
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servaciaus Likwelile.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Sebastian Likwelile, alisema serikali itahakikisha fedha hizo zinazaa matunda kwa wakati.
“Kwanza niishukuru Benki ya Dunia kwa kutupa mkopo wenye riba ndogo
na ya muda mrefu kwa ajili ya kusaidia uboreshaji wa huduma za afya kwa
mama na mtoto kutokana na kundi hili kukabiliwa na changamoto nyingi,”
alisema Likwelile.
Aidha, alisema pamoja na kuwapo kwa mikakati mbalimbali ya
kupambana na changamoto hizo, bado kuna kazi kubwa kuhakikisha huduma za
afya zinaboreshwa ili kupunguza vifo ambavyo si vya lazima kwa
wajawazito na watoto wachanga.
"Serikali imekuwa ikipambana kupunguza tatizo hili na kufanikiwa
kwa kiwango kidogo kutokana na upungufu wa vifaa ambapo mwaka 2010
wajawazito 454 kati ya 100,000 walifariki dunia," alisema.
Aliongeza kuwa watoto 26 kati ya 1,000 wenye umri wa kati ya miaka
mitano, hufariki dunia kutokana na magonjwa mbalimbali na wengine
wakati wa kuzaliwa.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bernad Konga,
aliishukuru WB kwa mkopo huo na kusema kuwa utasaidia kwa kiwango
kikubwa kuimarisha huduma za afya.
"Tunaahidi kuwa fedha hizo zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa
ili kuhakikisha vifo vya watoto wachanga na wanawake wakati wa
kujifungua vinapungua," alisema Konga.
“Sekta ya afya inakabiliwa na changamoto nyingi lakini kwa kutumia
fedha hizi, tutahakikisha zinatatuliwa kwa kiwango kikubwa katika
kipindi cha miaka mitano ijayo,” alisema Konga.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment