
Dk. John Magufuli.
Serikali imewaagiza wakandarasi kukamilisha ujenzi
wa barabara ndogo zote za jijini Dar es Salaam kwa kiwango cha lami
kabla ya Aprili mwaka huu katika harakati zake ya kupunguza msongamano
wa magari.
Waziri wa Ujenzi, Dk.John Magufuli, alitoa agizo hilo jana jijini
Dar es Salaam wakati wa ziara ya kuweka jiwe la msingi katika shule sita
za msingi zilizopo jijini na kusema kazi hiyo imetengewa bajeti ya Sh.
bilioni 56.323 katika bajeti ya mwaka 2015.
Akiweka jiwe la msingi katika barabara katika Shule ya Msingi
Ubungo Msewe, Makuburi na eneo la Kigogo Polisi, Kinyerezi na Goba
Tangibovu jana, Waziri alisema barabara hizo zimekamilika kwa asilimia
12 katika hatua za awali.
“Barabara hizo ni zile ambazo ziko chini ya Wakala wa Barabara
(Tanroads) na katika bajeti ya 2015, serikali imetenga Sh. bilioni 16
kwa ajili ya barabara ndogo zilizopo katika manispaa zake zote,
Kinondoni milioni 10.4 Temeke bilioni 1.8 na Ilala bilioni 4.4,” alisema
Dk. Magufuli.
Barabara zilizowekwa msingi jana ni ya kutoka Ubungo Msewe-Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 2.6 ya Ubungo
External-Kilungule inayoungana na Tabata Kimanga, kilomita tatu, Tabata
Dampo-Kigogo kilomita 1.6, Mbezi mwisho- Goba Matangini kilomita 16. Aidha, Dk. Magufuli alisema serikali imetenga trilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kuu za Jiji la Dar es Salaam.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment