Jenerali Niyungeko Juvenal (katikati) akipelekwa katika Mahakama Kuu
mjini Bujumbura kujibu shtaka la kujaribu kumpindua Rais Pierre
Nkurunziza.
Maofisa 17
wa Jeshi la Burundi wametiwa mbaroni wakiwamo majenerali watano na
kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuipindua Serikali ya Rais Pierre
Nkurunziza. Wanajeshi watatu wametajwa kuwa vinara wa kupanga
njama za kuipindua Serikali ya Burundi wakiwamo maofisa wawili wa ngazi
za juu wa polisi.
Msemaji wa Ikulu ya Burundi, Gervais Abayeho
alisema jana kwamba washtakiwa wengine wanne ni maofisa wenye vyeo vya
chini na wanane ni wanajeshi wa kawaida. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya kukamatwa kwa Meja Jenerali Godefroid Niyombare ambaye aliongoza mapinduzi hayo.
Askaribi hao wanatuhumiwa kufanya jaribio la
kumpindua Rais Nkurunziza wakipinga uamuzi wake wa kugombea urais kwa
muhula wa tatu.
Abayeho alisema wakati maandamano yakiendelea
Bujumbura kupinga uamuzi wa Chama cha CNDD-FDD kumteua Nkurunziza
kugombea nafasi hiyo kwa mara nyingine, Meja Jenerali Niyombare
alitangaza kutomtambua Nkurunziza kama rais wa nchi hiyo. Mawakili
wanaowatetea watuhumiwa hao walisema kwamba baada ya wateja wao
kukamatwa waliteswa na kuumizwa.
“Wamepigwa na ukiwatazama wamechoka na hawana mashati wala viatu,” alisema mmoja wa mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao kutoka Kampuni ya Mawakili ya Bar, Miburo Anatole.
“Wamepigwa na ukiwatazama wamechoka na hawana mashati wala viatu,” alisema mmoja wa mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao kutoka Kampuni ya Mawakili ya Bar, Miburo Anatole.
Anatole alisema anamwakilisha Meja Jenerali
Cyrille Ndayirukiye ambaye alikuwa waziri wa zamani wa ulinzi wa nchi
hiyo na maofisa wawili wa polisi. Wakili mwingine, Cyriaque Nibitegeka alisema mteja
wake ambaye ni ofisa wa jeshi la nchi hiyo alilazimishwa kwa mtutu wa
bunduki kukiri kwamba alihusika kuipindua nchi hiyo. Alisema mteja huyo
amegoma kula tangu walipokamatwa wiki iliyopita.
Taarifa zilieleza kwamba endapo watuhumiwa hao watapatikana na hatia watahukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani. Ijumaa iliyopita, Nkurunziza alirejea mjini Bujumbura akitokea Tanzania, huku maandamano ya kumpinga yakiendelea.
Licha ya Serikali kuzuia kufanyika kwa maandamano,
waandamanaji vikiwamo vyama vya upinzani na wananchi wameapa kuendelea
hadi Rais Nkurunziza atakapotangaza kuacha mpango wake wa kugombea tena
urais. “Tutaendelea kufanya maandamano kwa kuwa malengo yetu ni kumtaka
Nkurunziza aache kugombea urais muhula wa tatu. Tunaona wanajaribu
kuzuia maandamano yetu, lakini sisi hatutasitisha maandamano.
Tutaendelea kuipigania katiba ili iheshimike,” alisema Jean Paul
Ndayiragije.
Idadi ya wakimbizi
Nkurunziza hadharani
Uchaguzi mkuu nchini humo unatarajiwa kufanyika Juni 26, mwaka huu.
Jaribio la kumpindua Rais Nkurunziza lilitekelezwa
na Meja Jenerali Niyombare na maofisa wenzake wa jeshi wakati
Nkurunziza akiwa nchini Tanzania kuhudhuria mkutano wa dharura kuhusu
mgogoro unaendelea nchini humo, lakini mapinduzi hayo yalizimwa na
maofisa wa jeshi wanaomtii.
Idadi ya wakimbizi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Tanzania,
Isaac Nantanga alisema Serikali imetoa ushirikiano mzuri katika shughuli
ya kuwapokea wakimbizi wanaotoka Burundi. Zaidi ya watu 105,000 wameikimbia Burundi, 70,000
wameingia Tanzania na 26, 300 wamekimbilia Rwanda tangu kuanza kwa
vurugu nchini humo. Wakimbizi wengi wanaishi katika Kambi ya Mahama.
“Taarifa zinaeleza kwamba watu 10,000 wako mpakani
mwa Tanzania na Burundi wakisubri kuingia katika kambi ya wakimbizi
mkoani Kigoma,” lilisema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR).
Nkurunziza hadharani
Kwa mara ya kwanza, Rais Nkurunziza alionekana
hadharani jana, huku akiwa amevaa kaunda suti ya bluu. Alionekana
akitabasamu, huku akiwasalimia waandishi wa habari na kuzungumza masuala
ya ugaidi bila kugusia jaribio la kuipindua serikali yake.
Rais Nkurunziza alizungumzia tishio la ugaidi
ambalo limetolewa na kundi la Al-Qaeda ambalo lina uhusiano na
wanamgambo wa Al- Shabaab. “Tumechukua tahadhari dhidi kundi la Al-Shabaab,
tishio hili tumelichukua kwa umakini mkubwa kwa ajili ya usalama wa raia
wetu,” alisema Rais Nkurunziza.
Burundi na nchi nyingine za Afrika zimepeleka majeshi ya kulinda amani nchini Somalia.
Katika tukio jingine, Raia wa Burundi wanaoishi Uingereza wamemuomba Waziri Mkuu wa nchi hiyo, David Cameron kusimamisha misaada ya kifedha kutokana na msimamo wa Rais Nkurunziza. Raia hao walisema uamuzi wa Rais Nkurunziza ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.
Katika tukio jingine, Raia wa Burundi wanaoishi Uingereza wamemuomba Waziri Mkuu wa nchi hiyo, David Cameron kusimamisha misaada ya kifedha kutokana na msimamo wa Rais Nkurunziza. Raia hao walisema uamuzi wa Rais Nkurunziza ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.
Watu hao waliandamana juzi jijini London wakipinga
Rais Nkurunziza kukiuka katiba na watu 22 waliouawa kwenye maadamano
mjini Bujumbura. Waandamanaji hao walikuwa wamebeba bendera ya nchi
hiyo, huku wakitaka Serikali kulinda amani na kumtaka Nkurunziza aache
kugombea urais muhula wa tatu.
Kwa mujibu wa Muungano wa Ulaya (EU), Burundi
imekuwa ikipewa msaada wa Dola 6 milioni mpaka 9 za Marekani kwa ajili
ya kusaidia shughuli za uchaguzi mkuu kila unapowadia.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment