Naibu Spika, Job Ndugai.
Mgomo usio na kikomo uliotangazwa na wafanyabiashara
nchini kuanzia jana umelitikisa Bunge, huku wabunge wakitaka serikali
ilegeze masharti ili Mwenyekiti wa wafanyabishara, Johnson Minja,
aachiwe kwa dhamana.
Jana asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni, wabunge kadhaa walisimama kuomba mwongozo wa kiti wakitaka mgomo huo ujadiliwe kama jambo la dharura kwa kuwa unaumiza uchumi wa nchi, unaikosesha serikali mapato na usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Aliyeanza kuzungumzia suala hilo ni Mbunge wa Njombe Kaskazini (CCM), Deo Sanga, ambaye alisema mgomo wa wafanyabiashara ulianza kidogo kuanzia Mbeya, Arusha, Tabora na Dodoma, lakini serikali haijatoa majibu ya uhakika.
Katika mwongozo wake, Sanga alitaka serikali itoe kauli ya uhakika kutokana na mgomo huo wa wafanyabiashara. Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari, alisema hali ni tete nchini kufuatia wafanyabiashara kugoma kufungua maduka, akisema dola nyingine huanguka kwa mambo kama haya ya migomo.
Alisema hoja hiyo iliibuliwa Ijumaa iliyopita na Mbunge wa Kisarawe (CCM), Seleman Jafo, akieleza kuwa wafanyabiashara wanalalamikia ongezeko la kodi kwa asilimia 100, lakini serikali imekaa kimya na jana wafanyabiashara mkoani Arusha waligoma kufungua maduka.
Naye Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage, alisema mjini Tabora maduka yamefungwa tangu juzi na wananchi wanahangaika kwa kukosa huduma. Alisema inashangaza kwamba, pamoja na unyeti wa tatizo hilo, serikali imeendelea kukaa kimya bila kutoa tamko lolote huku ikikosa kodi.
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, aliomba mwongozo kwa kutumia kanuni ya Bunge ya 47 (i), (ii), (iii) na ya 48 (3), akitaka Bunge lijadili mgomo huo kwa dharura kwa kuwa hali ni mbaya nchini. “Suala la wafanyabiashara kufunga maduka ni la dharura. Maduka hayafunguliwi, serikali haipati kodi, Taifa limesimama, tunajiuliza serikali ina taarifa za kweli? Tunataka tujadili leo (jana) ili tupate kauli ya serikali kwa sababu Bunge linaahirishwa kesho (leo),” alisema.
Alisema wafanyabiashara wana malalamiko mengi ya msingi likiwamo ongezeko la kodi kwa asilimia 100, mawakala wanaokusanya kodi kutoa risiti isiyoendana na kiasi kilicholipwa na kutaka kiongozi wao aachiwe kwa dhamana. Alisema malalamiko aliyoyapata kutoka kwa wafanyabiashara kuhusu mawakala ni kwamba mfanyabiashara anayelipa kodi Sh. milioni 40 anapewa risiti ya malipo ya Sh. milioni 10.
Kadhalika, alisema kosa la Minja lina dhamana kwa mujibu wa sheria, kwa kuwa hajaua, hajabaka, hajafanya uhaini wala hajafanya unyang’anyi kwa kutumia silaha. Baada ya maelezo hayo, Naibu Spika, Job Ndugai, alitoa fursa kwa serikali kutoa maelezo kuhusu hoja hizo za wabunge.
Akijibu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenister Mhagama, alisema Ijumaa iliyopita, serikali chini ya uratibu wa Waziri Mkuu, ilikutana na wafanyabiashara na kupokea kilio chao cha ongezeko la kodi, matumizi ya mashine za EFDs na kesi ya Minja.
Alisema baada ya majadiliano marefu, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alizielekeza Wizara za Fedha na Viwanda na Biashara chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, kwamba ndani ya mwezi mmoja viwe zimefanyika vikao kadhaa kumaliza mgogoro wa ongezeko la kodi na matumizi ya mashine za EFDs.
Alisema maelekezo mengine ni kuona namna ambavyo Minja anaweza kuachiwa. Hata hivyo, Mhagama alisema juzi serikali ilipokea barua ya wafanyabiashara ambayo inamkataa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum kuwa mwenyekiti wa vikao kama alivyokuwa ameelekeza Waziri Mkuu.
Alisema jana serikali iliitisha kikao cha dharura kuijadili barua hiyo na kwamba serikali imelenga kumaliza mgogoro kati yake na wafanyabiashara kwa njia ya majadiliano. Baada ya maelezo hayo, wabunge kadhaa walisimama na Rage alipopewa nafasi aliomba wabunge waipe muda serikali kufuatilia jambo hilo na kuwataka wafanyabiashara wafungue maduka.
Naye Mdee aliendelea kushikilia msimamo wake wa kutaka Bunge lijadili jambo hilo kwa dharura kwa kuwa huduma zimekosekana na kutaka serikali iseme ni lini maduka yatafunguliwa na ni lini Minja ataachiwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Luhaga Mpina, alipinga maelezo ya serikali akieleza kuwa Machi 10, mwaka huu, kamati yake ilikutana na wafanyabiashara na Machi 13, kamati iliitisha kikao kati yake, wafanyabishara, Mamlaka ya Mapato (TRA) na serikali, ambayo pamoja na mambo mengine ilibainika kwamba serikali ilizembea kuitisha vikao kwa miezi saba tangu tume ya maridhiano ilipoundwa Julai mwaka jana.
“Kamati yangu ikaiagiza serikali iitishe kikao ndani ya siku 14, kwa bahati nzuri siku nne baadaye kamati ilipata taarifa kwamba serikali imeitisha kikao,” alisema. Alisema Ijumaa iliyopita, viongozi wa kamati, serikali na wafanyabiashara walikaa kwenye kikao kwa takribani saa nne, na miongoni mwa makubaliano ni pamoja na Minja kupata dhamana ili majadiliano yaweze kuendelea vizuri.
Alisema inashangaza kuona kwamba pamoja na mazungumzo ya kina, serikali imeshindwa kusimamia na kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa.
Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, alitaka wabunge wanaotaka Minja atoke wakajenge hoja mahakamani kwa kuwa Bunge halina mamlaka ya kuingilia uhuru wa mahakama. Alisema Minja hakunyimwa dhamana kama inavyodaiwa, bali alikiuka masharti ya dhamana aliyopewa na serikali kutoa taarifa juu ya ukiukwaji huo hali iliyosababishwa kukamatwa.
Maelezo hayo yalimfanya azomewe na baadhi ya wabunge, lakini aliendelea kusisistiza kuwa Minja aliachiliwa kwa dhamana, lakini alikiuka masharti kwa kuitisha vikao na migomo, ndipo serikali ilipoieleza mahakama ambayo ilimfutia dhamana. Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde, aliendelea kushikilia kuwa serikali imeendelea kushikilia msimamo wa kumnyima dhamana wakati hajatenda kosa la kumnyima dhamana.
Alisema makosa yasiyo na dhamana ni unyang’anyi wa kutumia silaha, ubakaji, uhaini, uuzaji wa dawa za kulevya na mauaji, ambayo hayajatendwa na Minja. Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia, alisema mgogoro huo umeanza tangu mwaka jana na kwamba kama serikali ikiweka dhamira ya dhati inaweza kuumaliza kwa urahisi.
Naye Nassari alisema serikali inaweza kuomba mahakama impe dhamana kwa kuwa ndiyo iliyolalamika hadi akanyimwa dhamana. Baada ya majadiliano hayo, Naibu Spika, Job Ndugai, aliitisha kikao cha dharura cha kamati ya uongozi kujadili jambo hilo na kupata muafaka kabla ya kuahirishwa kwa kikao cha jana mchana.
Aidha, kabla ya kuahirisha kikao, Ndugai alisema kamati ya uongozi imeafikiana kwamba serikali iendelee kufanya mazungumzo na wafanyabiashara, lakini muda wa kumaliza jambo hilo uwe chini ya mwezi mmoja.
Kwa mara nyingine tena, wafanyabiashara katika mikoa mbalimbali kuanzia jana waligoma kufungua maduka ili kushinikiza mwenyekiti wao aachiwe kwa dhamana.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment