Waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Wizara ya Maliasili na Utalii, imesema ujangili ni
suala la watu wachache wenye roho mbaya wanaotaka utajiri wa haraka
wakishirikiana na watu waliopo kwenye mtandao ndani na nje ya nchi ili
kupata masoko.Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro
Nyalandu, wakati akihojiwa katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na
kituo cha ITV. Alisema ulinzi wa wanyamapori, misitu na mazao ya misitu na mali
kale ni changamoto kubwa kwa kuwa idadi ya watu inaongezeka siku hadi
siku na ardhi ikiwa ni ile ile.
Alisema haiwezekani Waziri au viongozi wa kisiasa wenyewe waweze
kukabiliana na ujangili na ndiyo maana wameongeza nguvu kazi yenye
mafunzo thaibiti na vitendea kazi vya kisasa. “Tumeongeza idadi ya askari wanyamapori, mfumo wa utendaji kazi na
vitendea kazi, magari na kutengeneza mifumo ya utawala ikiwamo kuanzisha
Mamlaka ya Wanyamapori kwa kuwa na kikosi cha kupambana na ujangili
uliokithiri,” alisema.
Alisema serikali inalitazama suala la ujangili kama ni tatizo
linaloendelea na kwamba kuna juhudi zinazoonekana na zisizoonekana
zinazofanywa. Alisema Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kuwa na tembo wengi na ya pili Afrika kwa kuwa na wanyamapori wengine.
Alisema siyo lazima kuchoma meno ya Tembo kwani kuna meno makubwa
mbayo yanatoweka na miaka ya baadaye yatakuwa ni kivutio kwa watu
mbalimbali na kwamba yanaondolewa katika soko kwa ajili ya kuyahifadhi
kwa uwazi baada ya kuwepo kwa makubalino ya mifumo ya kikompyuta yenye
kutambua meno hayo.
Nyalandu alisema ushirikiano wa Watanzania na vyombo vya ulinzi na
usalama, ndiyo wa kukomesha vitendo hivyo ili kupunguza matukio ya
ujangili. Alisema zaidi ya asilimia 70 ya watalii wanaofika nchini wanakuja
kuona wanyamapori na kupanda mlima Kilimanjaro na ndiyo maana serikali
imeiimarisha ulinzi wa wanyamapori.
Alisema serikali iko katika mpango wa kushirikiana na wadau wa
ndani na nje kwa kuifanya Tanzania iendelee kuheshimika kwa ulinzi wa
wanyamapori kama tembo na kwamba wako mbioni kutoa sensa ya tembo na
faru waliopo nchini.
Alisema mfumo wa kuwezesha kuwahesabu wanyama hao umekamilika kwa
kushirikiana na Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (Tawiri) na
mashirika ya Marekani na Ujerumani kwa kutengeneza mfumo wa kuhesabu
wanyama na kwamba ndani ya kipindi kifupi serikali itaeleza hali halisi
ikoje.
“Tumefanikiwa kuishawishi jamii ya kimataifa kuwa changamoto
zilizopo zimedhibitiwa na Tanzania ilishatangaza kuachana na uuzaji wa
meno ya tembo nje ya nchi, na tumefanya hivyo ili kupambana na mpango wa
ongezeko la mahitaji katika masoko nchini China na kwingine,
tunawalinda kwa kudhibiti masoko yanayozidi kuongezeka na kupandisha bei
ya nyara,” alibainisha. Umuhimu wa wananchi kushiriki kutoa maoni
katika miswada hiyo kabla ya kupitishwa na Bunge kwenye mkutano wa 19
unaoendelea mjini Dodoma.
Naye Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe,
ameandikiwa barua na wadau hao wakimuomba atumie nafasi yake kama
msemaji mkuu wa kambi hiyo bungeni kuishauri serikali iwasilishe miswada
hiyo chini ya mfumo wa kawaida na siyo chini ya hati ya dharura kwani
unawanyima wananchi fursa ya kutoa maoni yao kwenye miswada hiyo kabla
ya kupitishwa na Bunge.
Tangu serikali iseme kuwa inakusudia kuwasilisha miswada hiyo chini
ya hati ya dharura, wadau wa habari wamekuwa wakiomba ibadili msimamo
kwani kufanya hivyo kutawanyima wananchi fursa ya kutoa maoni juu ya
miswada hiyo kabla ya kuwa sheria.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment