusiwa kumzika.
Pamoja na mambo makubwa aliyopitia, Juma Duni
ameendelea kuwa mtumishi wa Wazanzibari wote akisimamia majukumu yake
kufa au kupona. Na yeye, namtakia kila lililo jema katika safari na
ndoto zake kisiasa.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment