Kutokuwa na kitambi ndio ndoto ya watu wengi kwa
 sasa wanaojali afya zao. Kutokana na kufumka kwa maradhi mbalimbali 
baadhi ya watu wamekuwa wakihangaika kutafuta njia rahisi za kupunguza 
ama kuondoa vitambi hivyo na uzito uliopitiliza.
Wapo waliamua kukaa na njaa na wengine kutumia dawa kali wakilenga kufikia malengo yao ambayo ni kupunguza uzito. Lakini kuwa na kitambi ama ongezeko la uzito linaweza kuondolewa kwa njia rahisi sana tofauti na unavyodhani. Tena njia isiyohusisha hata chembe ya dawa itakayoweza kukuletea madhara baadaye.
Wapo waliamua kukaa na njaa na wengine kutumia dawa kali wakilenga kufikia malengo yao ambayo ni kupunguza uzito. Lakini kuwa na kitambi ama ongezeko la uzito linaweza kuondolewa kwa njia rahisi sana tofauti na unavyodhani. Tena njia isiyohusisha hata chembe ya dawa itakayoweza kukuletea madhara baadaye.
Licha ya wataalamu wengi kusisitiza kuwa kitambi 
au ongezeko la uzito ni matokeo ya ulaji mbovu, lakini ukweli utabaki 
kuwa mazoezi kwa sehemu kubwa yana nafasi kubwa ya kupunguza uzito na 
kuondoa kitambi. Profesa Christine Rosenbloom, mtaalamu wa lishe 
kutoka Chuo Kikuu cha Georgia, Marekani anasema kupunguza mafuta mwilini
 kunaendana na ulaji wa chakula bora pamoja na mazoezi ya kila siku.
“Unatakiwa kufanya mazoezi kwa muda usiopungua 
dakika 60. Kwa kufanya hivi utaweza kuondokana na matatizo ya unene ama 
mafuta tumbo,” anasisitiza.
Naye Profesa Michael Jensen wa Kliniki ya Mayo 
anasema, mazoezi ya viungo yana nafasi kubwa sana ya kuutengeneza mwili 
wako katika hali nzuri zaidi na pia kuufanya uwe mwepesi pia. Ni muhimu kuelewa kuwa unapoushughulisha mwili 
wako, unauweka katika nafasi ya kuunguza mafuta na hivyo kujiweka kwenye
 nafasi ya kuondokana na unene. Ikiwa utafanya mfululizo ni wazi mwili 
hautakuwa na mlundikano wa mafuta.
Umuhimu wa mazoezi
Wataalamu wanasema watu wengi huamini kuwa unene 
ni matokeo ya kula vyakula vyenye kalori nyingi. Hivyo kwa kupunguza 
kalori wanaamini kuwa itakuwa ni njia rahisi ya kupunguza uzito wa 
mwili.
Licha ya kuamini hivyo lakini wataalamu 
wanasisitiza kufanywa kwa mazoezi kwani ndiyo njia pekee itakayoufanya 
mwili wako kukubaliana na mpango mzima wa kupunguza hizo kalori huku 
ukiipa nafasi misuli yako kuurudisha mwili katika hali inayotakiwa. Wanasema kupunguza kalori kwa njia isiyokuwa na 
mazoezi huwaweka wahusika katika hali ya kunenepa zaidi endapo ataamua 
kurudi katika ulaji wake wa kawaida.
Kujenga misuli
Jambo la muhimu unalopaswa kufahamu unapoamua 
kuanza mpango wa kupunguza uzito na mafuta mwilini ni kujua ni nini hasa
 unatakiwa kufanya. Kuwa na malengo ndiyo jambo la msingi 
litakalokusaidia kukutia nguvu na hata kufanikiwa. Watafiti kutoka maabara ya Chuo Kikuu cha San 
Diego Marekani, waliunganisha mazoezi mbalimbali ya tumbo. Matokeo yake 
waligundua kuwa mazoezi ya tumbo yana nafasi kubwa sana ya kuikaza 
misuli inayozunguka tumbo na hivyo kurahisisha zoezi la kupunguza 
kitambi na kulifanya tumbo kuwa bapa.
Yafuatayo ni mazoezi matano muhimu katika kupunguza mafuta tumboni: Zoezi la baiskeli – Hili husaidia kukata tumbo 
sehemu ya chini na ya juu. Unachotakiwa kufanya ni kulala chali. Kisha 
chukua mikono shika kichwani kwa nyuma upande wa kisogoni. Wakati 
umelala kunja miguu yako na kisha jinyanyue hadi kujikunja mfano wa ‘c’ 
iliyolalia mgongo. Fanya hivyo mara 12 hadi 16.
Zoezi la “Sit ups’
Ukiwa umelala chini. Nyoosha miguu yako. Kisha 
nyoosha juu mikono yako. Jinyanyue na kugusa miguu yako. Fanya hivyo 
mara 20 hadi 30
Zoezi la kunyoosha tumbo
Kaa chini na nyoosha miguu yako huku ukiitanua 
hadi kufikia uwezo wako wa mwisho. Geuza kifua chako hadi uweze kuona 
upande wa nyuma yako kwa uzuri zaidi bila kugeuka mwili mzima. Fanya 
hivyo huku ukibadilisha upande. Hakikisha unafanya mara 10 kwa kila 
upande, mkono wako wa kulia uweze kuzunguka.
Zoezi kunyonga miguu
Hili ni maalumu kwa ajili ya tumbo la chini. Lala 
chali na kisha nyanyua miguu yako. Anza kuinyonga kama unavyofanya 
unapoendesha baiskeli. Fanya hivyo mara 20. Utasikia maumivu katika 
tumbo lako la chini
Zoezi la kuzungusha kiuno
Simama na kisha shika mikono yako kiunoni. Tanua miguu yako ili kusimama imara. Zungusha mwili wako kuanzia kwenye kiuno kuja juu huku ukiwa umesimama bila kugeuka. Fanya hivyo mara 20. Ukihusisha mara kumi kwa kila upande.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment