Matembezi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), yaliyofanyika kwa siku 37 kutoka mkoa wa Geita
kuelekea Ikulu Dar es Salaam kukutana na Rais Jakaya Kikwete,
yametumbukia nyongo baada ya kuishia mikononi mwa polisi.
Wafuasi hao, Atanasi Michael, Khalid Seleman na Juma Maganga, walifanya
matembezi hayo kwa lengo la kulaani utumiaji mbaya wa rasilimali za
nchi, rushwa, kulinda ufisadi kwa kutochukua hatua dhidi ya wahusika na
uvunjifu wa haki za binadamu. Pia walitaka serikali ya Tanganyika
ifufuliwe kusambaza uzalendo kwa Watanzania.
Akizungumzia sakata la kukamatwa wanachama hao, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, alisema wanaoshikiliwa hadi jana jioni ni sita. Alieleza kuwa baada ya chama kupata taarifa za kukamatwa wanachama hao, walituma makamanda sita kwenda kuwawekea dhamana lakini cha ajabu waliswekwa rumande bila kusikilizwa. “Tumewatuma wanasheria wa chama kufuatilia kinachoendelea na namna ya kuwasaidia” alisema Makene.
Watembezi hao waliofuata nyayo za mwanapinduzi Seth Benjamin aliyetembea kutoka Arusha hadi Dar es Salaam, kuunga mkono Azimio la Arusha lakini akafariki dunia, walikuwa wamevalia magunia pamoja na bendera za Tanganyika na Tanzania huku wakisindikizwa na wafuasi wa Chadema waliokuwa na bendera za chama. Baada ya kuwasili Ubungo, walipokelewa na polisi waliowataka waende kwanza kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana.
Watu hao walitii agizo hilo na kuanza safari kuelekea Magomeni huku wakisindikizwa na polisi na baada ya kufika ofisi ya Rugimbana, walipotakiwa kutoa vibali vya kuelekea Ikulu, hawakuwa navyo. Kutokana na watu hao kukosa vibali, Rugimbana aliwashauri, wafuate utaratibu wa kuvishughulikia au wasubiri Ikulu itaarifiwe lakini walikataa na kuanza safari kuelekea kwa JK.
Wafuasi hao waliishia mikononi mwa polisi na kupelekwa kituo cha Magomeni, mita chache baada ya kutoka ofisi ya Rugimbana. Mmoja wa watu hao, Khalid alisema hakuna agizo la kisheria la kutaka watu wanaofanya matembezi ya amani kuwa na ruhusa ya kiserikali. Aidha alisema kwa mujibu wa ratiba yao,walitakiwa kuwa viwanja vya Ikulu.
Hata hivyo, Rugimbana, alisema matembezi hayo sio halali na kwamba kumuona Rais ni haki ya Mtanzania yeyote lakini walipaswa kufuata sheria. Alisema na kuongeza watalifanyia kazi suala hilo na kuwapa nafasi ya kujieleza na kusikia madai yao.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni , Camilius Wambura, alipohojiwa na NIPASHE Jumamosi, alipingana na Makene kuwa polisi ilikamata makamanda watatu waliokwenda kuwawekea wenzao dhamana. Alieleza kuwa walioongezeka ni wawili ambao ni wanachama waliokuwa wamewasindikiza wenzao kutoka mikoa ofisini kwa Mkuu wa Wilaya. “Wanahojiwa na taratibu za kisheria zitafuata.” alisema.

CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment