Maofisa wa eneo huria la
uwekezaji la Jafza katika Bandari Jebel Ali ya jijini hapa wamelalamikia
urasimu katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji Tanzania na kudai kuwa ndiyo
yanayokwamisha shughuli nyingi za maendeleo.
Maofisa hao wameitaka Serikali ya
Tanzania kujenga Bandari ya Bagamoyo ili kuvutia wawekezaji badala ya kusubiri
ijengwe na wawekezaji hao.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya DP
World wanaoisimamia Bandari ya Dubai, Mohamed Sharaf alisema hayo jana wakati
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na ujumbe wake walipotembelea bandarini hapo ikiwa ni
sehemu ya ziara yake ya siku saba ya kujenga uhusiano na kutafuta maeneo ya
uwekezaji.
Sharaf alisema walifika Tanzania
kutafuta maeneo na kufahamu utaratibu wa namna gani wanaweza kuwekeza, lakini
walikatishwa tamaa na urasimu uliopo kutoka kwa baadhi ya watendaji.
Alisema kama Serikali ya Tanzania
itafanikiwa kudhibiti hali hiyo, huenda wawekezaji wengi watajitokeza kuwekeza.
Akizungumzia ujenzi wa Bandari ya
Bagamoyo ambayo Serikali imeingia ubia na China, aliishauri ikamilishe ujenzi
kabla ya kuwakaribisha wawekezaji.
na imewezesha kuunganisha mataifa
zaidi ya 130 duniani yanayoitumia bandari hiyo.
Sharaf alisema hadi sasa kitengo cha
makontena kimeboreshwa na kinauwezo wa kuhudumia makontena milioni 15 kwa
mwaka, hatua ambayo imerahisishwa na ufanyaji kazi kwa njia ya mtandao.
“Tunafanya kazi usiku na mchana, kwa
sasa kuna kazi (transactions) zaidi ya milioni 18 ziko kwenye mtandao duniani,
ndizo zinazofanya kazi ya kuliingizia fedha Taifa letu,” alisema.
Mapema jana asubuhi, Waziri Mkuu
alikuwa na mazungumzo na Maofisa Watendaji Wakuu wa Emirates National Oil
Company (ENOC), Said Foemy na Fandraj Govindaraj kabla ya kutembelea Kituo cha
Biashara Dubai na kuonyeshwa mpango wa kituo hicho kujenga mji wa kisasa pamoja
na uwanja wake wa ndege.\
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment