Kiongozi wa Mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Fatou
Bensouda akizungumza na vyombo vya habari siku za hivi karibuni.
Wanasiasa waliotajwa na kiongozi
wa mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Fatou Bensouda
kuhusu kesi ya Rais Uhuru Kenyatta, wamejitokeza na mmoja wao amesema
upande wa mashtaka ulimtaka atoe ushahidi wa uongo.
Aliyekuwa mbunge wa Nakuru Mjini, David Manyara alisema mahakama hiyo ilimtaka awe shahidi wa upande wa ICC, lakini alikataa. “Bensouda ananitaja kwa ubaya kwa kuwa nilikataa
kuwa shahidi wa upande wa mashtaka, ingawa walitaka kunilipa Sh200
milioni ili nitoe ushahidi wa uongo kwenye kesi ya rais. “Wanasema nilikuwa nikisambaza bunduki, wakijua
sijawahi hata kugusa bunduki maishani mwangu. Mimi ni bondia na mikono
yangu ndiyo silaha yangu,” alifafanua.
Mfanyabiashara Bildad Kagai alisema inasikitisha kuwa Bensouda kumhusisha na madai ya rushwa ya mwaka 2009. “Haiwezekani kwamba ningemhonga mtu mwaka 2009, miaka mitatu kabla ya kesi ya ICC kujulikana,’’alisema. Alisema shahidi aliyetajwa kuwa James Kabutu alikuwa rafiki yake tangu mwaka 2009 na kwamba hakuwa na haja ya kumsumbua.
Naye Mwenyekiti wa Nacada, ambaye alikuwa mbunge
wa Naivasha wakati zikitokea vurugu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007,
John Mututho alisema Bensouda anataka kumfurahisha mtangulizi wake Luis
Moreno Ocampo.
“Ocampo anajua kwamba hakuwahi kumhoji John
Mututho wala aliyekuwa OCPD wa Naivasha, Willy Lugusa. Unawezaje kufanya
uchunguzi katika kesi ya kiwango cha juu namna hii bila ya kuwahoji
watu waliokuwapo? Hii siyo kanuni katika kesi za uhalifu, anapaswa
kuwahoji waliopo,” alihoji Mututho.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment