Social Icons

Pages

Friday, April 10, 2015

LOWASSA ASAIDIA WAATHIRIKA BUSEGA

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametoa msaada wa Sh. milioni tano kwa waathirika wa mafuriko katika kata ya Lamadi Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu (Nec) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, Raphael Chegeni, aliwasilisha msaada huo kwa niaba ya Lowassa. Chegeni alisema Lowassa ametoa msaada hguo baada ya kuguswa na janga hilo.
Chegeni alifafanua kuwa kiasi hicho cha fedha kilichotolewa kitanunua mafuta ya kula, unga, mchele na sukari. Wakati huo huo, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Mwanza, umetoa magodoro 50, mablanketi 70, kilo 500 za maharage na dawa za binadamu vyote vikiwa na thamani ya Sh. 500,000.
Meneja wa NHIF mkoani Mwanza, Dk. Mathias Sweya, alikabidhi msaada huo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Wilaya, Paul Mzindakaya, ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo. Dk. Sweya alisema NHIF imeguswa na janga hilo na hivyo kuamua kutoa msaada huo kwa jamii.
Aidha, Taasisi ya Mkapa Foundation na Mamlaka ya Bima Kanda ya Ziwa (Tira), walitoa misaada mbalimbali kwa waathirika hao. Akizungumza baada ya kupokea misaada hiyo, Mzindakaya aliwashukuru wote walioguswa na janga hilo na kuamua kutoa misaada kwa waathirika.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi wanaoishi mabondeni kuhama ili kuepukana na majanga ya mafuriko  mara kwa mara. Zaidi ya kaya 178 ziliathiriwa na mafuriko baada ya kunyesha mvua kubwa Jumamosi iliyopita.

CHANZO: NIPASHE

No comments: