
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, ametoa siku
90, kwa mkandarasi kampuni ya Megha Engineering Infrastructure Limitedi
inayosambaza bomba la maji la mradi wa Mlandizi-Kimara kufanikisha
mradi huo na kupeleka ripoti ya kwa Mamlka ya Majisafi na Majitaka Dar
es Salaam (Dawasco), kwa lengo la kupata thath mini ya mradi.
Alitoa agizo hilo jana mkoani Pwani wakati akikagua miradi minne ya
Dawasco ya kusambaza maji Ruvu Juu na Ruvu Chini kufikisha jijini Dar es
Salaam.
Prof. Maghembe alisema mpaka sasa mkandarasi alitakiwa awe amelaza bomba
kilomita 20, lakini cha kushangaza mkandarasi huyo amelilaza kilomita
12 tu.Prof. Maghembe alisema utendaji kazi wa mkandarasi huyo ni mbovu na aliwagiza wabadilike na na kuwaeleza kuwa atakwenda kukagua kazi hiyo baada ya siku 90, na kama kama kazi hiyo haitakamilika ndani ya muda huo itabidi awafukuze kazi. “Tumempatia mkandarasi huyu kiasi cha Dola za Kimarekani 59,ambazo ni sawa na Shilingi bilioni 96 za kitanzani, fedha hizi Watanzania watazilipa, hivyo ni vema mkandarasi huyu afanye kazi iliyomleta,” alisema Prof. Maghembe
Kuhusu mradi wa Ruvu Juu wa kusafisha maji, Waziri Maghembe aliridhika na utendaji kazi wa mkandarasi anayejenga mradi huo na kumtaka amalizie kufunga pampu mpya ili mgawo wa maji upungue Dar es Salaam. Aidha, alimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Dawasa, Archard Mutalemwa, kuhakikisha pampu zilizokwama bandarini zinafika leo na kufungwa kesho.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment