Mkuu wa Baraza la Ulaya, Waziri Mkuu wa Zamani wa Poland, Donald Tusk
Pengine ulikuwa mkutano mfupi kuliko yote iliyowahi kuitishwa hadi sasa
na Umoja wa ulaya mjini Brussels, lakini safari hii hakujakuwa na
mabishano na sera kuelekea Urusi zinajulikana zimesalia vile vile.
Maripota mjini Brussels wameduwaa:kwa mara ya kwanza kabisa mkutano wa
viongozi wa taifa na serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa ulaya
umemalizika siku moja kabla ya wakati. Kawaida viongozi hao wa mataifa 28
huendesha majadiliano makali yanayopelekea hata mikutano yao kuendelea
hadi usiku wa manane na mara nyengine kurefushwa pia.
Safari hii,mwenyekiti mpya wa baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk
alitamka baada ya karamu ya chakula cha usiku, iliyoaandaliwa baada ya
saa tano za usiku. "Tumemaliza." kikao cha kesho ijumaa hakina haja ya
kuitishwa. Ulikuwa mkutano wa kwanza wa kilele kusimamiwa na Donald Tusk.Alipokuwa
waziri mkuu wa Poland alikwisha shiriki mara 47 katika mikutano kama hii
ya kilele. Anatajikana kuwa mtu mwenye maarifa na aliyebobea.
Tusk alikuwa na mada mbili tu katika ajenda yake ya mazungumzo: Siasa ya
siku za mbele ya Umoja wa Ulaya kuelekea Urusi na mpango wa uwekezaji wa
Umoja wa Ulaya mpango uliolengwa kuinua shughuli za kiuchumi. Mada zote
mbili,hazikuwa za mabishano makubwa. Zote nyengine zitajadiliwa mkutano
mwengine wa kilele utakapoitishwa mwezi februari mwakani.
Hoja za rais wa Urusi hazina msingi
Katika sera zake kuhusu Urusi Umoja wa Ulaya unataka kuendelea
na mkakati wa ncha mbili. Vikwazo vya kiuchumi viendelezwe wakati huo huo
lakini kila la kufanywa lifanywe kusaka ufumbuzi wa kisiasa wa mzozo wa
Mashariki ya Ukraine pamoja pia na kumezwa na Urusi rasi ya Crimea
ambayo ni sehemu ya ardhi ya Ukraine.
Kiongozi mmoja tu,rais wa Lithuania Dalia Grybauskaite ndie anaeunga
mkono msimamo mkali kuelekea Urusi.Hoja za rais Vladimir Putin kwamba
Umoja wa Ulaya unabeba jukumu la mzozo wa umwagaji damu wa Ukraine
imetajwa kuwa ni uwongo mtupu.Amezisuta pia hoja za Putin kwamba mgogoro
wa kiuchumi na kuporomoka thamani sarafu ya Urusi Rubel ni matokeo ya
vikwazo vya nchi za magharibi.
Mwakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa Ulaya bibi Federica
Mogherini ametahadharisha akisema "watu wasifurahikie mgogoro wa fedha
wa Urusi kwasababu hautaiathiri pekee Urusi, bali pia Ukraine, Ulaya na
sehemu iliyobakia ya dunia". Kuhusu maombi ya Ukraine kusaidiwa haraka kifedha, viongozi wa Umoja wa
Ulaya wamekaa kimya. Wanasisitiza misaada ziada ya fedha itatolewa
mageuzi ya kiuchumi na juhudi za kupambana na rushwa zitakapoanzishwa. Kimsingi rais Petro Poroschenko alipendelea kuhudhuria kama shahidi
mkutano huo wa kilele,lakini mwenyekiti wa baraza la Ulaya Donald
Tusk, hakumwalika.
Ufafanuzi zaidi unahitajika kuhusu mpango wa uwekezaji
Ama kuhusu mpango wa vitega uchimi ulioshauriwa na mwenyekiti
wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya, Jean Claude Juncker, viongozi wa
Umoja huo wametoa ridhaa ya kimsingi tu. Wanataka kupata maelezo zaidi
kuhusu mpango huo uliolengwa kuhimiza ukuaji wa kiuchumi. Mengi
yanahitaji kufafanuliwa kwa mfano vitega uchumi hivyo vitagharimia
miradi ya aina gani na nchi husika zitachangia vipi? Halmashauri kuu ya
Umoja wa Ulaya inapanga kuwasilisha ufafanuzi kuhusu miradi hiyo
mwishoni mwa mwezi wa Januari ili kupata ridhaa ya baraza la mawaziri na
baadae bunge la Umoja wa Ulaya.
CHANZO: DW KISWAHILI
No comments:
Post a Comment