
Baadhi ya Mitambo iliyopo katika kiwanda cha Rungwe Gesi, inayotumika
kusindika gesi inayochimbwa katika kijiji cha Ikama Wilaya ya Rungwe
Mkoani Mbeya.
Wakazi wa Kijiji cha Ikama wilayani
Rungwe wameilalamikia Kampuni ya Tanzania Oxgyen Ltd (TOL), inayochimba
gesi asilia katika eneo kwa kushindwa kuchangia huduma za jamii kwa
wananchi.
Meneja wa kampuni hiyo, Benard Matiku alikiri kuwapo kwa changamoto hiyo, akisema kwamba suala hilo liko mikononi mwa mmiliki.
Mkazi wa kijiji hicho, Sunday Hassan alisema tangu
mwekezaji huyo aanze kuvuna gesi mwaka 2012, hakuna ahadi
iliyotekelezwa na wananchi wanazidi kutilia shaka uwapo wa mwekezaji
huyo.
Hassan alisema kijiji kilimtaka mwekezaji ajenge zahanati, barabara na vyumba vya madarasa, lakini hajachangia chochote.
Mkazi mwingine, Janken Mwangomango alisema pia vijana wa eneo hilo hawajapewa ajira ili kujikomboa na umaskini.
Luciana Desa alisema hata wanawake wanaendelea kutumia kuni badala ya gesi licha ya kuwapo kwa kampuni hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Zainabu Mbuse alisema
malalamiko ya wanakijiji hao aliyapata Aprili 8, mwaka huu alipotembelea
eneo hilo. Alisema atalifanyia kazi ili wananchi wafaidike na gesi hiyo.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment