
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
Dk. Richard Sezibera, ameipongeza Tanzania kwa kutaka kujiunga na mfumo
wa kutumia hati moja ya kusafiria ya kitalii.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Jumuiya hiyo
jijini hapa juzi, alisema jitihada ya Tanzania kujiunga kwenye mfumo
huo ni za kupongezwa.
Alisema amefurahi kuona Tanzania imeanza kuonyesha nia katika suala hilo kwa kuwa itarahisisha usafirishaji wao bila usumbufu. Dk. Sezibera alisema kwa sasa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda zimeanza kutumia hati hiyo na kurahisisha usafiri. Aidha alipongeza nchi za Tanzania na Rwanda kwa kuimarisha uhusiano wake kwa kuendeleza mazungumzo ya hatma ya reli watakayoitumia kwa nchi hizo.
Kuhusu uchaguzi mkuu nchini Burundi, alisema anatarajia itamaliza salama na kwa usalama kutokana na serikali kujiandaa ipasavyo na hata kwa Tanzania utapita salama.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment