Bunge
nchini Uganda limepitisha azimio ambalo linazuia usafirishwaji wa
mabinti na wanawake kwenda kufanya kazi nje ya nchi hiyo na azimio hili
limekuja baada ya kushuhudia vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji wa
jinsia hiyo kutoka kwa waajiri wao.
Marufuku hiyo inafuatia
waziri wa watu wazima na wale wenye ulemavu , Sulaiman Madada,ameeleza
kuwa serikali ya Uganda inatambua juu ya unyanyasaji huo na imepokea
malalamiko ya waathirika wa vitendo hivyo hasa Uarabuni kwa waganda
wanaofanya huko.
Hata hivyo ,ameongeza kuwa suala la ajira ni
muhimu mno wakati huu ili kuwapatia Waganda ajira,wakati huohuo serikali
ya Uganda ikiongeza nafasi za ajira kwa wajariramali wadogo na mpaka
sasa makampuni ishirini na manne yalipewa leseni ya kupeleka wafanyakazi
nje. Kufuatia hali hiyo,wabunge wameilaumu Serikali ya Uganda kwa
kushindwa kuwasaidia Waganda waliokata tamaa huko ughaibuni na kuwaacha
katika dhiki kuu wakiwa katika makampuni hayo waliyowapa leseni ambayo
yanaangalia faida wapatayo na sio majaaliwa ya waganda hao.
Malalamiko
mengi ya unyanyasaji wa kijinsia na kingono yamewafikia wanaharakati wa
haki za binadamu na kudai kwamba waganda wanalia kuingiliwa kwa nguvu
kinyume na maumbile na waajiri wao. Naye mbunge Medard Sseggona
ameeleza kuwa Waganda wengi wanataotafuta ajira nchi za kigeni wanasaini
mikataba wakiwa wamekata tamaa na kesi zao huwezi kuzipeleka
mahakamani.
Wabunge wawili Elijah Okupa na Sabiti waliibua hisia
za watu nchini humo baada ya kutoa ushuhuda wa binti mmoja ambaye
ametupwa jela na mwajiri wake mjini Kuwait ,ambaye ametoa wito kwa
wabunge na serikali kuingilia kati suala lake .
Msichan huyo kwa muujibu wa Okupa,anadai kuwa amegeuka kuwa mtumwa wa ngono kwa mwajiri wake.
Azimio
kama hilo lilikuwa mwaka 2009,dhidi ya kampuni ya Uganda Veterans Ltd
ambayo ilikuwa ikipeleka mabinti kutoka Uganda kwenda kufanya kazi Iraq
ama Marekani ambao waliishia kuteswa na familia za wa Iraq ambao
walikuwa wakikabiliana na manyanyaso makubwa bila mshahara.
Wasichana
hao mara wanapofika Ughaibuni hunyang’anywa pasi za kusafiria ,na
huamriwa kufanya kazi kinyume na makubaliano ya awali.Takwimu zinaonesha
kuwa waganda wpatao 42,015 waliondoka nchini humo kuelekea Mashariki ya
kati kwenda kutafuta ajira tangu mwaka 2006 na hawajaonekana tena
nchini mwao.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment