Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Makongoro Nyerere akila kiapo cha kulitumikia bunge hilo mjini Arusha.
Historia yake
Makongoro Nyerere ni mtoto wa tatu wa Rais wa
kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kwa sasa ni
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala). Makongoro alizaliwa Januari 30, 1956 (Amefikisha miaka 59 Januari mwaka huu).
Alisoma katika shule za msingi Bunge na Isika zote za Arusha kati ya mwaka 1964–1972 na akajiunga na shule sekondari ya Wavulana Tabora alikohitimu kidato cha nne. Mwaka 1979 alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na alipelekwa mstari wa mbele kwenye vita ya Uganda, kikosi cha Mizinga na baada ya vita yeye ni mmoja wa askari waliobakizwa ili kulinda amani ya wananchi wa Uganda lakini pia kufundisha askari wapya raia wa Uganda kwa ajili ya mipango ya baadaye ya kuilinda nchi yao wao wenyewe.
Alisoma katika shule za msingi Bunge na Isika zote za Arusha kati ya mwaka 1964–1972 na akajiunga na shule sekondari ya Wavulana Tabora alikohitimu kidato cha nne. Mwaka 1979 alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na alipelekwa mstari wa mbele kwenye vita ya Uganda, kikosi cha Mizinga na baada ya vita yeye ni mmoja wa askari waliobakizwa ili kulinda amani ya wananchi wa Uganda lakini pia kufundisha askari wapya raia wa Uganda kwa ajili ya mipango ya baadaye ya kuilinda nchi yao wao wenyewe.
Aliporejea nchini kutoka vitani Uganda aliendelea
kutumia jeshi kwa muda mfupi kabla ya kupelekwa katika Chuo cha Mafunzo
ya Maofisa wa Jeshi (TMA), Monduli–Arusha na alishiriki na kufuzu
mafunzo ya Ofisa Kadeti na akawa Ofisa wa Jeshi la Tanzania rasmi hadi
alipostaafu rasmi mwaka 1990 akiwa na nyota mbili “Luteni”. Baada ya kujiunga na kushiriki katika siasa kwa
miaka mitano, aliamua kwenda nchini Scotland ambako alisoma Shahada ya
Masuala ya Mikakati katika Chuo Kikuu cha Aberdeen, hii ilikuwa mwaka
2001 – 2003.
Makongoro ameshika nyadhifa mbalimbali ndani ya
CCM na wadhifa mkubwa aliowahi kushika ni uenyekiti wa chama hicho
katika Mkoa wa Mara 2007–2012, lakini pia Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya
CCM, moja ya vikao muhimu ndani ya chama hicho.
Makongoro amemuoa Jaji Aisha Nyerere na wamepata
watoto watatu, wa kwanza anaitwa Julius Kambarage Nyerere, wa pili ni
Daudi Nyerere na wa tatu ni Prince Nyerere.
Mbio za ubunge
Mwaka 1995, Makongoro Nyerere aliwashangaza
Watanzania na hasa wanachama wa CCM baada ya kufanya uamuzi wa kukihama
chama hicho na kujiunga na chama kilichokuwa maarufu sana wakati huo,
NCCR Mageuzi.
Baada ya kujiunga NCCR, Makongoro alitangaza kuwa
anagombea ubunge katika jimbo la Arusha Mjini kupitia NCCR. CCM ilifanya
kila iwezalo lakini nguvu ya Makongoro ikawa kubwa, akapata asilimia
41.6 na kumshinda Felix Christopher Mrema wa CCM (Aliyewahi kuwa Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali) aliyenyakua asilimia 39.9, huku Mzee Edwin
Mtei (Waziri Mstaafu wa Fedha na kiongozi wa Chadema wakati huo)
akipata asilimia 13.5 ya kura zote.
Mbio za urais
Nguvu yake
Mwalimu Nyerere mwenyewe aliwahi kusikika akitoa ‘kijembe’
kuhusu familia yake kuwa “…familia yangu iko mstari wa mbele mabadiliko.
Nina wafuasi wa CCM, CUF na NCCR…” Nyerere alikuwa anasema hivyo kwa
sababu, Leticia Nyerere (mke wa kijana wa Nyerere) ni mtoto wa Mzee
Musobi Mageni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF (miaka ya
1990).
Felix Christopher Mrema wa CCM alikata rufaa
katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, akilalamikia ushindi wa Makongoro
Nyerere. Felix alisisitiza kwenye rufaa yake kuwa Msimamizi wa Uchaguzi
hakuhesabu kura za vituo kadhaa na pia kulikuwa na kura hewa zaidi ya
5,246.
Mahakama Kuu ilitupilia mbali maombi ya Felix,
lakini akakata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa ambayo ilijiridhisha kuwa
Makongoro alishinda isivyo halali. Ubunge wa Makongoro ukatenguliwa na
uchaguzi mdogo ukaitishwa lakini yeye (Makongoro) hakushiriki.
Aliamua kupumzika masuala ya siasa na kujiendeleza
kielimu. Alikwenda nchini Urusi na baadaye Uskochi na mwaka 2000
alijiunga tena CCM na baada ya mwaka 2003 akarejea nchini kutoka
masomoni ambapo Rais Mkapa alimteua kuwa Mbunge mwaka 2004 – 2005.
Makongoro alirejea tena katika siasa kwa nguvu
alipokuwa akisaka ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Hii ilikuwa mwaka
2012 na alichaguliwa kwa kura 123 na kuwa mbunge wa Bunge hilo hadi
muda wake utakapokamilika mwaka 2017.
Mbio za urais
Vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikimuuliza
Makongoro Nyerere kujua kama yumo kwenye kinyang’anyiro cha kuomba
ridhaa ya urais kupitia CCM, hakuwahi kukubali au kukataa na mara ya
mwisho amehojiwa na gazeti la kila siku linaloheshimika sana nchini
Tanzania, bado akawa hakubali au hakatai.
Lakini vyanzo vyangu ndani ya CCM na hata watu wa
karibu na Makongoro, wamenithibitishia kuwa milango ikishafunguliwa
atachukua fomu. Nimesisitizwa kuwa tayari Makongoro amekwishafunga
safari na kuonana na viongozi wengi wa juu waliowahi kuongoza nchi hii
wakiwemo marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu, majaji wakuu wastaafu
na wakuu wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Inaonekana Makongoro hataki kuanza kutajwatajwa
sana lakini ana mipango thabiti. Nilipomuuliza juu ya nia hii,
hakukubali wala kukataa kwa hiyo mimi nimehitimisha kuwa “yumo kwenye
mtanange”.
Nguvu yake
Makongoro ni mtu wa kujitolea sana, siyo kwa kutoa
fedha, lah! Kujitolea kufanya mambo ambayo yatawasaidia watu wengine na
hata taifa lake. Mwaka 1979 alijiunga jeshini kama mmoja wa vijana
waliohitaji kulinda taifa lao dhidi ya nduli Idd Amin. Tunajua kuwa
watoto wengi tu wa vigogo wakati huo walikwepa wajibu huo, Makongoro
hakuwa mmoja wao.
Lakini Makongoro anapewa nguvu na mtazamo wa jamii
kumhusu. Anatazamwa kama mtu wa kawaida tu. Hakuwahi kuthubutu
kujijengea tabia za “Unyerere” kwa maana ya taswira ya baba yake. Ni mtu
ambaye ukikaa naye chini siku nzima, kama hujaambiwa na mtu wa jirani
kuwa huyu ni kijana wa Baba wa Taifa, hutaweza kugundua. Anaishi maisha
ya Utanzania zaidi kuliko ya “kuwa mtoto wa Rais wa Kwanza wa Taifa
hili”. Leo hii tunashuhudia watoto wangapi wa marais wetu ambao hawawezi
kupanda “bajaji au daladala”? Makongoro hachagui nini avae, nini ale na
nini apande. Watu wake wa karibu wananiambia kuwa amefaulu kabisa
kujijenga yeye kama yeye na si yeye kama mtoto wa Nyerere.
Udhaifu wake
Nini kinaweza kumfanya apitishwe?
Uthubutu ni nguvu ya tatu ya Makongoro. Kiongozi yeyote yule
anayejiandaa kuongoza dola lazima awe na uwezo wa kuthubutu kufanya
mambo fulani fulani ili kujenga mustakabali mwema mbele ya safari. Mwaka
1995 alipohamia NCCR huku baba yake akiwa ni muasisi wa mwanzo wa Tanu
na CCM, wengi walimshangaa sana lakini hakutishwa na kivuli cha
“mishangao” hiyo, alipigana na kushinda ubunge Arusha bila kusaidiwa na
kivuli cha baba yake? Watoto wangapi wa marais wengine wanaweza
kuthubutu kuhamia upinzani na wakagombea na kuishinda nguvu kubwa ya
dola za wazazi wao?
Lakini jambo la mwisho kwa hapa ni kufahamika.
Makongoro Nyerere ni mtoto wa Nyerere anayefahamika, kutajwa na
kuonekana sana kuliko watoto wengine wote. Walau kwa kizazi cha Mwalimu
Nyerere, unaweza kusema kuwa Makongoro ndiye amewapita wenzake wote
katika ushiriki wa juu wa masuala ya siasa na hata uongozi ndani ya CCM.
Kufahamika ni karata muhimu kwake katika mbio hizi.
Udhaifu wake
Udhaifu mkubwa wa Makongoro ni “kufanya maamuzi ya
haraka”. Watu wa karibu yake, waliofanya kazi naye bungeni na
kwingineko wanasema yeye ni mtu wa kufanya maamuzi na si kulaza viporo.
Mbunge mmoja wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania alinidokeza
kuwa yeye hutaka mambo yajadiliwe na kumalizwa na hapendi hata kidogo
kulaza masuala ambayo yalihitaji kukamilishwa kwa wakati.
Pamoja na kuwa nchi inahitaji kiongozi anayefanya
maamuzi haraka lakini yanapaswa kuwa maamuzi makini. Hadi sasa sijapata
ushahidi wa maamuzi yapi Makongoro aliwahi kuyasimamia kwa haraka lakini
yakawa na tija kubwa.
Udhaifu mwingine mkubwa wa Makongoro ni kutokuwa
na visheni ya kudumu katika siasa. Makongoro tofauti na wanasiasa wengi
wa Afrika anachukulia siasa kama suala la wakati na kipindi fulani.
Ndiyo maana alipoenguliwa katika nafasi ya ubunge mwaka 1997 pale
Arusha, akaamua kutogombea tena akarudi kusoma na baadaye kati ya mwaka
2005–2012 hakugombea nyadhifa zingine za kiuwakilishi kabla ya Eala.
Tabia hii ya kugombea miaka kadhaa na kuacha na
tena kurudi baada ya miaka mingine imemfanya Makongoro asijijengee
uhakika wa kisiasa na imemnyima fursa ya kusimamia masuala makubwa
ambayo leo angewaonyesha Watanzania kuwa aliwahi kutulia mahali fulani
na akasimamia masuala hayo. Watu wake wa karibu pia, wameutaja huu kama
udhaifu mkubwa.
Nini kinaweza kumfanya apitishwe?
Mambo kama matano hivi yanaweza kumfanya Makongoro avuke mchujo na kuwa mgombea wa CCM:
Jambo la kwanza ni historia yake ya kulitumikia
taifa jeshini hadi alipoamua kustaafu mwenyewe lakini pia uzoefu wake
ndani ya uongozi na katika kusimamia masuala ya kikanda (Afrika
Mshariki). Makongoro ni mmoja wa wabunge wa kutegemewa katika Bunge la
Afrika Mashariki akiisaidia Tanzania na ana bahati ya kukubalika hata
kwa viongozi wa nchi jirani kama Kenya na Uganda.
Kama CCM itamvusha Makongoro, pia ni kwa sababu ya
maadili. Yeye ni mtu mwenye msimamo na kusimamia maadili. Ndiyo maana
wakati wa vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM ni Makongoro ndiye alisimama
kidete na kuwanyooshea vidole makada kadhaa ambao walikuwa wanatuhumiwa
kukipatia chama hicho taswira mbaya. Makada hao ni watu wenye uwezo
mkubwa wa kifedha na wanaogopwa hasa ndani ya CCM, lakini Makongoro
alichukua msimamo mzito mno. CCM ya sasa inaweza kuhitaji mgombea wa
namna hii ili kuinusuru na kuirudishia heshima.
Jambo la tatu linaloweza kumvusha ni kuifahamu
vizuri CCM ikiwa ni pamoja na kutoharibu taswira ya baba yake. Nyerere
alichukia rushwa na Makongoro anachukia sana rushwa. Nilipomuuliza jambo
gani analolichukia kwenye ukurasa wake wa facebook, alinijibu kuwa la
kwanza ni rushwa, nilipomuuliza la pili alisisitiza “rushwa” na la tatu…
rushwa. Kwa sababu anakifahamu vizuri chama chake na ameweza kubeba
taswira ya baba yake, huenda akawa mwarobaini ndani ya CCM na hivyo
akavushwa.
Nini kinaweza kumwangusha?
Asipopitishwa (mpango B)
Jambo la nne linaloweza kumvusha Makongoro ni dhana ya kuua
nguvu ya makundi yanayoshindana na yaliyojipanga muda mrefu sana. Kama
CCM itahofia kuparaganyika vibaya na inahitaji kurejea kwenye heshima.
Makongoro anaweza kuwa mtu muhimu wa kubeba dhamana hiyo na labda
kukiacha chama hicho salama.
Gazeti moja la kila siku la Kiingereza, limewahi
kuandika kuwa:“Marketing Mr Makongoro is every easy because of the
enduring legacy his father left behind to ordinary Tanzanians as well as
the elite, many would empathise with him during the election.” (Tafsiri
yangu – “Kumuuza Makongoro ni rahisi sana kwa sababu ya heshima ambayo
baba yake aliiacha kwa Watanzania wa kawaida pamoja na watu wa kati,
watu wengi wataungana naye kwenye uchaguzi”). Hakika, kama CCM inahitaji
mtu anayeuzika katika uchaguzi wa mwaka huu, huenda Makongoro ni mmoja
wa mtu wa aina hiyo.
Nini kinaweza kumwangusha?
Mambo matatu makubwa yanaweza kumwangusha Makongoro:
La kwanza ni makundi yenye fedha na yaliyojipanga
kunyakua urais kupitia CCM, na yameshafanya hivyo kwa kipindi kirefu
sana na hivyo kuingia kwake katika hesabu kunaweza kuyafanya makundi
hayo yatumie kila mbinu kummaliza kisiasa kwanza ili wakosekane watu
mbadala wa kufikiriwa na chama hicho.
Jambo la pili ni uamuzi wake wa kuhama CCM mwaka
1995 na baadaye kurejea mwaka 2000. Chama hicho kinaweza kuwa bado kina
hofu na tabia yake ya kufanya maamuzi ya namna hiyo na kwa sababu katika
rekodi za marais waliotokana na CCM na kuongoza Tanzania, hakuna mmoja
wao ambaye aliwahi kuhamia upinzani kisha akarejea CCM, huenda “zengwe”
hili likatumika kummaliza.
Jambo la mwisho ni kukosa ufuasi mkubwa sana ndani
ya CCM. Kama CCM itataka kumpitisha mgombea urais wake kwa kutazama
nani ana wafuasi wengi ndani ya chama hicho kwa sasa, huenda Makongoro
asiwe chaguo. Makongoro hana ufuasi mkubwa ndani ya CCM kwa sababu
ufuasi ndani ya chama hicho unajengwa sana na nguvu ya fedha na
mitandao, mambo ambayo yeye aliniambia kuwa hawezi kujihusisha nayo.
Asipopitishwa (mpango B)
Namuona Makongoro akijielekeza katika mipango
miwili na kufanikiwa, iwapo hatapitishwa kugombea urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Mpango wa kwanza ni kuendelea kutumikia ubunge
wake wa Bunge la Afrika Mashariki na kisha atakapomaliza kipindi cha
kwanza aombe kingine na kuendelea kuwakilisha huko.
Mpango wa pili ni kujipanga na kugombea ubunge wa jimbo la Musoma Vijijini.
Mpango wa mwisho unaweza kuwa Kuendeleza kazi za
Baba wa Taifa katika maeneo ya haki, umoja na amani. Ikumbukwe kuwa
pamoja na taifa hili kupata mchango mkubwa kwa wazee wengi akiwamo
Mwalimu Nyerere, historia na kazi za wazee hao hazijatangazwa kitaifa na
kimataifa. Huenda Makongoro akaamua kuachana na siasa na kuanza
kutangaza juhudi za watu waliopigania taifa hili akiwamo baba yake huku
akihamasisha mshikamano katika taifa, umoja, haki na udugu.
Hitimisho
Hitimisho
Kujitokeza kwa Makongoro Nyerere katika kusaka
urais wa Tanzania kupitia CCM kuna maana kubwa sana, lakini ni kitisho
kikubwa kwa kambi zilizojipanga muda mrefu uliopita. Nchi nyingi duniani
pia zinaongozwa na vijana ambao wazazi wao walikuwa viongozi wakuu wa
mataifa hayo. Mimi huwa sielewi maana ya falsafa hiyo na nilipofuatilia
katika nchi zingine nimegundua kuwa vijana wa marais wanapoanza safari
ya kutaka ukuu, watu wengi huwachukulia kama wanafanya masihara lakini
mwisho wa siku huwa viongozi. Na kwa namna CCM ilivyozidiwa na mpasuko,
nina uhakika kuwa watu kama Makongoro Nyerere wana turufu muhimu sana
mkononi. Namtakia ndugu huyu ‘kama alivyoomba nimuite’ kila la heri
katika nia hii ya urais.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment