Maandamano ya kupinga shambulio dhidi ya jarida la "Charlie Hebdo"
Huenda ni ubinadamu unaotusukuma katika hali hii, kwamba baada ya
mshituko, hasira, na majonzi kuhusiana na shambulio la kigaidi dhidi ya
jarida la dhihaka la Charlie Hebdo, hata hapa ujerumani ulinzi
umeongezwa.
Msako bado unaendelea kuwatafuta ndugu wawili wanaoshukiwa kufanya
shambulio nchini Ufaransa dhidi ya wafanyakazi wa jarida la Charlie
Hebdo.
Baadhi ya magazeti yameongeza ulinzi katika maeneo yao. Hususan kwa
upande wa waandishi, ambao hapo kabla wametumia katuni za kudhihaki
zilizochapishwa na jarida hilo la "Charlie Hebdo".
Hali hiyo inakuja wakati baada ya maafisa wa usalama kufanya tathmini
yao kutokana na shambulio lililotokea nchini Ufaransa , kitisho nchini
Ujerumani pia hakujabadilika.
Hatari bado ya juu nchini Ujerumani
Hatari ya kutokea shambulio la kigaidi inaweza kuelezwa kuwa bado ni ya
juu. Hata hivyo hakuna taarifa juu ya uwezekano wa kutokea shambulio. Kuzuwia shambulio kama lililotokea nchini Ufaransa si rahisi, anaelezea
katika tathmini yake mtaalamu wa wa masuala ya uhalifu Andreas Armborst
kutoka chuo kikuu cha Leeds nchini Uingereza.
Kwa kuwa wapo magaidi, ambao wako tayari kufanya uhalifu huo,
inawezekana kabisa katika jamii yenye uhuru kuwapo na uwezekano huo, kwa
hiyo kutakuwa na mtu wa aina hiyo ambaye anaweza kuchukua hatua kama
hiyo, ameeleza Armborst katika mazungumzo na DW.
Hadi sasa ni shambulio moja tu la Waislamu wenye itikadi kali lililotokea nchini Ujerumani ambapo maisha ya watu yamepotea. Machi , 2011 Mualbania mwenye asili ya Kosovo aliwapiga risasi wanajeshi wawili wa Marekani katika uwanja wa ndege wa Frankfurt.
Hata hivyo kuna majaribio mengi ya mashambulio yaliyotokea. Majaribio hayo ama yameshindwa ama yamegunduliwa kabla. Hatari inaongezeka pamoja na ongezeko la matukio ya Waislamu.
Kundi la Salafisti ni hatari zaidi
Hususan hatari inaongezeka zaidi kutokana na kundi ambalo linaimani za kihafidhina zaidi la Salafi.
Idadi yao imeongezeka maradufu kutoka idadi inayoaminika kuwa watu
7,000. Na hasa kama wanavyoeleza wataalamu wa masuala ya usalama ni
wanaporejea kutoka katika vita nchini Syria na Iraq baadhi ya
wapiganaji. Tarakimu rasmi zinasema kuwa wako wapiganaji 600 wenye itikadi kali
katika eneo hilo la vita ambao wako katika kile kinachojulikana kama
Dola la Kiislamu.
Baadhi ya wachunguzi , kama mtaalamu wa masuala ya saikolojia na
wataalamu wanaoangalia hali ya Uislamu Ahmad Mansour anaeleza kuwa wako
Wajerumani 1,500 hadi 2,000 wanaopigana jihadi katika vita vya wenyewe
kwa wenyewe nchini Syria. Mtafiti kuhusu itikadi kali Peter Neumann kutoka chuo kikuu cha mjini
London cha Kings anatofautisha makundi matatu ya wale waliorejea, ambayo
yana uhusiano tofauti pia.
Baadhi ya wapiganaji wa jihadi ni hatari
Kiasi ya asilimia 10 ya kundi la watu hao anasema Neumann , ni hatari
sana, wana uwezo wa kuchukua hatua za kigaidi wakati wakirejea. Na hawa
ni watu , ambao kwa utaratibu jamii inapaswa kulinda dhidi yao. Ni kundi
ambalo linapaswa kufuatiliwa kwa karibu na kuadhibiwa kwa kufungwa
jela. Kundi la pili ni lile lililoathirika na kupata fadhaa na kwa kiasi
fulani kuathirika kiakili. Kundi hili anasema Neumann kuwa linapaswa
kupatiwa uangalizi wa kisaikolojia ama kiakili. Kundi la tatu anasema mtaalamu huyo kuwa ni wale wasio ridhika baada ya
kutoka Syria. Mmoja kati ya vijana hao ndugu wenye asili ya Algeria ,
ambao wanatuhumiwa kufanya shambulio dhidi ya wafanyakazi wa jarida la
Charlie Hebdo, ni wapiganaji wa jihadi wanaotokea nchini Iraq. Kabla ya
hapo mwaka 2008 alihukumiwa kwenda jela miaka mitatu, ambapo alitumikia
miezi 18. Msimamo wake haukubadilika. Inawezekana kwamba jela
imemzidishia zaidi itikadi yake kali, anafafanua mtaalamu wa masuala ya
usalama Raffaelo Pantucci kutoka London.
CHANZO: DW KISWAHILI
No comments:
Post a Comment