Yako baadhi ya uhusiano ambayo huwa yana vipindi vya
amani kwa kitambo kidogo na milipuko ya ugomvi kwa kipindi kingine.
Milipuko hii simaanishi kule kutoelewana kwa kawaida bali uhusiano
unaokumbwa na milipuko ya kutoelewana kwa kitu fulani kizito au ugomvi,
unakuwa mzito na wenye kuyumbisha pande zote mbili.
1. Kuchemka hadi kumwagika “The Boil Over”
Katika hali hii unaanza kuziona dalili za kuachana
kwenu kwa mbali. Labda mwenzako amekuwa akifanya au kusema vitu fulani
kwa muda mrefu na vimekuwa havikufurahishi, kila unapotaka kumpasukia
kuna kitu kinakwambia “subiri, mpe nafasi nyingine”, ndani yako unajiona
kabisa kuwa wakati umewadia sasa wa kumpasha habari yake kwa mara ya
kwanza na ya mwisho. Pia ndani yako unakuwa na utayari wa kubeba
majukumu kwa chochote utakachomwambia. Ghafla siku moja kinatokea kitu
kidogo tu, labda ni neno lililosemwa au kitu kilichofanywa na wewe au
mpenzi wako, mnagombana na kutofautiana sana na kutokana na machungu na
maumivu ya muda mrefu moyoni mmoja anaamua kuutumia upenyo huo kulitamka
neno “it’s over” (naomba tuachane) na huo unakuwa mwisho wa penzi lenu.
2. Kuachana kimlipuko
Yako baadhi ya uhusiano ambayo huwa yana vipindi
vya amani kwa kitambo kidogo na milipuko ya ugomvi kwa kipindi kingine.
Milipuko hii simaanishi kule kutoelewana kwa kawaida bali uhusiano
unaokumbwa na milipuko ya kutoelewana kwa kitu fulani kizito au ugomvi,
unakuwa mzito na wenye kuyumbisha pande zote mbili. Kwa mfano baada ya
kitambo cha amani na mapenzi kunagundulika kuwapo kwa uhusiano wa
pembeni kwa mmoja wa wapenzi (cheating) na hili linazua mlipuko wa
ugomvi ambao ghafla unalizima penzi na ule ukaribu wenu unafifia ghafla
na kutokomea jumla. Yamkini ni mlipuko mmoja tu umetokea, lakini mpenzi
mmoja aliyeumizwa hatamani hata kumwona mwenzake kwa macho, wapendanao
hawa wanajeuka maadui ghafla (one blow away).
3. Leo nje kesho ndani, kesho baridi keshokutwa moto
Hii ni staili ya kuachana ambayo wengi wetu
huitumia mara kwa mara na mara nyingine pasipo mhusika mmoja katika
penzi kufahamu kwamba safari ya kuachana ndo inawadia. Katika uhusiano
wa watu wa namna hii, kunakuwa na mazingira yanayowafanya leo
wanakorofishana kesho wanapatana, kesho wanakuwa pamoja keshokutwa
unaskia hawapo tena pamoja, mara unasikia wamerudiana, tena wanakuja
kufarakana na tabia hii inakuwa ndo maisha yao ya kila siku na mfumo wa
uhusiano yao. Tabia hii huendelea kudumu hadi inafika nyakati mmoja
akitoka basi anatoka jumla, kila mwenzake akiwaza kwamba yamkini atarudi
kama mazoea yao yalivyo lakini haiwi hivyo tena na penzi lao
linakatikia hapo.
4. Mkate ulioungua
Mara nyingi tunapopika mkate huuweka kwenye joto
kali ili uive na mara kwa mara muokaji huuangalia kama umeiva kwa
kuutumbukizia kitu kikali kama vile uma ili kuangalia hali yake ya ndani
ilivyo na kufahamu maendeleo ya uivaji wake. Mkate uliosahaulika
kuangaliwa mara kwa mara huungua na muokaji anapokuja kuutoboa ndipo
anapofahamu kuwa mambo yameshaharibika kuanzia ndani na mkate haufai
kuliwa tena.
Katika uhusiano wetu hususani kwa baadhi ya wale
walioweza kukaa muda mrefu au hata waliooana, bahati mbaya kwa sababu ya
masumbufu ya maisha ya kila siku na mapenzi ya kimazoea wakasahau
kuchochea na kuziamsha hamasa za penzi lao kila mara, penzi hilo
taratibu hushuka na kupoa ladha na taratibu pasipo wapendanao hawa
kugundua kila kitu kinakuwa chabaridi, kilichoganda, kisicho na ladha na
kilammoja akitamani penzi la ladha ya tofauti kutoka kwa mtu wa
tofauti. Hii inasasababisha wawili hawa kuchagua kuachana.
5. Ghafla moto ghafla baridi
Kama umewahi kutumia mashine ya kupashia joto
chakula “microwave” utaelewa kitu ninachojaribu kuzungumza hapa, tabia
ya mashine hii ni kupasha joto chakula kwa haraka sana na mara kikitoka
huweza kupoa kwa haraka zaidi pia. Yako mapenzi ambayo yameanzishwa
ghafla sana (kwa muda mfupi sana) na yakapaa juu sana, kila mmoja
akimhisi mwenzake kiukaribu sana, na hisia za wawili hawa zinakuwa za
moto kama zilizo wekwa kwenye ‘microwave’ lakini ghafla mmoja kati ya
wapendanao hawa anazimika na kutoendeleza tena moto uliokuwepo. Kwa
mfano mlianza ghafla kuhusiana na mapenzi yakawa moto kuliko
mlivyofikiri, kila siku mko wote na lazima muonane au muwasiliane kwa
simu, ghafla mwenzako hapokei simu na wala akiiona simu yako hawajibiki
kukupigia au kukwambia nini kinaendelea na tabia hiyo inaendelea hivyo
hivyo hadi unakata tama na unaamua kukubali yaishe.
Mapenzi haya yaliwaka na kuzima kwa mtindo wa
microwave. Wakati unahisi penzi lenu linafikia mwisho ni vyema mkafikiri
njia bora za kuachana na maranyingine ikibidi kuliongea hili kwa
pamoja. Baadhi ya zinazoweza kuwa na madhara makubwa na ya muda mrefu
kwa wahusika au muhusika mmoja na nyingine madhara yake ni madogo na
yasiyo ya muda mrefu.
Wakati wote tunashauri kuachana isiwe ndiyo njia mbadala ya
kwanza bali jitihada za kusuluhisha na kubadilika tabia ziangaliwe
kwanza na kupewa kipaumbele na kila anayehusika katika penzi.
Kumbuka kuwa katika jitihada za kubadili tabia ni
zoezi linalotakiwa kusaidiana baina ya wawili wapendanao na siyo kazi ya
mtu mmoja. Nakutakia kufanikiwa zaidi katika uhusiano yako na sio
kukimbilia kuachana.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment