Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Balozi Seid Ali Idd, amesema serikali itakuwa tayari kupambana
na mtu au kikundi chochote kitakachothubutu kuharibu Mapinduzi.
Alitoa kauli hiyo jana kwenye ufunguzi wa matembezi ya Jumuiya ya Vijana
wa CCM (UVCCM) kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema serikali ya Mapinduzi ni ya wananchi wenyewe ambao hawako tayari
kuona uhuru na ukombozi wao ukipuuzwa na watu wachache kwa ajili ya
maslahi yao.Alisema kuwa serikali ya Zanzibar bado ipo imara wakati wowote na wapo makini dhidi ya chokochoko zozote. “Tunashangaa baadhi ya watu sasa waliokataa kuyatambua Mapinduzi, sasa nao wanaimba nyimbo za kusifu kwa unafiki,” alisema Balozi Seif bila kuwataja.
Balozi Self alisema unafiki wa watu hao hujidhihirisha kutokana na vitendo vyao kwa kuwa wanayoyasema ni mambo tofauti na yale yaliyoko kwenye mioyo yao na kuwataka wananchi wa Zanzibar kuwa macho na watu hao. Aidha Muungano, alisema kitendo chochote cha kudhoofisha Muungano kamwe kisipewe nafasi kwani Muungano wa Tanganyika na Zanzibar si wa makaratasi bali ni damu.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment