
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM ), Sixtus Raphael Mapunda. Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete anatarajiwa
kuzindua Jukwaa la kimataifa la vijana kutoka nchi 43 za Africa na
China lenye lengo la kudumisha urafiki ,ushirikiano wa kimaendeleo
katika Nyanja za kiuchumi ,kijamii na kisiasa.
Mkutano wa Jukwaa hilo ambalo Tanzania ni mwenyeji
wake utahusisha pia vyama vya siasa 57, wafanyabiashara vijana 32
ambao kwa pamoja watajadili ushirikiano kati ya China na bara la Afrika
katika kuleta maendeleo. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar
es Salaam Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa
(UVCCM ) ,Sixtus Raphael Mapunda amesema jukwaa hilo litafanyika kuanzia
machi 27 hadi 31 mwaka huu katika ukumbi wa Hoteli ya Ngurudoto Mkoani
Arusha
“Tunatarajia kupokea ugeni mkubwa wakati wa
mkutano wa jukwa hili, nchi 43 kutoka Afrika zitahudhuria, vyama vya
siasa 57 vitashiriki pia kutakuwa na wafanyabiashara vijana 32 kutoka
nchi mbalimbali za Africa.
Amesema Tanzania itawakilishwa na vijana 70 na
vijana wengine 50 watatoka nchini China ambapo lengo kuu ni kujadili
fursa zilizopo na jinsi ya kuzifikia kwa ajili ya maendeleo ya Vijana
wa Africa ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali
zinazojitokeza Afrika.
Mapunda ameongeza kuwa hii ni mara ya tatu ya
kufanyika kwa mkutano wa jukwaa hilo ambapo mara ya kwanza lilifanyiak
mwaka 2011 katika mji wa Windhoek nchini Namibia na kufuatiwa mwaka 2012
Beijing China ambapo walijadili uhusiano wa fursa katika biashara
utumike kwa maendeleo.
Amesema kuwa jukwaa hilo litajadili maendeleo ya
mahusiano kati ya Africa na China ,ushiriki uhusiano wa vijana katika
maendeleo na wajibu wa asasi zisizo kuwa za kiserikali katika kukuza
mahusiano na maendeleo kati ya china na Africa.
Aidha amesema mgeni rasmi katika ufunguzi wa
jukwaa hilo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh.Dr.Jakaya Kikwete ambapo ataambatana na Waziri wa mambo ya ndani wa
China, Waziri wa Biashara na Viwanda, Dk Abdallah Kigoda na Waziri wa
Nishati na Madini, George Simbachawene
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment