William Ngeleja, Mbunge wa Sengerema alisoma katika Shule ya Msingi Bitoto mwaka
1976 – 1982 kabla ya kuelekea mkoani Dodoma kwa masomo ya kidato cha
kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Mpwapwa kati ya mwaka
1983 –1986. Baada ya kufaulu vizuri aliendelea na masomo ya kidato cha
tano na sita katika Shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera kati ya
mwaka 1987 – 1989.
Historia yake
William Mganga Ngeleja alizaliwa Oktoba 5, 1967 mkoani Mwanza hivyo atafikisha miaka 48 mwezi Oktoba mwaka huu.
Ngeleja alisoma katika Shule ya Msingi Bitoto
mwaka 1976 – 1982 kabla ya kuelekea mkoani Dodoma kwa masomo ya kidato
cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Mpwapwa kati ya mwaka
1983 –1986. Baada ya kufaulu vizuri aliendelea na masomo ya kidato cha
tano na sita katika Shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera kati ya
mwaka 1987 – 1989. Ngeleja alifaulu vizuri masomo yake na akajiunga moja
kwa moja Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) sehemu ya Mlimani
akichukua kozi ya sheria mwaka 1991. Alihitimu na kutunukiwa shahada ya
kwanza ya sheria (LLB) mwaka 1994 na kuajiriwa serikalini kama
Mwanasheria wa Serikali mwaka 1994–1996. Ngeleja aliamua kujiendeleza
zaidi, akarejea UDSM mwaka 1996 kusomea shahada ya uzamili ya sheria
(LLM) na kuhitimu mwaka 1999.
Kati ya mwaka 1995 hadi 2000 Ngeleja pia alifanya
kazi na kampuni maarufu ya uwakili duniani ya Price WaterHouse Coopers,
ambayo ina matawi mengi ulimwenguni ikiwamo Tanzania.
Mwaka 2000 aliacha kazi Price WaterHouse Coopers
na kujiunga na kampuni ya Vodacom ambako alifanya kazi kama mwanasheria
wa kampuni, kwa miaka mitano, hadi 2005. Katika kipindi chote hiki
Ngeleja aliendelea na kazi huku akikisaidia chama chake, CCM, katika
masuala mbalimbali na wakati huohuo akifikiria kuingia katika siasa za
ushindani.
Mbio za ubunge
Safari ya kuusaka ubunge aliianza mwaka 2005
alipojitosa kuomba ridhaa ya ubunge katika Jimbo la Sengerema; akapita
mchujo wa kura za maoni na kuwa mgombea wa CCM. Kwenye uchaguzi alikumbana na Essau Balalukuliliza
Pelece wa UDP, Stella Cosmas Chetto wa CUF na Joshua Zebrone Subi wa
Chadema akawashinda kwa kupata asilimia 69.3 ya kura zote. Baada ya kuwa
mbunge alitumikia nafasi hiyo, kwa mwaka mmoja, kabla ya kuongezewa
wadhifa wa unaibu waziri katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kwenye
wizara ya Nishati na Madini kutokea Januari 2007 hadi Agosti 2008.
Mwaka 2008 kulipofanyika mabadiliko katika Baraza
la Mawaziri, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Ngoyayi Lowassa
kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond, Rais Kikwete aliunda Baraza la
Mawaziri jipya na kukuza “ngekewa” ya Ngeleja ambaye alipewa uwaziri
kamili wa Nishati na Madini kukamilisha miaka miwili iliyokuwa imebakia
kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwkaa 2010.
Mwaka 2010 Ngeleja alijitosa tena kwenye
kinyang’anyiro cha ubunge kutetea nafasi yake; alishinda kura za maoni
na kwenye uchaguzi wenyewe akawa hana mpinzani, yaani wagombea wa
upinzani waliingia “mitini” na kumpa “zawadi ya ushindi”.
Baada ya kupita bila kupingwa aliteuliwa kuwa
Waziri wa Nishati na Madini, nafasi aliyoitumikia hadi Juni 2012 mwaka
ambao Rais Kikwete alifanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri
na kumtupa nje Ngeleja. Nafasi yake ilichukuliwa na Profesa Sospeter
Muhongo.
Pamoja na kuwa nje ya uwaziri, safari yake kisiasa
iliendelea kukumbwa na mawimbi mengi. Mwanzoni mwa mwaka huu,
alilazimika kuachia ngazi katika nafasi ya uenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kutokana na kuwa miongoni mwa
viongozi waliopokea mgawo wa fedha zilizochukuliwa kutoka kwenye akaunti
ya Tegeta Escrow.
Mbio za urais
Nguvu zake
Alipoitwa kujieleza kwenye Tume ya Maadili, Ngeleja alikiri
kuwekewa shilingi 40.4milioni na mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering
& Marketing, James Rugemalira lakini mwenyewe alisisitiza kuwa fedha
hizo hazikuwekwa kwa nia mbaya. Na kibaya zaidi yeye mwenyewe hakutoa
taarifa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Mbio za urais
Ngeleja ni mmoja wa watu waliotajwa sana kama watu
wanaomuunga mkono Lowassa katika safari ya kuisaka Ikulu tangu
alipokuwa Waziri Mkuu chini ya Rais Kikwete na hata baada ya kujiuzulu
nafasi hiyo mwaka 2008.
Na hata Ngeleja alipoteuliwa tena kuwa Waziri wa
Nishati na Madini, mara baada ya kuteuliwa kwa mara ya pili Januari
2011, ilisemekana kuwa anamuunga mkono waziri mkuu huyo aliyejiuzulu.
Lakini katikati ya mwaka 2013, inasemekana wanamtandao wa urais katika
kundi la Lowassa wanaotokea Kanda ya Ziwa, waliona vema kumuibua mgombea
anayeweza kuungwa mkono kutoka kanda yao na ndipo akainuliwa Ngeleja.
Katika harakati za chini kwa chini akawa miongoni
mwa makada sita walionaswa na chama wakifanya kampeni za siri na
wakazuiwa kwa miezi 12 kuanzia Februari mwaka jana. Kamati ya Maadili
inaendelea kuwachunguza.
Hata harakati zake za kuwapigania wachimbaji
wadogowadogo wapate maeneo zaidi kwa ajili ya uchimbaji, kuwaanzishia
mfuko maalum wa kuwasaidia, kupiga marufuku usafirishaji wa madini ghafi
kwenda nje ya nchi, na hatua kama hizo, zilikuwa zinahusishwa na mbio
hizo hasa kwa kuzingatia kuwa maeneo yenye madini yana wapigakura wengi
sana. Hata hivyo, jambo hilo halijathibitishwa.
Watu walio karibu naye, miongoni mwao wakiwa
wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, wanasema kwamba yeye huwa anajinasibu
kuwa anaweza kuwa chaguo mbadala makada maarufu watakapokatwa majina
yao.
Nguvu zake
Ngeleja amewahi kuwa karibu sana na Lowassa, na
hadi leo. Kwa hiyo, anaujua vizuri mtandao wa ushindi ndani ya CCM hasa
kwa sababu alishiriki pia shughuli kama hiyo wakati wa kumpigania
Kikwete mwaka 2005. Jambo hili linampa nguvu kubwa.
Nguvu nyingine ya Ngeleja inatokana na umri wake,
kwani anaonekana bado kijana sana. Ikiwa CCM itahitaji kupitisha mgombea
mwenye umri wa “usasa” na ambaye ana kaliba inayoweza kuwavutia vijana
na watu wengine, Ngeleja atakuwa miongoni mwa watu wenye sifa hiyo.
Tukija katika uzoefu, eneo hili pia linampa
Ngeleja nguvu kubwa. Tangu mwaka 1994 Ngeleja ameweza kutumika
serikalini na katika mashirika binafsi na ya kimataifa kama mwanasheria.
Uzoefu huo una maana kuwa anaifahamu vizuri nchi na mazingira ya kazi
katika sekta ya umma na sekta binafsi. Hakika kigezo hiki kinampa nguvu
ya kipekee tofauti na wagombea wengine ambao labda wamewahi kufanya kazi
serikalini tu.
Nguvu nyingine ya Ngeleja inapatikana kwenye
taaluma yake. Sheria ni taaluma ya “kipekee” na ina tofauti kubwa sana
na masomo ya sanaa. Mara nyingi viongozi wanasheria wanatarajiwa
kujiamini na kutenda masuala ambayo yanaweza kutohojiwa kirahisi. Ikiwa
itachukuliwa kwa mtazamo huo na kwamba CCM inahitaji msomi mzuri mwenye
taaluma ya kipekee na inayoweza kumfanya mtu afanye kazi katika
mazingira yoyote kwenye sekta nyingine, basi Ngeleja atakuwa miongoni
mwa wanaofuzu.
Udhaifu wake
Nini kinaweza kumfanya apitishwe?
Nini kinaweza kumwangusha?
Hitimisho
Naona kama Ngeleja atakuwa na wakati mgumu kupita kwenye mchujo wa wagombea urais ndani ya CCM na ni kama vile jina lake linaweza kukatwa mapema ili kuwapisha wana CCM wengine wenye sifa zaidi waweze kuchukua jukumu hilo la kidemokrasia. Lakini pia hatujui chama hicho kitatumia mfumo gani na sifa zipi kumpata mgombea wake. Kwa lolote lile litakalojiri, naye tunamtakia kila la heri kwenye malengo yake.
CHANZO: MWANANCHI
Udhaifu wake
Udhaifu mkubwa wa Ngeleja ni kuwa karibu na
wanasiasa wanaotajwa vibaya na wenye taswira hasi katika jamii. Kama
nilivyowahi kueleza katika maandiko yangu mengine, CCM safari hii,
itahitaji kuwa na mgombea ambaye ana rekodi sahihi na mwenye nguvu ya
kutosha kukisaidia chama chake kishinde uchaguzi kirahisi na siyo mtu
ambaye atakuwa mzigo au kusafishwa kwa “dodoki”. Kwa dhana hii Ngeleja
anaweza kuonekana kuwa mmoja wa “mizigo” inayopigwa vita.
Udhaifu mwingine wa Ngeleja upo kwenye utendaji.
Ngeleja amekuwa Waziri wa Nishati na Madini kwa takribani miaka sita,
lakini ameondoka katika wadhifa huo nchi ikiwa na changamoto kubwa sana
za kiusimamizi na kimiundombinu. Jambo moja linaweza kuhitimishwa katika
hali kama hiyo, kwamba siyo mtendaji mzuri. Pamoja na baadhi ya mazuri aliyofanya Ngeleja, lakini aliiacha wizara ikiwa na matatizo mengi kama mtangulizi wake.
Na mfano mwingine ni namna alivyokuwa
akishughulikia ukosefu wa nishati ya umeme. Mwanzoni mwa Desemba 2010
Ngeleja aliwatangazia Watanzania kuwa “mgawo wa umeme sasa basi”. Lakini
wiki tatu baadaye, hata kabla mwezi huo haujaisha, Tanesco ikatangaza
mgawo wa umeme mkali kuliko uliowahi kutokea nyuma yake. Udhaifu huu
kiusimamizi na kimamlaka hautapita hivi hivi bila kujadiliwa.
Ndani ya Bunge kwenyewe, alilalamikiwa sana
kutokana na utendaji wake mbovu katika sekta ya Nishati na Madini. Mwaka
2011 matatizo yale yale ya mgawo wa umeme yaliendelea kujitokeza hadi
aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January
Makamba alimshutumu Ngeleja kuwa amekuwa mtu wa kukimbia, kujificha na
kutosema ukweli kuhusu tatizo la umeme nchini.
Ngeleja alitupiwa shutuma kwa sababu kauli ya
Serikali aliyoitoa bungeni juu ya hali ya umeme nchini ikiwemo
kukodishwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 260 ifikapo Juni
na Julai mwaka huo wa 2011 haikuwa imetekelezwa huku Waziri akiwa kimya.
CCM katika baadhi ya matamko yake kwenye mikutano ya hadhara
ilisisitiza pia kuwa “kitendo cha Waziri Ngeleja kukimbia na kujificha,
kinaonyesha kuna ombwe la uongozi ndani ya Wizara ya Nishati na Madini”.
Chama kiliungana na Kamati ya Makamba na kumsisitiza ambane Ngeleja ili
aeleze utekelezaji wa mipango yote aliyoiainisha kwenye ahadi za
serikali vinginevyo aachie ngazi.
Nini kinaweza kumfanya apitishwe?
Kama kuna jambo litaweza kumbeba Ngeleja basi ni
elimu na uzoefu wake. Kama nilivyoeleza hapo awali Ngeleja ana elimu
nzuri na ana uzoefu mzuri wa kufanya kazi na sekta binafsi na ya umma na
anaifahamu nchi hii vizuri. Kama CCM ikiamua kumpitisha basi hii
itakuwa sababu mojawapo.
Lakini pia, Ngeleja ni mtu wa kuthubutu. Pamoja na
mapungufu yake yote, anaweza kusimamia jambo fulani na likaonekana
japokuwa anaweza kuonekana kama amelifanya kwa kiwango cha chini
utakapomlinganisha na watu wengine wenye uwezo kumshinda. Nilitoa mfano
wa kusimamia masuala ya vitalu vya wachimbaji wadogowadogo na kuanzisha
mfuko wao. Haya ni mambo ambayo wamekuwa wakiyalalamikia muda mrefu
lakini hayakufanikishwa hadi alipoingia Ngeleja japo hadi sasa hayajawa
na tija. Hata hivyo, walau unaweza kusema yeye ni mtu wa kuthubutu.
Na pia, ikiwa CCM itataka kumpitisha mgombea ili
kuyafurahisha makundi yanayosigana, yeye anaweza kuwa chaguo. Kwamba
yale makundi makubwa na wakuu wao, itakapoonekana hawastahili basi
atafutwe mtu ambaye anaweza kuwa anaungwa mkono na kundi lolote na
ambaye akiteuliwa makundi yote yanaweza kumkubali kwa sababu si mkuu wa
kundi fulani, atakuwa Ngeleja, japokuwa ikifikia hapa chama kitakuwa
kinajimaliza chenyewe.
Nini kinaweza kumwangusha?
Ngeleja ana taswira ya kukosa uadilifu na hivyo ndivyo ilivyo.
Alipokuwa Waziri wa Nishati na Madini, wizara yake iliendelea kutuhumiwa
kufanya “madudu” mengi sana.
Alishindwa kuwasimamia watendaji wa Tanesco na
mashirika mengine yaliyo chini ya wizara yake dhidi ya ubadhirifu mkubwa
ambao ulikuwa unafanywa huko. Kuna wakati ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Serikali ilionyesha madudu mengi katika wizara yake na kila
yalipokuwa yanatajwa unaona mengine yangeweza kuondoshwa kwa juhudi za
waziri mwenyewe, lakini hakuchukua hatua.
Wakati wa mgawo mkali wa umeme mwaka 2011, mmoja
wa wananchi alimkejeli Ngeleja kwenye mitandao ya kijamii juu ya mgawo
wa umeme akisema “….Ni kweli tangu alipoingia madarakani msimu wa kwanza
wa 2005-2010 na sasa msimu huu wa 2010-2015 kauli yake imekuwa ni hiyo
hiyo. Na ukweli ni kwamba nampongeza sana ‘Mheshimiwa’ huyu kwani
ametekeleza ahadi yake ya kuufanya mgawo wa umeme kuwa ni historia, na
imekuwa historia ambayo inajulikana hata na mtoto mchanga”.
Mwananchi huyo aliendelea kusisitiza kuwa “….kwa
hiyo msimshambulie anatekeleza kauli yake na ahadi yake ya kufanya mgawo
wa umeme kuwa ni historia katika nchi hii. Mgawo wa umeme umeongezeka
siku hadi siku na umebaki kuwa historia, mmuelewe hivyo na kama hivyo
tena ameahidi kupigana kufa na kupona kuufanya uendelee kuwa ni
historia. Kipi kigumu hapo wakuu?”
Utendaji wa aina hii alioufanya Ngeleja kwenye
sekta muhimu kama nishati na madini utamhukumu kwenye kinyang’anyiro cha
urais bila ajizi.
Sakata la Escrow linaweza kumsababishia anguko.
Sote tunajua kuwa sakata hili lilimhusisha yeye kuchukua kiasi cha
Sh40.4 milioni kutoka kwa James Rugemalira, mfanyabiashara ambaye
alikuwa mbia katika kampuni ya kufua umeme ya IPTL. Na inatafsiriwa ni
kama vile Ngeleja alikuwa analipwa fadhila kwa kusimamia jambo fulani.
Ikumbukwe, Ngeleja aliwahi kuwa Waziri wa Nishati
na Madini katika vipindi ambavyo Tanesco na IPTL vilikuwa kwenye mvutano
mkubwa kuhusu viwango vya tozo. Huyo ndiye baadaye naye anaonekana
amepokea fedha zilizotokana na mgogoro wa sekta ambayo alikuwa
anaiongoza. Mbaya zaidi ni kwamba anapopokea fedha hizo hafuati mkondo
wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kutoa taarifa. Sakata la
Escrow linaweza kumuumiza kabisa Ngeleja kisiasa na kumuondoa miongoni
mwa watarajiwa ndani ya CCM.
Lakini pia ikumbukwe kuwa Ngeleja ni miongoni mwa
makada sita ambao walinaswa na chama wakifanya kampeni za siri na
wakazuiwa kwa miezi 12 kuanzia Februari mwaka jana. Kamati ya Maadili
inaendelea kuwachunguza hatujui kamati hiyo itakuja na uamuzi gani, hapo
napo ni mtihani kwa Ngeleja.
Asipopitishwa (Mpango B)
Ikiwa Ngeleja hatapitishwa kugombea urais ndani ya
CCM nadhani atarudi Sengerema kugombea ubunge na anaweza kushinda.
Tatizo ambalo naliona katika harakati za kurudi kwenye ubunge ni kwamba
chama chake kinaweza kumtosa kwa staili ile ile na sababu zile zile
zitakazokuwa zimemwangusha kwenye urais. Kwamba CCM itahofu kuwa na
mgombea mwenye tuhuma za kuhusishwa na Escrow na labda chama hicho
kitataka kujitutumua kwa wananchi kuwa kinapambana na ufisadi kwa
vitendo.
Ngeleja ni mwanasheria mwenye uzoefu mkubwa na
amefanya kazi serikalini na nje ya serikali, kwa hiyo, anaweza kuwa na
mchango mkubwa kwa jamii ikiwa ataendeleza taaluma yake hasa
itakapotokea kuwa CCM imemtosa kwenye urais na labda hata kwenye ubunge.
Namwona kama mwanasheria mwenye mafanikio makubwa baadaye ikiwa
itampasa kupita kwenye njia hii.
Hitimisho
Naona kama Ngeleja atakuwa na wakati mgumu kupita kwenye mchujo wa wagombea urais ndani ya CCM na ni kama vile jina lake linaweza kukatwa mapema ili kuwapisha wana CCM wengine wenye sifa zaidi waweze kuchukua jukumu hilo la kidemokrasia. Lakini pia hatujui chama hicho kitatumia mfumo gani na sifa zipi kumpata mgombea wake. Kwa lolote lile litakalojiri, naye tunamtakia kila la heri kwenye malengo yake.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment