 
Chini ya wiki moja tangu pale Wasri Lanka walipomchagua rais mpya 
Sirisena Papa Francis amewasili katika nchi hiyo yenye waumini wengi wa 
Kibudha jana Jumanne, akianza ziara ya wiki nzima.
Katika wakati wa kampeni ya uchaguzi nchini Sri Lanka , jamii ya waumini
 wa Kikristo nchini humo ilivutiwa na wagombea wote rais wa zamani 
Mahinda Rajapaksa na mrithi wake Maithripala Sirisena. Wadadi wanasema 
kanisa Katoliki linaweza kuwa daraja la kuleta ukaribiano kati ya jamii 
hasimu za Wasinhale ambao ndio wengi na Watamil. Wakati wote ambapo mbio za kuelekea uchaguzi zilivyokaribia, wagombea 
hao wawili walipambana kuweza kupata kura za Wakristo. Mwezi Novemba 
mwaka 2014, wafuasi wa Rajapaksa waliweka mabango kote nchini yakionesha
 kiongozi wao akiwa na papa Francis. Rajapaksa na Sirisena pia 
walihudhuria mkutano wa maaskofu wa Kikatoliki mapema mwezi Desemba 
kuonesha kuunga kwao mkono Wakristo. Lakini kundi la Wakatoliki halina nia ya kuhusishwa na kambi zote mbili.
 Pia wameonya kuhusu mgawanyiko katika ziara ya papa Francis, iliyokuwa 
ianze kuanzia jana Januari 13 hadi 15.
Rajapaksa achafuliwa
Mwaka mmoja uliopita , mkutano wa maaskofu ulitoa ushahidi wa kuchafua 
dhidi ya sera za Rajapaksa ambazo alizitumia baada ya kumalizika kwa 
vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochukua miongo kadhaa. Desemba mwaka 
2013, mkutano huo ulitoa wito wa maridhiano na ujenzi mpya wa taifa 
hilo, "mageuzi ya msingi" na kurejea katika kile ilichokiita "utawala wa
 sheria". Kuanzia mwaka 1983 hadi 2009, wapiganaji wa Kitamil walitaka kujitenga 
walipigana kupata uhuru wa eneo lao katika upande wa kaskazini na 
mashariki mwa nchi hiyo. Mzozo huo wa kijeshi ulimalizika kwa kushindwa 
kwa waasi , na kusababisha kiasi ya watu 80,000 ahadi laki moja kupoteza
 maisha. Wakristo Wakatoliki ni asilimia sita ya wakaazi wote wa Sri Lanka 
wapatao milioni 21. Wakatoliki wanapatikana kutoka jamii zote za 
Wasinhale waliowengi na Watamil ambao ni wachache. Kanisa Katoliki linaweza kuchukua jukumu muhimu katika wakati huu na pia
 kutokana na ukweli kwamba ni taasisi pekee yenye ushawishi ambayo 
inawawakilishi katika jamii zote.
Papa anatafuta amani 
Kanisa la Sri Lanka limeweka wazi kwamba papa anatafuta amani," 
mwanasayansi ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Heidelberg na mtaalamu wa 
masuala ya Sri Lanka Radu Carciumaru amesema. "Anakuja kukutana na Wasri Lanka , ambao ni Wasinhale, Watamil, Wabudha na Waislamu. "Ni tukio la kiroho,"ameongeza. Lakini miaka mitano baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa 
wenyewe, hali ya kisiasa katika taifa hilo la visiwani inaendelea kuwa 
ya wasi wasi. "Bado kuna hali ya juu ya kutoaminiana katika maeneo ya zamani ya vita ,
 hususan katika eneo la kaskazini lenye shughuli nyingi za kijeshi. Hali
 hii inafanya kutokuwa na uwezekano wa kurejea katika maisha ya kawaida,
 amesema Carciumaru, akiongeza kwamba serikali iliyopita haikufanya 
lolote kubadilisha hali hiyo. " Mtu anaweza hata kusema serikali ya 
Rajapaksa imezuwia juhudi za uchunguzi wa uhalifu wa kivita uliofanywa 
na jeshi lake. Wakati huo huo, mamia ya wapiganaji waasi wa Kitamil wa 
zamani bado wanaendelea kubaki magerezani. Papa Francis anatarajiwa kutoa wito tena na tena wa amani, hususan 
wakati mzozo huo wa kikabila kati ya Wasinhale walio wengi na Watamil 
ambao ni wachache sio suala pekee linalowatenganisha kijamii watu wa 
nchi hiyo. Wabudha wenye msimamo mkali wanachochea ghasia na kuchokoza 
makundi mengine ya kidini, hususan Waislamu pamoja na Wakristo wa 
madhehebu ya kiinjili ambao inawashutumu kwa kufanya kazi za 
kimisionari, amesema Carciumaru. Nafikiri Sri Lanka bado iko mbali mno na kupata mtazamo wa pamoja. 
lakini hapa ndio kanisa Katoliki linalokuwa muhimu. Hii ni mifano kadhaa
 ya vipi juhudi zinazoelekezwa na kanisa zinavyoonekana, hususan katika 
ngazi hii. Pamoja na hayo , kanisa linaunga mkono kwa dhati elimu na 
linahusika katika kazi za hisani , ambazo zote zinasaidia kuimarisha 
jamii ya Sri Lanka. Ziara ya Papa Francis itasaidia kuonesha juhudi hizi
 zote.
CHANZO: DW KISWAHILI
 

No comments:
Post a Comment