Boniface Wambura,Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeanika majina
ya nyota wa kigeni walioombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) baada
ya dirisha dogo la usajili msimu wa 2014/2015 kufungwa usiku wa kuamkia
jana.
Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, alisema jijini Dar es
Salaam kuwa wachezaji 15 kutoka nje wamembewa ITC kutoka nchi
mbalimbali huku akieleza kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya
TFF itakutana muda wowote kupitia usajili wa dirisha dogo.Aliwataja wachezaji walioombewa ITC kwa timu za Ligi Kuu ni Abdulhalim Humoud kutoka Sofapaka ya Kenya kwenda Coastal Union, Brian Majwega kutoka KCC (Uganda) kwenda Azam FC, Castory Mumbara kutoka Three Star Club (Nepal) kwenda Polisi Mara, Charles Misheto kutoka SP Selbitiz (Ujerumani) kwenda Stand United na Chinedu Michael Nwankwoeze kutoka Nigeria kwenda Stand United.
Dan Sserunkuma kutoka Gor Mahia (Kenya) kwenda Simba, Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Bonsucesso FC (Brasil) kwenda Yanga, Halidi Suleiman kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United na Juuko Murshid kutoka SC Victoria University (Uganda) kwenda Simba. Kpah Sean Sherman kutoka Aries FC (Liberia) kwenda Yanga, Meshack Abel kutoka KCB (Kenya) kwenda Polisi Morogoro, Moussa Omar kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Nduwimana Michel kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Serge Pascal Wawa kutoka El Merreikh (Sudan) kwenda Azam na Simon Sserunkuma kutoka Express FC (Uganda) kwenda Simba.
Orodha hiyo hapo chini inaonesha wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo, waliotemwa na kutolewa kwa mkopo na timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL);
AZAM FC; walioingia ni Wawa, Majwega na Amri Kiemba. Waliotoka ni Ismail Diara raia wa Mali (katemwa) na Mhaiti Lionel Saint-Preux (katemwa).
YANGA; walioingia ni Sherman, Amissi Tambwe, Danny Mrwanda, Athuman Majogo (Friends Rangers) na Emerson (amesajiliwa na kutemwa). Walioondoka ni Hamis Kiiza (katemwa), Omega Seme (mkopo Ndanda FC), Hamis Thabit (mkopo Stand United), Geilson Santos Santana 'Jaja' (ametemwa) na Said Bahanunzi (mkopo Polisi Morogoro).
SIMBA; walioingia ni Sserunkuma, Simon Sserunkuma, Murshid na Hassan Kessy (Mtibwa Sugar). Walioondoka ni Kiemba (Azam), Miraj Adam (mkopo Mtibwa Sugar), Haroun Chanongo (mkopo Stand United), Joram Mgeveke (mkopo Mwadui FC) na Uhuru Seleman (Mwadui FC - Uhuru kavunja mkataba Simba).
COASTAL UNION; walioingia ni Humud na Geofrey Wambura (huru), Bakari Thabit (Friends Rangers). Walioondoka ni Razak Khalfan (mkopo Mwadui FC), Peter Heri (katemwa).
STAND UNITED; walioingia ni Hamis Thabit (Yanga), Chanongo (Simba), Nduwimana (Burundi), Shaban Kondo, Chinedu, Hamis Shengo na Misheto (Ujerumani). Walioondoka ni Nelson Kimath na Omar Mtaki (wote Geita FC), Hussein Chepe na Lucas Charles (wote Polisi Tabora), Robert Magadula na Patrick Mrope (wamevunja mikataba).
MTIBWA SUGAR; walioingia ni Henry Joseph (huru) na Miraj (mkopo Simba) na Ibrahim Jeba (huru). Walioondoka ni Hassan Kessy (Simba).
NDANDA FC; walioingia ni Omega (Yanga), Kigi Makasi (huru). Stamili Mbonde (Villa Squad), Raymond Zabron (Villa Squad), Issa Said (huru), Mohamed Masou (huru) na Zuberi Ubwa (huru). Walioondoka ni Amri Msumi (mkopo Kurugenzi Iringa) na Hamis Saleh (huru).
KAGERA SUGAR; hakuna aliyeingia wala kutoka.
MBEYA CITY; Kipa Kalyesubula Hannington (huru), Juma Issa 'Nyoso' (huru), Idrisa Rashid, Fredy Cosmas, Soneka Peter (U20) na Selemani Hassan (U20). Walioondoka ni Anthony matogolo (mkopo Panone FC), Saad Kipanga (mkopo Polisi Tabora), Ramadhani Abdu (mkopo Majimaji FC), Medson Mwakatundu - U20 (mkopo Rhino Rangers), Ramadhani Kapela - U20 (mkopo Coca Cola Mbeya), Majid Shabani - U20 (mkopo Coca-Cola Mbeya), Abdalah Said - U20 (mkopo Coca-Cola Mbeya) na Waziri Ramadhani - U20 (mkopo Burkinafaso FC).
TANZANIA PRISONS; hakuna aliyeingia wala kutoka.
POLISI MOROGORO; walioingia ni Said Bahanunzi (Yanga), Zahoro Pazi (huru), Meshack Abel (KCB, Kenya) na Iman Mapunda (huru). Walioondoka ni Danny Mrwanda (Simba), Makungu Siame (mkopo Malindi, Unguja), Emilian Mgeta (mkopo Villa Squad) na Mosses Mtitu (Majimaji FC).
RUVU SHOOTING; walioingia ni Mwita Kimaronge (Toto Africans), Betram Mwombeki (huru), Yahya Tumbo (Mtendeni FC, Zanzibar) na Ally Yusuph (Ruvu Shooting B).
JKT MGAMBO; hakuna aliyeingia wala kutoka.
JKT RUVU: hakuna wapya na hawajauza wala kuoa mchezaji kwa mkopo.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment