Jaji Mstaafu Mark Bomani akizungumza na wandishi wa habari kuhusu
mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya jijini Dar es Salaam jana.
Mwanasheria Mkuu
wa Serikali mstaafu, Jaji Mark Bomani ameshauri Kura ya Maoni ya Katiba
Inayopendekezwa iahirishwe na badala yake Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) iendelee kuboresha Daftari la Wapigakura.
Pia, alisema Serikali iachane na mfumo wa
uandikishaji wananchi wa Biometrick Voters Registration (BVR) kwa kuwa
ilikurupuka bila ya kufanya maandalizi ya kutosha na fedha na vifaa
havitoshi kuendeshea mpango huo. Jaji Bomani alisema jana kuwa mujibu wa Tangazo la
Rais, Kura ya Maoni itapigwa Aprili 30 mwaka huu, lakini
walioandikishwa hawazidi milioni moja.
Alisema Serikali ikilazimisha upigaji kura, itasababisha mgogoro mkubwa na manung’uniko mengi nchini.
“Hadi hii leo, uandikishaji wapigakura bado
unasuasua, zaidi ya watu milioni 20 wataweza kweli kuandikishwa katika
wiki nne zilizobaki?
“Itakuwa ni muujiza kufanya hivyo na ni Mkoa wa Njombe tu ambao wanaendelea kuandikishwa,” alisema Jaji Bomani. Alisema Tume ya Jaji Joseph Warioba ya kukusanya maoni, ilifanya kazi kwa umakini na kukamilisha Desemba 2013 na kuitishwa Bunge Maalumu la Katiba liangalie ripoti ya Rasimu Iliyopendekezwa.
“Itakuwa ni muujiza kufanya hivyo na ni Mkoa wa Njombe tu ambao wanaendelea kuandikishwa,” alisema Jaji Bomani. Alisema Tume ya Jaji Joseph Warioba ya kukusanya maoni, ilifanya kazi kwa umakini na kukamilisha Desemba 2013 na kuitishwa Bunge Maalumu la Katiba liangalie ripoti ya Rasimu Iliyopendekezwa.
Alisema Bunge lilifanya kazi yake, lakini ilikuwa
siyo nzuri, hivyo kusababisha baadhi ya wajumbe kutoka nje ya ukumbi kwa
kutofautiana. “Katiba haitegemei kura za washiriki wachache
wanaokubali ndiyo na hapana, bali kupata Katiba Mpya kwa maelewano ya
kila upande,” alisema.
Pia, alisema baadhi ya mambo mazuri yaliyomo
kwenye Katiba Inayopendekezwa yafanyiwe mabadiliko ili yatumike kwenye
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Wakati Jaji Bomani akisema hayo, tamko lilitolewa
tume hiyo na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi wake, Dk Sist Cariah linasema
upigaji wa Kura ya Maoni uko pale pale kama ulivyopangwa.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment