Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
Viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali wilayani
Mbozi, Mbeya wameshitushwa na ufafanuzi wa hakimu kwamba kitendo cha
mtu kushawishi watu aina ya kura ya kuipigia Katiba inayopendekezwa ni
ukiukaji wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 29 ya
mwaka 1977 na kwamba ni kosa kuingilia uhuru wa mtu mwingine.
Akiwasilisha mada katika kikao cha pamoja na viongozi hao na wazee
maarufu, kati ya Kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya kilichoitishwa na
Mkuu wa wilaya ya Mbozi, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya, Rahimu Mushi,
alisema katika mjadala wa katiba inayopendekezwa yameibuka makundi
ambayo yameanza kufanya kazi ya watu wengine ikiwemo kuingilia uhuru na
haki za watu wengine.
Alisema chanzo cha makundi hayo ni tabia ya Watanzania kutopenda
kusoma ambayo imechangia hata wengi kushindwa kuisoma Katiba
inayopendekezwa licha ya kugawiwa bure, hivyo kutoa mwanya wa baadhi ya
watu kuwasomea na kuwashauri aina ya kura wanayostahili kupigia Katiba
hiyo.
Hakimu huyo alisema katika ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, inatoa uhuru wa mtu kuwasilisha mawazo yake,
lakini Ibara ya 39 kifungu kidogo cha (1) ( a na b) katika katiba
inayopendekezwa inatoa uhuru huo pia, lakini ibara ya 19 inakataza mtu
kuingilia uhuru wa mtu mwingine, hivyo kuhamasisha watu aina ya kura ya
kuipigia katiba hiyo kuwa ni kosa.
Mushi aliongeza kuwa ni vizuri wananchi wenyewe wakaisoma katiba ya
sasa na inayopendekezwa, lakini inapotokea mijadala basi waelezwe uzuri
wa katiba hizo na ubaya wake kisha waachwe wenyewe watoe maamuzi
wanayotaka.
Mchungaji wa Kanisala Baptist, Mlowo Ibrahimu Bukuku, alisema
wamepewa katiba hii ili waisome na waelimishe waumini wao inakujaje
tena wanaanza kutishiwa, wakati huko nyuma tayari watu wamesikika
wakiwaambia watu waipigie kura ya ndiyo na wengine kura ya habana.
Alisema kauli ya hakimu imekuja kama kutoa mwelekeo fulani na
vitisho kwa wachungaji na kwamba basi kama ni hivyo waanze kukamatwa
kwanza waliotangaza kuwa katiba inayopendekezwa ipigiwe kura ya hapana
ama ya ndiyo.
Awali akifungua kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ahmad Namohe,
aliwaomba viongozi wa dini kuwaelimisha waumini wao kuhusu suala la
amani katika jamii na kuacha kuhubiri chuki kwa kupandikiza maneno ya
uchochezi hasa katiba inayopendeezwa.
Aidha, aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika
daftari la wapigakura muda utakapowadia ili kuwapa nafasi ya kushiriki
katika uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais Oktoba mwaka huu
pamoja na kuipigaia katiba kura ya ndiyo au hapana baada ya tarehe
kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment