
Maofisa wa ngazi za juu wa Burundi wamekamatwa kwa tuhuma za kupanga njama za kumpindua Rais Pierre Nkurunziza.
Wakati jaribio la kumng’oa mpiganaji huyo wa
zamani wa msituni likiwa limeshindikana, wananchi wamerejea mitaani
kuandamana ikiwa ni ishara ya kupinga mpango wake wa kugombeas urais kwa
kipindi cha tatu kinyume na katiba.
Msemaji wa Rais, Gervais Abayeho alisema jana
kwamba majenerali watatu wa jeshi na wawili wa polisi walikamatwa jana.
Pia maofisa watatu wa ngazi za chini na askari wanane, walikamatwa.
Jaribio la kumpindua kiongozi huyo lilifanywa wakati akiwa Tanzania
kuhudhuria mkutano wa amani uliopanga kujadili machafuko ya Burundi
yaliyotokana na wananchi kupinga mpango wa Nkuruzinza kutaka kugombea
tena urais.
Watu warudi mitaani
Hali jijini Bujumbura ambayo ilitulia juzi, jana
ilianza tena kuharibika baada ya zaidi ya waandamanaji 30 kuandamana
kushinikiza rais huyo afute mpango wake wa kugombea tena urais. “Tutaendeleza maandamano kupinga mpango wa Rais
kujiongezea muda wa kutawala. Unaona wanataka kutuzuia, lakini sisi
tunasema hatutaacha kuandamana.
Tunataka katiba iheshimiwe,” alisema mmoja wa waandamanaji, Jean Paul Ndayiragije.
Tunataka katiba iheshimiwe,” alisema mmoja wa waandamanaji, Jean Paul Ndayiragije.
Viongozi wa upinzani na vyombo vyua habari vya
binafsi, vina wasiwasi na serikali ya Nkurunziza hasa baada ya jaribio
las mapinduzi kukwama. Tume ya Uchaguzi Burundi imesema itapitia upya
taratibu za uchaguzi ambao Rais Nkurunziza alisema kuwa ataheshimu
matokeo yoyote.
Waiombea vikwazo
Raia wa Burundi wanaoishi Uingereza wamemuomba
Waziri Mkuu David Cameron kusimamisha misaada ya kifedha kutokana na
msimamo wa Rais Nkurunziza kuwania urais muhula wa tatu.
Raia hao walisema uamuzi wa Nkurunziza ni kinyume cha Katiba ya nchi hiyo. Watu hao waliandamana jana jijini London wakipinga
Rais Nkurunziza kukiuka katiba, makubaliano ya Arusha na mauaji ya raia
22 wa nchi hiyo yaliyosababishwa na maadamano ya wiki mbili zilizopita.
Waandamanaji hao walikuwa wamebeba bendera ya nchi
hiyo, huku wakitaka serikali kulinda amani na kumtaka Nkurunziza aache
kugombea urais muhula wa tatu.
Barua kwa David Cameron
Waandamanaji hao waliwasilisha barua Ikulu ya Uingereza iliyoko Mtaa wa 10 Downing wakitaka nchi yao kuwekewa vikwazo. Kwa mujibu wa Muungano wa Ulaya (EU), Burundi
imekuwa ikipewa msaada wa Dola 6 hadi 9milioni za Marekani kwa ajili ya
kusaidia shughuli za Uchaguzi Mkuu.
Kutokana na vurugu zinazoendelea nchini humo,
waandamanaji jijini London walisema ushiriki wa Uingereza katika
uchaguzi huo kwa namna moja au nyingine ni kinyume cha sheria za
uchaguzi.
Mmoja wa waandamanaji hao nchini Uingereza
alisema: “Kama Uingereza imekuwa ikizungumzia demokrasia na utawala
bora, tunawaomba watende haki. Uingereza wanapaswa kuchukua uamuzi
mgumu.
“Hakuna haja kwa Uingereza kutoa fedha kwa ajili
ya kusaidia uchaguzi Juni 26, mwaka huu katika nchi ambayo haina utawala
bora. Asilimia 50 ya bajeti ya nchi hiyo inategemea nchi za Magharibi
hivyo hakuna haja ya kuisaidia Burundi.
Mwanaharakati alonga
Mwanaharakati wa vuguvugu la maandamano ambaye pia
ni mwenyekiti wa chama cha UPD –Zigamibanga cha Burundi, Mugwengezo
Chauvineau ametaja sababu za maandamano nchini humo kuwa ni Rais
Nkurunzinza kushindwa kuweka uwiano baina ya Warundi sambamba na
kutekeleza haki za binadamu.
Alisema waandamanaji wamekuwa kiungo, njia, nguzo na sababu ya rais aliyepo madarakani kutaka kupinduliwa.
Akizungumza katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam, Chauvineau alisema kwa mtazamo wa wananchi wa Burundi kitendo
cha Rais Nkurunzinza kuendelea kukaa madarakani, kimewafanya wengi wawe
tayari hata kunywa sumu, ili kutoweka kinyume na kuishi katika utawala
butu.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment