Afisa Habari mpya wa timu ya Yanga Jerry Muro
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba Klabu
ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imemtangaza rasmi Kocha Hans van
Pluijm kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo akisaidiwa na Boniface Mkwasa kama Kocha Msaidizi.
Kuanza kazi kwa makocha hao kunahalalisha kutimuliwa kwa makocha Wabrazil ambao ni Marcio Maximo na Leonado Neiva. Aidha Taarifa za ndani ya kikao hicho zimeeleza
kuwa Yanga imeamua kutangaza pia viongozi wapya kwa lengo la kuziba
nafasi zilizokuwa wazi na kuimarisha maeneo yaliyokuwa yanasuasua.
Baadhi ya viongozi waliojiunga na timu hiyo ni Dr
Jonas Tiboroha nafasi ya Katibu Mkuu, Jerry Muro Afisa Habari, Omari
Kaya Afisa Masoko, Frank Chacha Mwanasheria na Baraka Deusdedit anakuwaM kuu wa Idara ya Fedha.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment